Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

Showing posts with label Tangazo. Show all posts
Showing posts with label Tangazo. Show all posts

July 01, 2014

  • Public Notice - Fraud Email Circulation.



  • June 30, 2014

  • KITAA WEAR (DUKANI)




    KITAA WEAR (DUKANI)
     Kama umependa KITAA wear
    Niibox ili nijue vitu vifuatavyo

    1. Namba ya Simu
    2. Wapi Ulipo, kama upo Dar utaletewa ulipo ukiishalipia
         mkoani tutatuma kwa njia ambayo kwako ni rahisi kukufikia
    3. Aina ya T-Shirt , kwenye advert nimeweka number chagua number ya
    tshirt uliyoipenda
    4. Size
    5.Price 20,000/=

    Payments through Mpesa 0754310202
    NB: Ukinunua kuanzia T-Shirt 5 bei ni 18,000/= T-Shs
    Pia gharama za kutuma mzigo mkoani ni za mteja
    Dar es salaam napatikana jengo la science na technology (Kijitonyama)
    Aksanteni sana

    For more information visit my blog www.kitaawear.blogspot.com


  • NYAMA CHOMA FESTIVAL INVITE


    NYAMA CHOMA FESTIVAL INVITE



  • KITAA WEAR (DUKANI)


    KITAA WEAR (DUKANI)
     Kama umependa KITAA wear
    Niibox ili nijue vitu vifuatavyo

    1. Namba ya Simu
    2. Wapi Ulipo, kama upo Dar utaletewa ulipo ukiishalipia
         mkoani tutatuma kwa njia ambayo kwako ni rahisi kukufikia
    3. Aina ya T-Shirt , kwenye advert nimeweka number chagua number ya
    tshirt uliyoipenda
    4. Size
    5.Price 20,000/=

    Payments through Mpesa 0754310202
    NB: Ukinunua kuanzia T-Shirt 5 bei ni 18,000/= T-Shs
    Pia gharama za kutuma mzigo mkoani ni za mteja
    Dar es salaam napatikana jengo la science na technology (Kijitonyama)
    Aksanteni sana
    For more information visit my blog www.kitaawear.blogspot.com












  • Taste Of Tanzania:Morden Swahili Recipes For The West ON SALE NOW!!



    Taste Of Tanzania:Morden Swahili Recipes For The West ON SALE NOW!!

    "To my Muslim Community, a blessed month of Ramadhan to you and your families; May the Spirit of this special month illuminate your homes and your souls" 
    For those in USA, Taste of Tanzania has reduced the price of Pilau Masala for this month of Ramadhan. Its time to stock for Eid-Ul-Fitr. http://www.amazon.com/gp/product/B00G2U1NW6/
    In Addition coming just on time for Eid-Ul-Fitr, Taste of Tanzania: Modern Swahili Recipes For The West, cookbook is now Available at Amazon World-wide. Check Amazon in your country. Also in USA you can get at Walmart and Barnes and Noble Online or ask your nearest store. Now on sale at Amazon USA http://www.amazon.com/dp/0988735903/ 
    Thank you Miriam Kinunda Author of Taste of Tanzania Cookbook


  • RATIBA YA RAMADHAN LEICESTER UK


    RATIBA YA RAMADHAN LEICESTER UK
    Assalaamu Alaykum,
    Jumuia ya Kiislamu ya An Noor ya Leicester Uingereza inapenda kuwatakia
    Waislamu wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
    Allah akujaalieni nyote afya na nguvu za kutekeleza ibada nyingi zaidi ndani Ya Mwezi huu Adhimu. Pia awape Shufaa ndugu zetu wenye matatizo ya Kiafya na mengineyo. Amin

    Jumuia ya An Noor inapenda pia kuwatangazia Waislamu wenzao waishio Leicester Na vitongoji vya karibu kuwa Programu ya Ramadhan InshaaAllah
    Itaendelea kama kawaida mwaka huu kwa utaratibu wa Kawaida.
    Kila Jumamosi na Jumapili kutakuwa na Darasa za Mwezi wa Ramadhan
    Kuanzia Saa Moja na Nusu jioni katika jengo letu 170a Belgrave Gate LE1 3XL Leicester
    Baada ya hapo tutakuwa na Futari ya pamoja.
    Kama kawaida kila Familia itashiriki katika kuleta futari
    Kadhalika kila Familia inakumbushwa kuchangia £5 kila wiki kwa ajili ya Maandalizi.
    Programu InshaaAllah itaanza Jumamosi 5/7/2014.
    Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na hawa wafuatao:

    Malik 07983614261 au ust Farid 07792174408
    au tutumie email: madrasatulnoor.01@gmail.com
    Kullu Am Wa Antum Bikhayr


    Mohammed Omar, 
    Mwenyekiti wa Jumuia 


  • June 28, 2014

  • AIRTEL YAZINDUA SIMU MPYA AINA YA IPHONE 5S



    AIRTEL YAZINDUA SIMU MPYA AINA YA IPHONE 5S
    Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo (kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.
    Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo ( kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.
    Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati Kampuni ya Airtel kwa kushirikiana na Apple ilipofanya uzinduzi wa simu mpya ya iPhone 5s pamoja na ofa kabambe kwa wateja wa Airtel, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ofa hiyo itawawezesha wateja wa Airtel kupata sms 5000, muda wa maongezi dakika 1500 pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB. Wanaoshuhudia ni Meneja Masoko wa Airtel, Prisca Tembo ( wa pili kulia) na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja wa kampuni ya Apple.

    Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.

    ·Ni kampuni ya kwanza ya mawasiliano nchini kuingia mkataba wa ushirikiano na Apple

    KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma bora na nafuu leo imetangaza ushirika wake na kampuni kubwa inayotengeneza simu za mkononi ya Apple.

    Airtel imeweka historia kwa kuwa kampuni ya kwanza ya mawasiiliano nchini Tanzania kuingia mkataba na Apple kupitia simu ya iPhone S5.

    Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu huo jijini Dar es Saalam Meneja Masoko wa Airtel Bi Prisca Tembo alisema" leo tunazindua  simu ya iPhone 5s na kuwapatia wateja wetu ofa kabambe ya vifurushi vya muda wa maongezi , ujumbe mfupi na internet. Mteja atakaponunua simu ya iphone S5 atapata kifurushi cha internet cha 3GB, dakika 1450 za maongezi na SMS 5000 kwa mwezi. Natoa wito kwa watanzania na wateja wetu kutumbelea maduka yetu na mawakala wetu ili kuweza kujipatia simu hii.

    Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano Bi, Beatrice Singano alisema "Uzinduzi huu leo utato fulsa kwa wateja wetu  kupata uzoefu tofauti wa huduma zetu na kuwawezesha  kuendelea kufurahia huduma yetu ya SWITCH on, huduma ambayo imezinduliwa ili kuwawezesha wateja wetu kupata internet yenye kasi zaidi bila kikomo kupitia mtandao wa Airtel"

    "Simu hii ya iPhone 5s itawawezesha wateja wetu pia kupiga picha, kutuma video na kuwaunganisha na marafiki na familia .

    Ili kupata maelezo zaidi kuhusu ofa hii ya simu ya iPhone 5s tembelea tovuti yawww.apple.com/phone "aliongeza mmbando.


  • RATIBA YA KOMBE LA DUNIA LEO



    RATIBA YA KOMBE LA DUNIA LEO



  • June 26, 2014

  • KUPUNGUZA UZITO KWA AFYA YAKO

     

    CLEAN 9 ni nini na ina nini??

    Ina mchanganyiko wa bidhaa nne (Alovera Gel chupa 3, Ultra Lite, Bee pollen na Garcinia. Pia ina tape measure pamoja na chupa ya kupimia)

    Ina kitabu cha muongozo wa jinsi ya kutumia.
    CLEAN 9 ni muhimu katika kupunguza mwili kwasababu inafanya kazi ya kusaidia mfumo wako wa mmeng'enyo wa chakula,kuondoa sumu mwilini,kuondoa mafuta yaliyozidi mwilini na kukupa mfumo bora wa ulaji chakula.

    Matumizi yake ni rahisi sana. Tumia bidhaa kwa usahihi kisha utahitaji kufanya mazoezi walau dakika 20 (kutembea,kuruka kamba,kukimbia au gym ukipenda), Kunywa maji ya kutosha angalau lita tatu kwa siku pungza au acha kabisa ulaji wa vyakula vyenye sukari,wanga na mafuta.
     
    Unatumia kwa siku tisa na itakusaidia kupungua kilo 3 mpaka 8 na kupungua zaidi utatumia Nutri lean ambayo ina bidhaa za mwezi mzima na una uwezo wa kupungua kilo 10 mpaka 15. Rahisi eeh??
    Wasiliana nasi kwa kupiga au watsup kwa maelezo zaidi +255 713 418 475
  • June 23, 2014

  • Sekretarieti ya Ajira Yazipa Rungu Serikali za Mitaa


    Sekretarieti ya Ajira Yazipa Rungu Serikali za Mitaa

    Serikali za mitaa zitaruhusiwa kuanza kuajiri watumishi wa baadhi ya kada za chini katika mwaka wa fedha wa 2014/2015.
     
    Akihojiwa katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, Msemaji wa Sekretarieti  ya Ajira  katika Utumishi wa Umma,  Riziki Abraham, alithibitisha kuwa Sekretarieti hiyo itakasimu sehemu ya madaraka yake ya kuendesha mchakato wa jira serikalini kwa serikali za mitaa.
     
    "Sekretarieti ya Ajira imeandaa mpango wa kukasimisha madaraka yake ya kuendesha mchakato wa ajira serikalini kwa baadhi ya kada za chini (operation staff) kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa na mchakato huo utaanza mwaka wa fedha 2014/15" alisema.
     
    Pia, alisema katika kila nafasi ya kazi inayotangazwa kwa waombaji, Sekretarieti hiyo haizingatii GPA (kiwango cha ufaulu kwa masomo yote ). Alieleza kuwa zipo kada, ambazo GPA inazingatiwa ;na zipo kada ambazo kinachoangaliwa ni ufaulu tu wa kawaida na sifa zilizoainishwa.
     
    "Zipo baadhi ya kada ambazo masharti yake ni pamoja na kuwa na GPA ya kiwango fulani. Kada ambazo ni lazima GPA kuangaliwa ni kama vile kada za wakufunzi wa vyuo mbalimbali. Kazi nyingine hazina masharti ya GPA, kinachoangaliwa ni ufaulu tu na sifa zilizoainishwa katika tangazo la nafasi za kazi kulingana na kada husika", alisema Riziki.
     
    Alitaja moja ya matatizo wanayopata waombaji wa kazi kuwa ni kupotelewa na vyeti vya kitaaluma. Alisema waombaji wa kazi ambao wamepata tatizo hilo, wanachopaswa kufanya ni kuripoti kwenye mamlaka husika, alikokuwa amepata cheti hicho ili apewe mwongozo wa kufanya na kutangaza kupotelewa kwa cheti au vyeti kwenye chombo cha  habari (gazeti).

     "Ikithibitika hivyo mamlaka husika kwa mfano Baraza la Mitihani wana utaratibu wa kuwasiliana na Sekretarieti ya Ajira kwa kutoa majina ya watu waliopoteza vyeti na hatimaye huruhusiwa kufanya usaili" alisema.


  • RATIBA YA KOMBE LA DUNIA 2014 LEO HUKO NCHINI BRAZIL



    RATIBA YA KOMBE LA DUNIA 2014 LEO HUKO NCHINI BRAZIL



  • June 18, 2014

  • NSSF YAHITIMISHA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE KANDA YA ZIWA



    NSSF YAHITIMISHA ZOEZI LA UPIMAJI AFYA BURE KANDA YA ZIWA

    Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), lahitimisha   kambi za upimaji wa Afya bure kwa wakazi wa kanda ya Ziwa.

    Lengo la kambi hizi zilikuwa ni kuweza kutoa elimu na  kuwahamasisha wanachama wa NSSF na wananchi kwa ujumla waweze kujenga  tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kujiwekea mfumo bora wa maisha ili kuepukana na magonjwa sugu yasiyoambukiza.

    Zoezi ambalo lilianzia mkoa wa Mara na kupata mwitiko mkubwa wa wakazi wa Mara kwa kupima watu 1582 na kufuatiwa na mkoa wa Shinyanga hususani wilaya ya Kahama ambako walijitokeza watu 700, Mkoa wa Geita ambako watu1000 walijitokeza, litahitimishwa kwa kupima wakazi wa Mkoa Kagera wilaya ya Bukoba Mjini  , kwenye Viwanja vya Mashujaa (Platform),  kuanzia tarehe 14/06/2014,  kwa siku tatu mfululizo, kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi na moja Jioni.

    HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA
    Huduma mbalimbali zitatolewa  kwenye kambi hizi zikiwemo;
      Upimaji wa Shinikizo la damu
    Upimaji wa sukari kwenye damu- Kisukari
    Upimaji wa hali ya lishe (Uwiano wa Urefu kwa Unene)
    Utoaji wa dawa za Minyoo
     Ushauri wa kitaalam kwa watakaokutwa na Matatizo
    Ushauri nasaha  na upimaji hiari wa VVU (UKIMWI)
      Kutoa vipeperushi vya Maelezo ya uboreshaji wa Afya.

    Huducma  zote hizi zitatolewa na NSSF, BURE.

    Pia kutakuwa na zoezi la uchangiaji damu kwa hiyari kwenye kambi hii ya Bukoba ambalo litaendeshwa na chama cha msalaba mwekundu.

    NSSF inaendelea kuwasii na kuwahimiza wakazi wa kanda ya ziwa kuwa waendelee kujiandikisha kwenye NSSF HIARI Scheme. 

    NSSF HIARI Scheme ni kwa ajili ya wajasiriamali wadogo, wachimbaji wadogo, Ushirika wa Bodaboda, Ushirika wa Wakulima pamoja na wanachama wa Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.

    Jiunge na NSSF HIARI Scheme ili uweze kujipatia mafao bora ya NSSF yakiwemo Bima ya Afya BURE kwa familia nzima (SHIB), mikopo nafuu ya SACCOS,  pamoja na Mafao bora mengineyo.

    Wananchi wa kanda ya ziwa wanakumbushwa na kuhimizwa kujitokeza kwa wingi ili kupimwa na kupewa ushauri wa afya zao Bure.

    NSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE.
    Banda la NSSF.
    Maofisa wa NSSF wakisikiiza kwa makini Hotuba ya Mgeni Rasmi wakati wa Ufunguzi wa Kambi ya upimaji Afya Bukoba.
    Meza kuu wakifurahi wakati wimbo wa mkoa wa Kagera ukiimbwa. Toka Kushoto, Dr.Ruta Thomas, Mganga Mkuu mkoa wa Kagera, Bw.Adoh Mapunda ,Mkurugenzi wilaya ya Bukoba, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, Mkuu wa mkoa wa Kagera, Bw.Leornard Faustine Kachebonaho, Mwenyekiti wa Chama cha msalaba mwekundu , Kagera . Dr.Ali Mtulia Meneja wa Mafao ya Matibabu –SHIB na Mratibu wa Chama cha Msalaba mwekundu mkoa wa Kagera, Bi.Robi Wambura.
    Mkuu wa mkoa Kanali Mstaafu Fabian Massawe akisisitiza jambo wakati wa risala yake ya ufunguzi.
    Dokta Ali Mtulia, Meneja wa Mafao ya Matibabu NSSF akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, watatu toka kushoto, Huku Mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dr.Ruta Thomas(wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa wilaya ya Bukoba, Bw.Adoh Mapunda(wa pili Kulia) na Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundu Kagera , Bw.Leonard F Kachebonah0 (wan ne toka kushoto) wakisikiliza kwa Makini.
    Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Masawe (katika), akikagua mabanda wakati wa zoezi la kupima afya bure kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera.
    Ofisa Uhusiano Jumanne Mbepo akimkabidhi Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe vipeperushi na Fulana alipotembelea banda la kutoa elimu kwa umma juu ya NSSF.
    Wakazi wa mkoa wa Kagera wakijiandikisha kwa ajili ya kupima afya.
    :Dokta  Ali Mtulia akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe aweze kukagua mabanda yanayotoa huduma za upimaji.
    Dokta Ali Mtulia akimuelekeza Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu, Fabia Masawe upimaji wa Uzito na Urefu ili kutambua uwiano wa uzito na urefu kwa lengo la kushauri lishe bora.
    Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Masawe, akiuliza maswali na kujibiwa na Dk.Ali Mtulia kuhusu huduma zitolewazo na NSSF.


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.