Wapiganaji wa Islamic State (IS) wamesema wamewaua mateka wawili, raia wa Norway na raia wa Uchina.
Kundi hilo la IS halikutoa maelezo zaidi kuhusu ni wapi au lini Ole Johan Grimsgaard-Ofstad, 48, kutoka Norway na Fan Jinghui, 50, kutoka Uchina waliuawa. IS walikuwa vikombozi kutoka kwa mataifa hayo kuwaachilia huru mateka hao.
Waziri mkuu wa Norway Erna Solberg amesema hakuna sababu zozote za kutilia shaka tangazo la wapiganaji hao, na kutaja kitendo chao kuwa "unyama".
Wizara ya mashauri ya kigeni ya Uchina imesema imeshtushwa sana na mauaji hayo.
Jarida la IS la Dabiq limechapisha picha ambazo linadai zinawaonyesha wawili hao wakiwa hao na baada yao kuuawa. Wanaonekana kana kwamba walipigwa risasi.
Msemaji wa wizara ya kigeni ya Uchina Hong Lei amesema kupitia taarifa kwamba tangu raia huyo akamatwe, taifa hilo limekuwa likijaribu kadiri ya uwezo wake kumuokoa.
Wapiganaji hao walikuwa wametangaza kutekwa nyara kwa wawili hao kwenye nakala ya awali ya jarida lao la Dabiq.
BBC.
0 comments:
Post a Comment