Watu zaidi wameendelea kutoroka mji wa Bujumbura            nchini Burundi baada ya kuongezeka kwa mapigano.
        Jumatano, watu wanne waliuawa katika mitaa miwili ya            mji huo mkuu. Maafisa wa serikali wanasema wawili waliuawa            kwenye ufyatulianaji wa risasi kati ya makundi ya watu wenye            silaha na maafisa wa polisi usiku.
        Mtu wa tatu aliuawa na watu wenye silaha, ambao polisi            wamesema walikuwa waasi. Bado haijabainika ni nini kilichomuua            mtu wa nne.
        Mauaji yamekuwa yakitokea nchini Burundi tangu Aprili            baada ya kuanza kwa maandamano ya kupinga hatua ya Rais Pierre            Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
        Rais huyo ameahidi kuwasaka na kuwaadhibu            wanaosababisha mauaji hayo.
        Mitaa ya Mutakura na Cibitoke ilifahamika sana kwa            maandamano ya kupinga hatua ya Bw Nkurunziza kuwania urais            tena.
        Aliapishwa mwezi Julai kwa muhula wa tatu, ambao            wapinzani wake wanasema ni kinyume na katiba
        Tangu wakati huo, visa vimekuwa vikiripotiwa vya            mauaji ya wafuasi na wapinzani wa serikali.
        Rais huyo amewapa watu wenye silaya makataa ya hadi            Jumamosi kuzisalimisha la sivyo maafisa wa usalama watatumia            kila njia kusitisha mapigano hayo.
        Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura Prime Ndikumagenge            anasema wengi wa wanaotoroka makwao walionekana wamebeba            godoro na nyungu za kupikia wakiondoka.
        Baadhi wanasema wanahofia yatakayojiri baada ya            makataa hayo ya rais kupita Jumamosi.
        
0 comments:
Post a Comment