November 19, 2015

  • NSSF YAWAFATA WAKULIMA MASHAMBANI MKOANI MBEYA



    NSSF YAWAFATA WAKULIMA MASHAMBANI MKOANI MBEYA
    SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)  limeanza  kampeni  ijulikanayo kama NSSF Kwanza ambayo itafanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, Kampeni hiyo imeanza kwa kuwafikia wakulima kwenye vijiji vyao na Mashamba yao  Mkoani Mbeya ili kuweza kuwapa elimu juu ya hifadhi ya jamii na faida zake.

    Kampeni hiyo imeanzia kwenye Kijiji cha Iyumpi wilayani Mbozi ambako wakulima wa Kahawa zaidi ya 44 wamejiunga na NSSF. Pia Kampeni hiyo inatarajia kwenda Wilayani Ileje, Vijiji vya Mloo na Igamba.

    NSSF inaendelea kuwasihi Wakazi wa Mbeya na Vitongoji vyake waendelee kujiunga na NSSF ili waweze kujipatia Mafao bora yakiwemo Bima ya Matibabu bure kwa Mwanachama na familia yake.
    Wakazi wa Kijiji cha Itumpi wilaya ya Mbozi wakiwa wamekusanyika ili kusikiliza elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima kupitia Mpango maalumu wa Wakulima Scheme kwenye kampeni inayoendeshwa na NSSF ijulikanayo kama NSSF Kwanza.
     Afisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF,  Salim Kimaro akitoa elimu kwa wakazi wa kijiji cha Itumpi Wilaya ya Mbozi juu ya mpango wa Wakulima Scheme .
     Wakulima wa Kijiji cha Iyumpi wakisikiliza kwa makini maelezo yanayotolewa na wafanyakazi wa NSSF juu ya huduma zitolewazo na NSSF .
    Maafisa Matekelezo  Mkoa wa Mbeya wakitoa elimu jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga na NSSF kwa mmoja wa wakulima wa Kijiji cha Iyumpi.
    Gari maalumu la matangazo la NSSF likiwa limefungwa mitambo ya matangazo ambalo hutumika kuzunguka mitaani na kutoa matangazo kwa wakazi wa vijiji mbalimbali vya mkoa wa Mbeya.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.