Waandishi wa habari                wakitembelea katika eneo la ujenzi huo.
                        Picha                zote na Philemon Solomon-Fullshangweblog.
        ..................................................................................................
        Na Philemon Solomon                  Fullshangweblog
          SHIRIKA la Nyumba la                  Taifa (NHC) lazindua mauzo ya nyumba                  katika mradi wake mpya wa Seven Eleven (711) ulioko Kawe                  ,ambapo ujenzi huo ulianza Januari 2015.
          Akizungumza na                  waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi                Mkuu wa Shirika la Nyumba la                  Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando                  Mchechu alisema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa                  kukamilika ifikapo Desemba 2018 ,ikiwa ni takribani                  miezi 48 baada ya kuanza ujenzi. Mradi huo una ukubwa wa                  mita za mraba 111,842.90 ambao unatarajiwa kugarimu                  kiasi cha zaidi ya Sh 187, 927, 105,500 mpaka                  utakapomalizika .
          Pia                  ikumbukwe kuwa mradi huu ni seemu ya mji mpya wa kisasa                  (Satellite City) unajengwa hapa ,mradi huu upo katika                  eneo tulivu la Kawe Jijini Dar es Salaam ambalo liko                  mita chache kutoka fuko za bahari ya Hindi pia karibu na                  maeneo muhimu kama Mbezi Beach, Masaki, Oysterbay,                  Morocco na Mikocheni mradi huu una jumla ya nyumba 422                  za kuuzwa zilizopo kwenye majengo nane tofauti ya                  ghorofa 18 kila moja, ukiwa na huduma zote muhimu za                  kijamii.pia kutakuwepo na seemu ya maduka makubwa kwa                  ajili ya wakazi na maeneo ya jirani"Alisema Mchechu.
        
0 comments:
Post a Comment