Wakati tukizisubiria saa chache zijazo ili kuifikia November 5,2015 kwaajili ya kushuhudia tukio la kitaifa la kuapishwa kwa rais mteule wa Tanzania kwa awamu ya tano DK. John Pombe Magufuli,nakusogezea hii stori kutoka kwa aliyekuwa mgombea urais nchini kupitia chama cha "CHAUMA" Hasheem Rungwe ambaye amepanga kufungua kesi mahakama kuu ili iweze kutoa tafsiri ya nguvu ya tume ya uchaguzi kutohojiwa au kupelekwa mahakamani.
'Mahakama itupe tafsiri ya sheria, wanamaana gani kwa kutuzuia kuihoji tume.? Demokrasia haikubaliani na hali hii, watu lazima waende mahali na vyombo vyenye mamlaka kutoa maamuzi viseme, hatuwezi kukaa kimya' – Hasheem Rungwe
'Sisi tunaenda mahakamani, kuomba mahakama iingilie kati ili watu wajue na tupate majibu" ;-Hasheem Rungwe
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Hasheem Rungwe
0 comments:
Post a Comment