Zaidi-ya wanafundi 50,000          watashindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu kutokana na          kushindwa kupata mikopo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya          Juu (HESLB).
        Hayo yamebainika ikiwa ni siku          tatu tangu HESLB kutoa majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata          mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016, huku idadi kubwa ikiwa          haimo katika majina hayo.Katika mwaka huu wa masomo bodi ya          mikopo imeweza kuwapatia mikopo wanafunzi 12,000 pekee sawa na          17.1% ya waombaji zaidi ya 70,000, hivyo kufanya idadi ya          wanafunzi waliokosa mikopo kufikia asilimia 82.9 ya waombaji          wote.
        Wanafunzi waliokosa mikopo ya          kuwawezesha kujiunga na elimu ya juu na hivyo wazazi wao          kutakiwa kugharamia elimu hiyo wameelezea kusikitishwa na hali          hiyo huku wakiitaka serikali kuwaangalia kwa jicho la kipekee          kwani hawana uwezo wa kuanza masomo pasipo kufadhiliwa na          serikali.
        Wanafunzi hao walionekana kukata          tamaa ya kutimiza ndoto yao ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu,          wamefika makao makuu ya bodi hiyo huku wakiongozana na baadhi ya          viongozi wa serikali ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es          Salaam (UDSM) kutaka kujua hatima yao.
        Nimetokea Tabora, wazazi wangu          walinipa Sh. 100,000 ya kutumia wakiamini tunapewa mikopo na          serikali, lakini tumenyimwa na hatujui hatima yetu, nimebakiwa          na Sh. 6,000, naomba serikali ituhurumie, isikie kilio chetu          hatustahili kuteseka hivi,?-ameeleza Abdul Omary mwanafunzi          mteule UDSM.Fatuma Bakari, mwanafunzi mwingine kutoka UDSM,          amesema:-
        Siwezi kujiunga na Chuo bila          mkopo, tumefika hapa ili kuomba bodi ya mikopo itusaidie hatuna          tumaini lolote zaidi ya kuomba Mungu atusaidie tuweze kupata          mikopo na kuanza masomo.
        Waziri wa Mikopo serikali ya          wanafunzi (Daruso), Shitindi Venance ameeleza kutokukubaliana na          majibu waliyopewa na uongozi wa juu wa bodi ya mikopo kwani          yanakatisha tamaa na kuzima ndoto za wanafunzi wa masikini          kusoma chuo kikuu.?Hapa UDSM ni wanafunzi 600 tu waliopata          mikopo kati ya wanafunzi 7,000 waliopangiwa kuanza masomo, hili          ni janga kubwa kwa watoto wa masikini kwani hawawezi kujisajili          chuoni wala kupata makazi katika mabweni mpaka walipe ada na          wengi wametoka mikoani.
        Tunachukua hatua moja mbele na          kuamua kulifuatilia suala hili kwa katibu mkuu wa wizara ya          elimu na katibu mkuu wa wizara ya fedha kwa sababu bodi bado          wanasisitiza tuwe na subira ilihali muda umeenda na wanafunzi          wanateseka ameeleza Shitindi.
        Mkurugenzi wa Habari, Elimu na          Mawasiliano wa HESLB, Omega Ngole amewaambia wanahabari          waliofika ofisini kwake kuwa bodi haistahili kulaumiwa kwani          serikali kupitia wizara ya fedha na wizara ya elimu ndio yenye          uwezo wa kutenga kiasi cha fedha kulingana na mahitaji ya wakati          husika.
        Lengo la bodi ya mikopo ni          kuwawezesha wanafunzi wa vyuo vikuu kusoma kwa ufadhili wa          serikali na wala sio kuwakwamisha, tunaendelea kujadiliana na          serikali kuona kama itatuongeza fedha ili tuweze kutoa awamu ya          pili ya majina ya wanafunzi waliopata mikopo, tunawaomba          wanafunzi wavute subira,?-anaeleza NgoleHata hivyo Ngole amesema          hawezi kusema lini watatangaza majina ya awamu ya pili kwani          hilo linategemea ni lini serikali itatoa fedha kwa ajili ya          wanafunzi wa awam ya pili.
        Katika mwaka uliopita wa masomo          2014/2015 serikali ilitoa mikopo kwa wanafunzi 30,000 sawa na          51.7% ya waombaji wote 58,000 na hivyo kufanya waliokosa mikopo          kuwa wanafunzi 28,000 sawa na 49% pekee tofauti na mwaka huu          ambapo waliokosa wamefikia asilimia 82.9
        Chanzo: Mpekuzi blog
        
0 comments:
Post a Comment