Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

Showing posts with label Udakuzi. Show all posts
Showing posts with label Udakuzi. Show all posts

July 12, 2014

  • DAKTARI FEKI MWINGINE ADAKWA HOSPITALI YA RUFAA MOROGORO



    DAKTARI FEKI MWINGINE ADAKWA HOSPITALI YA RUFAA MOROGORO
    Askari Polisi wakimtoa nje daktari feki, Karume Habibu (22) kutoka kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako alihojiwa kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano zaidi.
    Daktari feki akielekea kwenye gari.
    Daktari feki, Karume Habibu akiingizwa kwenye gari.
    Akificha uso kukwepa kamera za GPL.
    Baadhi ya wafanyakazi wa Hospital ya Rufaa ya 
    Mkoa wa Morogoro wakishuhudia tukio hilo.

    WIMBI la madaktari feki kuingia katika hospitali wakijifanya madaktari na kutoa huduma mbalimbali limeendelea ambapo leo amenaswa mwingine mkoani Morogoro.
    Daktari huyo feki aitwaye Karume Habibu (22)amenaswa katika Hospitiil ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa mahojiano zaidi.


    PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO


  • July 03, 2014

  • HATIMAYE MCHUNGAJI ANAYETUHUMIWA KUVUNJA AMRI YA 6 YA MUNGU NA FLORA MBASHA AFUNGUKA LIVE!!



    HATIMAYE MCHUNGAJI ANAYETUHUMIWA KUVUNJA AMRI YA 6 YA MUNGU NA FLORA MBASHA AFUNGUKA LIVE!!
    gwajima na mbasha

    MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima, amefunguka na kuuweka hadharani uhusiano wake na familia ya waimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha na mume wake, Emmanuel Mbasha.


    Gwajima amekuwa akitajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Flora na kwamba hatua hiyo inadaiwa kuchangia mvurugano kwenye ndoa ya wanamuziki hao.

    Mbali ya kutajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Flora, pia anatajwa kuwa nyuma ya kesi ya ubakaji inayomkabili Mbasha ambapo kumekuwa na taarifa mbalimbali zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuhusisha mchungaji huyo na zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikimuhusisha mchungaji huyo na kesi hiyo iliyoanza kutajwa Juni 17 mwaka huu.

    Akizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu sakata hilo kwenye mahojiano maalumu na gazeti hili, Gwajima akiwa katikati ya madhabahu ya kanisa lake lililopo Kawe jijini Dar es Salaam huku akiwa na wasaidizi wake pamoja na watoto wake wawili, alisema taarifa zinazoenezwa ni za kijinga na hazina ukweli wowote.
    Alisema mgogoro wa Mbasha na Flora unaonekana kuwa ni wa muda mrefu na kwamba umekuja kujitokeza kanisani kwake baada ya kuanza kufanya nao kazi ya kutoa huduma ambapo wawili hao walikuwa waburudishaji kwenye mikutano yake.

    "Nilimfahamu Flora na Mbasha mwezi wa tisa mwaka jana… kipindi hicho nilikuwa na mkutano Arusha. Wote wawili niliwaalika tukaenda nao kwenye mkutano na pindi mkutano ulipomalizika walirudi nyumbani tukaenda tena katika mikoa mingine ya Moshi, Tanga, Morogoro na Kilombero wote wawili walikuja kushiriki mikutano hii kama waimbaji na wote walirudi nyumbani kwao.
    "Nimekuwa nikiona kwenye mitandao wakisema kuwa nilikwenda na Flora peke yake katika baadhi ya maeneo kama Morogoro… si kweli, muda wote walikwenda wote wawili na walirudi wote wawili, pia sina uhusiano wa kimapenzi na Flora kama inavyodaiwa. "Kwanza watu wote waliokwenda kwenye mkutano walikuwa 300, kila mkoa walikuwa watu 300. Naamini kuna mtu ana hoja zake binafsi anataka kuudanganya umma kwamba Gwajima ana uhusiano na Flora.

    "Nataka niwakumbushe Watanzania kuwa baada ya kumaliza hii mikutano hawakuwa washirika wetu kanisani, kwa maana kuwa hawakuwa wakisali kanisani kwangu kwa sababu tuliwaalika kuja kuimba na walikuwa wanalipwa kwa sababu ya kuimba pekee," alisema.

    Aidha alisema baada ya kumaliza mikutano hiyo na kukaa kwa muda, Flora aliamua kwa mapenzi yake kwenda kusali kanisani kwake na baadaye mumewe naye akajiunga na mke wake kushiriki ibada kwenye kanisa lake. Akizungumzia suala la kuwa nyuma ya kesi inayomkabili Mbasha na kuwa amekuwa akimpatia fedha Flora ili kufanikisha dhamira ovu dhidi ya mumewe, Gwajima alisema si la kweli.

    "Hili suala la kumpatia fedha Flora ili amuangamize mume wake halina ukweli, ukweli ni kwamba baada ya Mbasha kutuhumiwa kubaka alitoweka nyumbani, mke wake hakuwa na sehemu ya kupata msaada, kutokana na hali hiyo ndipo Flora alikuja kanisani kwetu kuomba msaada wa fedha na kwa vile ni mshirika wetu tulimsaidia.

    "Nilizungumza na wachungaji wenzangu tukaona ni vyema tuitishe harambee ili waumini wamchangie kama wanavyochangia watu wengine wenye matatizo mbalimbali kwa sababu Flora alisema jamani hana fedha na mume wake amemkimbia na hana chochote, watu wakamchangai!

    "Sasa nadhani zipo fikra kwamba, Gwajima anachangisha fedha za Flora ili apate fedha za kuendelea kumshtaki mumewe, pia zipo fikra kwamba kanisa langu ndilo limemzuia Flora kurudi kwake.
    "Zikianza kusambazwa picha mbaya za Gwajima kwenye mitandao ya kijamii ili nichukue uamuzi wa kumfukuza Flora kanisani kwangu ili akapate matatizo, siwezi kumfukuza Flora kanisani kwangu wala hilo halitatokea… nimechukua hatua mbalimbali ikiwamo kumshauri Flora arudi kwa mume wake lakini alikataa mwenyewe," alisema.

    Aidha, Mchungaji huyo pamoja na kukanusha kuwa yeye sio chanzo cha mgogoro huo pia alisema hajamsomesha wala hakuwahi kutoa fedha za kufadhili masomo ya Flora nchini Uingereza.
    "Unaweza kumpeleka ng'ombe kisimani lakini jukumu la kunywa maji ni lake, akikataa ni mwenyewe, akinywa ni mwenyewe, mimi siku zote nawashauri Flora na Mbasha wawe na uhusiano mzuri, warudishe uhusiano wapatane, hata kesho (leo) nitampigia simu baba yake mzazi Mbasha na wadogo zake ili nijaribu kuwaita tena kujaribu kuona kama tunaweza kuwasaida kuwarejesha kwenye ndoa yao.

    "Hata hivyo uamuzi wa kurudiana bado utakuwa ni wa kwao wao mimi siwezi kuwalazimisha," alisema.
    Mbasha (32) alipandishwa kizimbani Juni 17 mwaka huu katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji na kusomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Wilberforce Luago.

    Akisoma mashtaka Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai mshtakiwa ambaye pia ni mfanyabiashara alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam.
    Kesi ya Mbasha inatarajia kusomwa tena Juni 17, mwaka huu kwenye Mahakama hiyo ambapo mshtakiwa huyo yuko nje kwa dhamana.
    CHANZO:MTANZANIA


  • Ridhiwani akana kujihusisha na biashara ya madawa pamoja na kumiliki magari ya UDA



    Ridhiwani akana kujihusisha na biashara ya madawa pamoja na kumiliki magari ya UDA 5_1Mbunge wa Chalinze kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete amekana kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya pamoja na kuwa miongoni mwa watu ambao wanamiliki mabasi ya UDA.


    Ridhiwani amekana hayo leo kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live kinachofanyika kila siku ya Jumatano kupitia ukurasa huo.

    Ridhiwani alisema kuwa anasikitishwa na kuumizwa na watu wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya kwa kuwa yamekuwa yakiathiri vijana kwa namna mbalimbali na pia alikana kuhusika na biashara ya mafuta na gesi pamoja na kumiliki kampuni ya mabasi inayomiliki mabasi ya UDA.


  • July 02, 2014

  • UKATILI HUU ULIOFANYWA NA MWANASHERIA MAARUFU NCHINI


    UKATILI HUU ULIOFANYWA NA MWANASHERIA MAARUFU NCHINI
    1.  Ndugu Wanahakati.
    2.  Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
    Wasalaam.
    Mtoto MELINA amakumbwa na matatizi makubwa sana. Anahitaji msaada wetu sote kama Watanzania na wapenda haki.
    Melina ambaye amelazwa katika Taasisi ya Mifupa (Moi) ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar baada ya kujeruhiwa vibaya usoni na kichwani na bosi wake YASINTA RWECHUNGURA ambaye ni mwanasheria mkubwa nchini anahitaji msaada wako.
    SIKU 730 au miaka miwili ya unyama na ukatili uliombatana na vipigo mfululizo, vimempa wakati mgumu katika maisha mtoto wa miaka 15, Melina aliyefika katika Jiji la Dar es Salaam mwaka 2012 akitokea  kijijini Ishozi- Kiziba, Kagera kwa lengo la kufanya kazi za ndani, yaani 'hausigeli'.

    Katika tukio la hivi karibuni na la kusikitisha, lilijiri Ijumaa iliyopita nyumbani kwa mwanamke huyo YASINTA RWECHUNGURA, Boko-Magengeni jijini Dar ambako Melina alikuwa akifanyia kazi.
    Binti huyo ambaye wakati anafika jijini Dar alikuwa na miaka 12, licha ya umri wake kuwa mdogo alifanya kazi kwa bidii ili mshahara wake uweze kuwasaidia wazazi wake ambao hawajiwezi kimaisha kule kijijini.
    Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika, Melina alichukuliwa na bosi wake huyo kwa makubaliano ya mshahara wa shilingi  40,000 kwa mwezi huku shilingi 20,000 zikitumwa nyumbani kwao Kagera kwa wazazi wake.
    "Lakini katika hali ya kushangaza, bosi wake alikuwa hampi zile shilingi 20,000 kama makubaliano yao yalivyokuwa akisema kwamba anamtunzia kuepuka matumizi mabaya.
    "Ikaelezwa kuwa, akiwa ndani ya kazi, binti huyo alijikuta akipata mateso makubwa kama vile kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kwa madai ya kukosa, kufanya kazi vibaya au tofauti na maelekezo," kilisema chanzo.
    Akizungumza kwa uchungu na maumivu makali akiwa hospitalini hapo, Melina anaanza kwa kusema:
    "Nimechoka sana ndugu zanguni, nimeteseka sana, nisaidieni nirudi kwetu Kagera. Kosa dogo napigwa na blenda na nyaya za kompyuta. Ndiyo maana sehemu mbalimbali za mwili hadi kichwani nina makovu kama hivi".
    "Mara hii ya mwisho nilipigwa na kwanja la kufyekea ndiyo majeraha haya. Wakati akinitesa bosi wangu alikuwa akiniambia hakuna wa kumtisha. Nisaidieni jamani, miaka miwili ya mateso  mfululizo sasa nataka kurudi kwa wazazi wangu japokuwa hawana uwezo tutaishi hivyohivyo tu. "
    Mtoto huyo ana makovu (majeraha yaliyopona) 73 kichwani na mwilini mwake ambayo yote yanadaiwa yalitokana na adhabu ya mashambulizi ya kudhuru mwili ingawa haikubainika kama ni kutoka kwa bosi wake huyo au la!
    Mnamo tarehe 11 Juni, mwaka huu (2014), saa 3 usiku, Melina alipelekwa  katika hospitali binafsi iliyopo Mbezi, Dar akiwa na majeraha makubwa kichwani. Aliambatana na wanawake watatu, Mama Betty, Mama Winnie na mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Rwechungura (Anasemekana ndiye bosi wake).
    Kwa kutotaka kuonekana kama wanahusika na huyo motto, walisema kuwa wao ni majirani wanaoishi karibu na binti huyo na walifika hospitalini hapo kwa lengo la kumsindikiza na kujua nini kinaendelea. Swali kama wao hawaishi nae bali ni majirani, je huyo anayeishi nae alikuwa wapi wakati mtoto anapata maswaibu hayo? Na kwanini hawakutaka kutoa namba zao za simu wapoombwa na daktari?
    Daktari aliyekuwa zamu usiku huo inasemekana kuwa alishtushwa na hali ya Melina kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi usoni na kichwani.
    Daktari kwa kutaka kujua zaidi kilichotokea ndipo akapasua jipu kwamba alikuwa amepigwa na bosi wake na kwamba hata makovu mengine ni majeraha yaliyopona ambayo yalitokana na kipigo cha mara kwa mara.
    Habari zinazidi kudai kuwa, daktari huyo aliendelea kuokoa maisha ya Melina kwa kumshona nyuzi karibu kumi na mbili katika maeneo yaliyopasuka  lakini kutokana na hali ya majeruhi kuwa mbaya, ilibidi aende kutoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi cha Kawe.
    "Polisi walikwenda nyumbani kwa mwanasheria huyo, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida walikuta nyumba haina mtu tena ikiwa wazi kwa usiku huo.
    "Inasemekana katika wale wanawake watatu waliompeleka Melina hospitali, mtuhumiwa alikuwepo ila alitoroka baada ya polisi kuonesha nia ya kumkamata.
    "Hali ya Melina ilizidi kuwa mbaya. Alfajiri ya Juni 12, mwaka huu ilibidi ahamishiwe kwenye Hospitali ya Mwananyamala ambapo alipokelewa na kupewa matibabu. Hali ikazidi kuwa mbaya, akahamishiwa Muhimbili.
    Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni,  Camillius Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kwamba, mtuhumiwa alitoroka lakini Jumamosi iliyopita alitiwa mbaroni maeneo ya Mbagala jijini Dar es salaam, tayari amefikishwa mahakama ya mkazi kinondoni. Kesi ya jinai namba 226/2014, itatajwa tena tarehe 1 Julai, 2014.
    OMBI:
    1.    Wanaharakati nyote mnaombwa kuhudhuria siku hiyo ya tarehe 1 Julai, 2014 ili kumtia moyo huyo mtoto nakumfariji. Mtoto anahitaji msaada wa kisheria, ikiwemo na fedha za kujikimu.
    2.    Kurudishwa shule na kupata mfadhili wa kulipia masomo
    3.    Kumchangie mama mzazi wa huyo MELINA aweze kuja hapa Dar Es Salaam ili akamuguuze mtoto wake, ili mtoto aweze kuwa na amani na utulivu kwani kwa sasa hivi ana wasiwasi mkubwa mno kwa kuwazakuwa Yule mbaya wake atamfuata hospitalini na kuweza kumdhuru
    TAARIFA ZA KUSIKITISHA
    1.    Mtuhumiwa kwa kushirikiana na ndugu zake wamemrubinu baba mtoto huyo, toka afike Dar es salaam hajawahi kuwasiliana na wajomba wa mtoto Melina ambao ndiyo yaliwasiliana na huyo jamaa kumjulisha aliyotokea huku
    2.    Inasemekana kuwa mipango inafanyika kuweza kupoteza ushaidi kwa namna yoyote iwayo. Mtoto ana wasiwasi sana na kila wakati anaomba wajomba zake wamtoe hospitali
    3.    Pia inasemekana YASINTA RWECHUNGURA kwa kutumia watu Fulani, na ambao walikwenda hospitali wakajitambulisha kwa baadhi ya madaktari kuwa wanahitaji waelewane nano (kuwaonga) ili wayamalize kimyakimya. Hapa maanake hayaeleweki. Kwa upande wa madaktari waliyoelezwa mambo hayo na ndugu zake huyo YASINTA RWECHUNGURA walikataa jambo la eti kuelewana nao. Maswali wametanda kwenye vichwa vya ndugu zake huyo motto MELINA, kuwa je, 1) usalama wa mtoto huyo utalindwa na uongozi wa hospitali ya Muhimbili? 2) Je, uongozi wa juu wa Muhimbili una taarifa hizo? 3) Je, huyo baba wa motto huyo ambaye ametoka nyumbani kagera bila kumshirikisha mamake motto ana nia njema? Kwani inasemekana mipango ilifanywa na ndugu zake YASINTA RWECHUNGURA yakumfuata huyo bwana huko kijijini na kuongea nae kutaka wayamalize.
    4.    Baba mtoto huyo amejificha au amefichwa na wabaya wa mtoto wake, swali je, nae anahusika? 1) Kwanini baada ya kupokea taarifa ya yaliyokea kwa motto wake aliamua kufanya vikao vya siri na ndgu zake YASINTA RWECHUNGURA na kuamua kutomtaarufu mke wake na kuamua kuja huku Dar es salaam kisirisiri?
    Wanahakati tunawaomba mfuatilie kwa karibu suala hili na vilevile mlisimamie MELINA awe salama na apate haki stahili yake.
    Tazama picha zake akiwa hospitali alikolazwa.
    TUNAOMBA MSAADA WENU.


  • July 01, 2014

  • BARUA KUTOKA KWA MUME WA FLORA MBASHA KWENDA KWA MCHUNGAJI GWAJIMA

     
     
     
     
    "Mchungaji ...yapata kama wiki mbili zilizopita nilihoji kupitia vyombo vya habari juu ya 'utajiri' wa ghafla wa mkewangu Mara baada ya mgogoro kutokea kati yangu na yeye, bila kupoteza muda mkewangu akanijibu kupitia gazeti moja la udaku kuwa amechangiwa fedha kiasi cha milioni 9 na waumini kanisani kwakoMchungaji, naomba uelewe kuwa nafahamu juu ya mipango yote mnayoipanga kuliko unavyodhani!! Kwanza ni kweli kuwa mlipitisha harambee ya kumchangia mkewangu, lakini kiwango kilichopatikana kilikuwa ni milioni 2 na laki tatu na si milioni tisa kama mlivyotangaza!! Lakini mlitangaza uongo huo makusudi iwe rahisi kutimiza malengo yenu ya kidhalimu mliyoyapanga juu yangu!!Mnamo tarehe 3 mwezi juni mwaka huu, mlifungua akaunti mpya kwa jina la mkewangu katika benki ya crdb morogoro, na siku nne baadae mkewangu aliingiziwa fedha kiasi cha milioni 18 kutoka akaunti ya MWANAMAPINDUZI FOUNDATION ambayo hyo accnt ipo nmb mwanza! Ambapo asasi hii inamilikiwa na mchungaji wako msaidizi Maximilian Machumu pamoja na mbunge wa viti maalumu kutoka mikoa ya kaskazini!
    Nashukuru kama ulimpa fedha hizi kwa nia ya kumsaidia, lakini hofu yangu ni kuwa kwanini kitendo hiki kifanyike kwa kificho?? Kwanini mtumie njia za siri ambazo si rahisi watu kujua kama mmempa fedha??
    Pia napatwa na mashaka zaidi kwani siku moja baada ya fedha hizi kuingizwa taarifa ya benki inaonyesha kuwa kiasi cha milioni sita cash zilitolewa na siku hiyo hiyo wapo waandishi watatu wa magazeti ya udaku ambao wanaonekana waliingiziwa fedha kiasi cha milioni moja kila mtu na aliyedeposit hizo fedha ni moja ya viongozi wako hapo kanisani!! Kuna nini hapo??
    Mchungaji, naomba tusizunguke mbuyu! Ni dhahiri shahiri kuwa umekuwa na uhusiano wenye utata na mkewangu kwa muda mrefu sasa!
    Binafsi nilianza kupata wasiwasi mwaka jana mwezi desemba tulipoenda katika mkutano wako wa injili pale morogoro! Mimi na mkewangu tulifikia hoteli ya kingsway msamvu na wewe ulifikia Nashera Hotel maeneo ya forest hill!!
    Baada ya siku tatu za mahubiri mkutano wako ulipigwa marufuku na serikali kwasababu ya maneno yakichochezi uliyokuwa unahubiri, hvyo ikatulazimu waimbaji wote turejee dar es salaam!!
    Lakini uliniomba mkewangu abaki na wewe kwani ulipanga uwe unawafanyia watu maombi pale kanisani kwako kihonda kwa muda wa siku nne!! Nilikubali na nikamuacha mkewangu nyumbani kwa dada yako pale mazimbu!! Lakini kesho yake dada yako alisafiri kwenda mwanza na ikabidi mkewangu arudi hotelini kingsway!!
    Kwaa taarifa nilizonazo na nimezithibitisha kupitia wahudumu wa pale hotelini ni kuwa mkewangu hakuwahi kulala pale hata siku moja ingawa chumba kililipiwa kwa siku zote zile!! Unaweza kunijibu alikuwa analala wapi?? Je unaweza kunieleza kwanini mkewangu alikuwa analetwa nashera hoteli na taxi kila siku usiku!! Sibahatishi katika hili kwani hata namba ya dereva taxi ninayo!!
    Yote haya nilivumilia, na hapa kati kati kuna mengi sana yametokea lakini nikajifanya mjinga nikajishusha nikavumilia kwa lengo la kulinda ndoa yangu isiharibike lakini naona wenzangu hambadiliki wala hamjishitukii sana sana mapenzi ndio yanzidi kuwa motomoto kati yenu!! Ulikuwa unategemea nivumilie mpaka lini, nijishushe kiasi gani, niwe mjinga kiasi gani Nilikuvumilia sana mchungaji lakini sasa imefika point hapana, imetosha lazima nikuondelee uvivu watanzania na dunia ikufahamu jinsi ulivyo na kitendo ulichonifanyaia na unataka kuniziba mdomo kwa kunitishia jela miaka 30!!!
    Wewe ni mpuuzi na shetani anaishi ndani yako... na nataka nikuahidi kitu kimoja kuwa NITAKUSHINDA! Najua utanisumbua sana kutokana na hela zako but at the end, I will be the last man standing!! Narudia tena, nitakushinda.!!
    Bila kusahau naomba niongee na wewe pia mkewangu, hivi ni nini kilichokukuta ndani ya moyo wako How did we get here?? Je ni fedha zilizokufanya ukengeuke kiasi hicho au kuna kingine?? Kama unanichukia mimi kiasi hiki je, uwahurumii hata watoto wetu?? Mbona tunawatengenezea mikosi wakiwa wadogo hivi?? Hivi unadhani watoto wanajisikiaje watakaposikia kuwa baba ameenda jela kwa kosa la kubaka lakini aliyechongesha muvi yote hiyo ni mama?? Hivi kisaikolojia hawa watoto watakuwaje Si watakuwa huku wanatuchukia sisi wote wawili kwa aibu na mikosi hii tunayowatengenezea Kwanini tunataka kuwataabisha watoto kwa dhambi ambayo hawajaitenda
    Yes nafahamu nimekukosea mengi and am very sory for that, lakini basi embu kumbuka mkewangu nimekuvumilia mambo mangapi mkewangu, kumbuka makosa mazito uliyonifanyia lakini nikakusamehe ni sijamsimulia hata ndugu yako ama ndugu yangu ili kulinda heshima yako!! Kumbuka jinsi tulivyopogana na changamoto mbalimbali mpaka leo hii umefikia kuwa moja ya icons wa muziki wa injili hapa nchini?? Kumbuka shida, manyanyaso, dhuluma, kuchekwa na kudharauliwa ambako tumepitia mpaka leo hii tuko hapa!!!
    Mkewangu, kwa miaka yote hii nimekubali nionekane bushoke tu huku watu hawajui kuwa mimi ndiye ninayechora ramani ya kila ishu yako!! Mimi ndiye nimekuwa nafatilia na kufanikisha kila kitu chako from scratch!!!
    Lakini nimekubali jamii inione bushoke kwani nilikuwa najua nini mimi na wewe tunatengeneza kwa maisha yetu ya sasa na baadae!!! Nini kilichokubadilisha mkewangu Fedha Au huyo mchungaji mwanamazingaombwe
    Hivi kweli kabisa umefikia hatua ya kulipa waandishi wa habari ili wanikandamize nionekane sifai katika jamii Ni nini kilichokuoata mkewangu??
    Naomba uelewe kuwa binafsi siogopi kwenda jela kwasababu ya hiyo muvi mliyonizushia, kwani ni bora nikakae jela kuliko kuishi huru huku mkininyanyasa kiasi cha kuondoa utu wangu kama bidamu, lakini kinachoniuma ni familia yetu!! Kwanini watoto wateseke kwa sababu ya tamaa zetu binafsi!! Nikifikiria hilo naumia sana!
    Najua kwa sasa inaonekana kama vile ni impossible kwa mimi na wewe kurudiana tena, lakini binafsi naamini tunaweza!! Najua haitakuwa rahisi kwani tumeharibu mno, lakini ni heri ya kujaribu kuliko kuendelea kufanya huu upuuzi tunoufanya sasa!!
    Kumbuka hiki tunachokifanya sasa hatujajipaka matope sisi tu pekee, bali mziki wote wa injili Tanzania, na tusipotubu tukajirudi Mungu atatuhukumu kwa dhambi hii!!
    Kumbuka kuwa hakuna kati yenu atakayeshinda katika hii vita, vyombo vya habari pekee ndivyo vitakavyo nufaika lakini mimi, wewe na mchungaji wote tuta loose!!
    Mwisho nimalizie na wewe mchungaji, tulipokutana mara ya kwanza nilikuchukulia kama kaka na kama mlezi wetu wa kiroho!! Lakini umegeuka shetani mwenye pembe saba, umeparaganyisha familia yangu, umeleta maumivu makali kwenye ukoo!!
    Nakuonya tena kwa mara nyingine, muache mkewangu!! Huyo ni mkewangu, nilimtolea mahali mimi mwenyewe na wazazi wake waliniamini na kunikabidhi!!! Nasema niachie mkewangu!!
    Wewe ni nyoka, imefika time watanzania wakujue ukweli wako wewe mbwa mwitu mkali uliyevaa ngozi ya kondoo!!!
    Umedanganya watu vya kutosha na umefarakanisha ndoa nyingi sana kwa sababu ya kiburi cha pesa zako chafu za sembe!! Umeudhalilisha ulokole kiasi cha kutosha imefika time tuwaeleze watanzania ukweli na wakufahamu kuwa wewe ni nyoka!!
    Sitakubali kuona ukiendelea kuitesa familia yangu, nitapambana na nitakushinda!!! Siogopi fedha zako wala connection ulizonazo, ni bora nife nikiwa nimesimama kuliko kuishi nimepiga magoti!
    Nitapambana na wewe mpaka mwisho ili historia isomeke vizuri ili hata wanangu wakiwa wakubwa wajue kuwa baba yao sikuwa lofa kiasi cha kupiga magoti na kuelekeza shingo kibla kuruhusu mdhalimu kama wewe uichinje familia yangu, bali licha ya umasikini wangu nilisimama kiume na kupigana kutetea familia yangu!!!
    Narudia tena mchungaji, nitapambana na nitakushinda..
  • June 22, 2014

  • Yale yaleeeeee: Eh, wazee wa chuma chakavu mtatuulia magari jamani....



    Yale yaleeeeee: Eh, wazee wa chuma chakavu mtatuulia magari jamani....
     "Ohoooooo.... Gari langu maskini...." Dereva wa teksi anatoka nje kuangalia jinsi gari lake lilivyoingia kwenye chemba ya maji machafu ambayo mfuniko wame umeeshaenda kusikojulikana na kuacha shimo kubwa katikati ya barabara ya Mtaa wa Zanaki jijini Dar es salaam leo
     Wasamaria wema wanasogea kuja kumuokoa
     "Hayaaaa....twendeeeeee" Gari linatoka
     Anapiga rivasi taratibu huku mshimo ukiwa umeachama  
    Anaondoka taratibu huku akisikitika na kujiuliza nini kifanyike kuondoa adha hii jijini....


  • June 20, 2014

  • Wajeruhiwa kwa Risasi za Moto Baada ya Kunaswa Wakicheza Ngoma za Vigodoro Wakiwa Utupu



    Wajeruhiwa kwa Risasi za Moto Baada ya Kunaswa Wakicheza Ngoma za Vigodoro Wakiwa Utupu
    Watu watatu wakazi wa Mwananyamala Jijini Dar Es Salaam wamejeruhiwa katika tukio lililohusisha risasi za moto linalodaiwa kufanywa na polisi baada ya kukutwa wakikesha kwenye ngoma maarufu za Kigodoro, ambazo tayari zimekwishapigwa marufuku na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam.
    Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi na nusu jioni katika eneo la shule ya msingi kisiwani ambapo mmoja  wa  majeruhi hao  tayari amekwisahruhusiwa kurudi nyumbani na mwingine akiendelea na matibabu kwenye hospitali ya Mwananyamala.

    Wakiwa kwenye ngoma hiyo maarufu Jijini Dar es Salaam ya Kigodoro, eneo la Kisiwani mwananyamala, mara gahfala polisi walivamia eneo hilo, na kusimamisha shughuli nzima kwa madai ya kucheza wakiwa hawana nguo, jambo ambalo ni kinyume na maadili.

    Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni Kamishna msaidizi Camillius Wambura anathibitisha kutokea kwa tukio hilo.

  • Sakata la Mumewe kusota Rumande Kwa Ubakaji….Flora Mbasha Ajikuta Akiambulia AIBU ya Mwaka.



    Sakata la Mumewe kusota Rumande Kwa Ubakaji….Flora Mbasha Ajikuta Akiambulia AIBU ya Mwaka.
    Wakati jana mumewe Emmanuel Mbasha (32) akipandishwa kizimbani kwa mara ya pili kwa soo la ubakaji wa shemejiye, mwimba Injili kinara Bongo, Flora Mbasha (31) amepitia katika hatua tatu za aibu.
     
    Mbasha ambaye naye ni mwimba Injili na mfanyabiashara alitarajiwa kupandishwa kizimbani jana kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Ilala, Dar akitokea mahabusu Keko akikabiliwa na mashtaka mawili ya ubakaji wa shemejiye mwenye umri wa miaka 17.

    Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa Flora ambaye alihama nyumbani na kwenda kuishi hotelini maeneo ya Sinza, Dar, kitendo hicho kilimuingiza staa huyo kwenye hatua ya tatu ya aibu na kujikuta akiwa katika masikitiko makubwa.

    AIBU YA KWANZA
    Kwa mujibu wa mtu huyo wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina, aibu ya kwanza inayomuuma Flora ni ile ya ndoa yake kuingia kwenye gogoro kisha kudaiwa kutengana na mumewe kinyume na kile anachokihubiri kupitia nyimbo zake zinazopendwa na wengi ndani na nje ya Bongo.
     
    "Unajua lile neno la 'mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe' (Mithali 14:1) linamfanya awe na aibu mbele za watu.

    "Unaambiwa kanisani (anasali Kanisa la Ufufuo na Uzima la Mchungaji Josephat Gwajima kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Dar) anaona aibu hasa kwa waumini wenzake.

    "Flora amedumu na Ima (Mbasha) kwenye ndoa kwa miaka 12 hivyo kutokea kwa kilichotokea ni aibu kwani tayari walikuwa wamekomaa tofauti na walipoona wakiwa na umri mdogo.

    "Hebu fikiria, mtoto amekuwa mkubwa, anaposikia mama ana matatizo na baba si ni aibu jamani? Cha msingi tuwaombee wamalize matatizo yao, inaweza kusaidia kuifuta aibu hiyo kwani imeandikwa 'Ndoa na iheshimiwe na watu wote…' ( Waebrania 13 : 4 -)," alisema mnyetishaji wetu akisisitiza kuwa akitajwa  ataonekana mvujishaji wa mambo ya siri ya wanandoa hao.
    AIBU YA PILI

    Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa aibu ya pili inayomkabili Flora ni skendo ya yeye kudaiwa kuhamishia makazi kwa mchungaji wake, Gwajima.
     
    Katika aibu hiyo, mumewe alinukuliwa na gazeti la Uwazi akimlalamikia mchungaji huyo amwachie mkewe kwani yeye ndiye alisababisha sakarakasi zote hizo za ndoa yake.

    Ilidaiwa kuwa kwa mke wa mtu achilia mbali mhubiri kwa njia ya nyimbo, kitendo cha kukumbwa na skendo nayo ni aibu pia.
     
    "Kwa mtumishi kutajwa kwenye jambo kama hilo lisilo na mrengo wa kupendeza masikioni mwa watu, ni aibu kuu," kilidai chanzo hicho.

    AIBU KUU YA TATU

    Ilisemekana kuwa achilia mbali ndoa, mambo ya mchepuko lakini aibu kuu ya tatu kwa Flora, ni kashfa ya ubakaji wa shemejiye inayomkabili mumewe Mbasha.

    "Unajua usifikirie kwamba mume akipata aibu mke anaweza kuikwepa. Hawezi kwa sababu 'wanazungumza lugha moja' (yaani ni mwili mmoja). Ona sasa mume anapandishwa kizimbani kwa ubakaji.
     
    "Pia usifikiri watu watasema kashfa ni ya Ima peke yake. Kwanza hata kutamka watu wanasema mume wa Flora. Ikumbukwe aibu ya mume ni ya mke pia. Ni vigumu mno kwa Flora kusema aibu ni ya mumewe pekee," alitiririka mto habari huyo.
    FAMILIA ZATOFAUTIANA

    Wakati hayo yakiendelea, habari zinadai kuwa familia za pande zote zinatofautiana huku kila moja ikilaumu nyingine.
    Ilidaiwa kuwa upande wa Mbasha unamlalamikia mama wa Flora kuwa anamuunga mkono mwanaye badala ya kusaidia kutuliza hali ya hewa.
    Ilielezwa kuwa upande wa Flora wao wanamlaumu Mbasha kwa madai kuwa chanzo cha yote ni mgawanyo wa mali hasa baada ya kuona kuwa hakuna tena ndoa.

    FLORA ANASEMAJE?

    Akizungumza na Ijumaa juzi kwa njia ya simu, Flora alitoa la moyoni: "Kweli naumia sana tena sana. Kwa sasa kesi ipo mahakamani, siwezi kuizungumzia lakini ndiyo hivyo. Siyo siri nateseka sana."

    Mbasha anadaiwa kumbaka ndugu wa Flora ambaye ni yatima kati ya  Mei 23 na 25, mwaka huu ambapo kesi yake inaendelea kuunguruma baada ya kukaa mahabusu ya Keko kwa siku kadhaa ambapo sheria ndiyo itakayoanika siri zote juu ya sakata hilo.

    Crediti: GPL


  • Sitakaa Nimwamini Mwanamke Maisha Mwangu




    Sitakaa Nimwamini Mwanamke Maisha Mwangu
    Nimeamini ule msemo wa mwanamke sio ndugu yako na sitakaa katika maisha yangu nimwamini mwanamke, sijaamini kama Florah angemwacha Mbasha aingie jela ama kweli hujafa hujaumbika hivi kweli mwanaume hata kama mmekosana unaweza kukubali apelekwe jela, wanawake sio hawana ubinadamu...Naamini kabisa Flora alikuwa na uwezo mkubwa wa kuingilia hilo na kuyamaliza kinyumbani...Nahakika asilimia 100 Mbasha akifungwa Jela baada ya miaka kadhaa atajutia alichofanya cha kukaa na kuangalia mume wake akienda Jela Bila Msaada wowote....Flora angeibuka Shujaa Kama Angeibuka na Kufuta kesi na kuyamaliza kifamilia 
    Je wewe Kwa hilo Unasemaje?


  • Tundu Lissu Ailipua Tena Serikali Kwa Kutoa Taarifa za Uongo



    Tundu Lissu Ailipua Tena Serikali Kwa Kutoa Taarifa za Ungo
    Serikali imeumbuliwa bungeni ikidaiwa kuwasilisha taarifa za uongo kupitia Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu ugawaji wa madawati yaliyonunuliwa kwa 'chenji ya rada'.

    Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu alitoa tuhuma hizo jana, wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014, akisema Serikali imewadanganya wabunge kwa kuwa hakuna kitu kilichofanyika.

    Alisema katika majibu ya Serikali kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kwa kuwa imetangaza kununua madawati 93,740 na kuyagawa katika halmashauri mbalimbali nchini wakati siyo kweli.

    Alisema kwa mtindo huo, Serikali imelidanganya Bunge pamoja na Watanzania kwa kuwa imetangaza madawati hewa ambayo hayapo.

    "Wabunge kama kweli mnatimiza majukumu yenu na hampo hapa kwa masilahi yenu tu, hebu hojini halmashauri zetu zimepelekewa haya madawati 93,000 yanayozungumzwa humu au mnapiga makofi tu? Serikali inadanganya tunatakiwa tuihoji tuiwajibishe," alisema.

    Lissu ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alitoa mfano wa mgawo huo kwenye Halmashauri ya Ikungi, Singida kwamba ilitangazwa kupelekewa madawati 508 lakini amekwenda jimboni na hakukuta dawati hata moja.

    Alisema uchunguzi wake umebaini kuwa hata katika wilaya mbalimbali ikiwamo ya Iringa, hakuna kitu kama hicho.

    "Jana sikuwa hapa bungeni nilikwenda kwenye halmashauri yangu, hakuna dawati hata moja. Hata Halmashauri ya Iringa kwa Mchungaji Msigwa (Peter) hapa ananiambia hakuna dawati hata moja, mnatudanganya ili iweje?" Aliwashauri wabunge wengine kufanya utafiti katika maeneo yao iwapo kuna madawati ambayo yamepelekwa kutokana na fedha zilizorejeshwa na Serikali kama chenji ya rada.

    Lissu alisema ni maneno matupu ambayo yamekuwa yakiwahadaa wabunge na kuwafanya wasahau wajibu wao wa kuisimamia Serikali na kujikuta ni washangiliaji wakati wote. Lissu alisema kinyume na taarifa hizo za Waziri Mkuu, Bunge jana lilikuwa limeelezwa na Naibu Waziri (hakumtaja) kuwa madawati hayo hayajagawanywa.

    Katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa akijibu swali la nyongeza la Ibrahim Sanya (Mji Mkongwe - CUF), kuhusu madawati hayo, alisema kwa kuwa madawati hayo bado yanagawanywa, watakaa na kuangalia utaratibu mzuri wa kuyafikisha Zanzibar.

    Lissu pia alisema fedha ambazo zilitajwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospter Muhongo kuwa ni pato la Watanzania ni uongo kwa kuwa ni mali ya wamiliki wa migodi.

    Alisema takwimu za waziri zimesababisha Watanzania kuamini kuwa wameingiza fedha nyingi ilihali kiasi kilichoingia hakifikii hata asilimia 10 ya pato la wawekezaji.


  • June 16, 2014

  • Rais Kikwete aagiza waliolipua Bomu Zanzibar wasakwe na kukamatwa haraka



    Rais Kikwete aagiza waliolipua Bomu Zanzibar wasakwe na kukamatwa haraka

    RAIS Jakaya Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki watu wote waliohusika katika ulipuaji bomu lililosababisha kifo na kujeruhi watu saba mjini Unguja, Zanzibar.
     
    Rais  Kikwete ambaye amesema kitendo hicho ni cha kulaaniwa kwa nguvu zote na watu wote wapenda amani Bara na Visiwani, amekitaja kuwa ni cha woga kisicho na ustaarabu, kisichokubalika katika dunia ya sasa.
     
    Alisema hayo katika salamu za rambirambi alizotuma jana kwa Rais Ali Mohamed Shein wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
     
    Bomu hilo lilirushwa katika shughuli ya kidini iliyokuwa ikifanyika katika eneo la Darajani , mjini Unguja. Miongoni mwa majeruhi, yumo mhubiri wa amani ajulikanaye kama Sheikh Ahmed Haidari Jabir wa Zanzibar.
     
    "Hicho ni kitendo cha kulaaniwa kwa nguvu zote na watu wote wapenda amani Bara na Visiwani, ni kitendo cha woga na kisicho na ustaarabu na wala hakikubaliki katika dunia ya sasa," alisema Rais Kikwete  na  kuongeza:
     
    "Hiki ni kitendo kilichofanywa na watu waoga, wasio na ustaarabu wa aina yeyote ile."
     
    Alikemea wanaofanya vitendo hivyo na akahimiza watu kuwa wastaarabu, wavumilivu na kuheshimu imani na mitizamo ya watu wengine hata kama hawakubaliani nao.
     
    Akiendelea kulaani, alisema amesikitishwa zaidi na watu hao wasio na ustaarabu ambao wamefanya kitendo hicho cha kihalifu kwenye shughuli ya kidini ambapo ndipo mahali panapostahili amani, uvumilivu na unyenyekevu zaidi kwa kuwa ni wakati ambapo binadamu anapofanya mawasiliano na muumba wake.
     
    Alihimiza polisi kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki wahusika wa tukio hilo. Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai wa Zanzibar, Yussfu Ilembo, aliyekufa papo hapo ni Muhammad Mkombalaguha (26), mkazi wa Tanga.
     
    Kutokana na tukio hilo, polisi visiwani humo ilitangazia hali ya hatari kwa  watu waliohusika na shambulio hilo. Ilielezwa kwamba uchunguzi umeanzia kwenye mabaki ya vitu vilivyokutwa katika eneo la tukio.
     
    Miongoni mwa vielelezo vilivyokusanywa ni pamoja na vipande vya mabaki ya gundi ya karatasi na vitu vingine ambavyo vinasadikikwa vimetumika kutengeneza bomu hilo.
     
    Mtu aliyekufa pamoja na majeruhi, walikutwa na mkasa huo wakati wakitoa Msikiti wa Darajani baada ya Ibada ya Swala ya Isha inayoswaliwa kuanzia saa 1:45 usiku na kuendelea.
     
    Baada ya kumalizika ibada hiyo, walitoka msikitini na kufika eneo la Darajani wakisubiri gari na ndipo mlipuko mkubwa uliposikika ambao unasadikiwa kuwa ni bomu.
     
    Katika hatua nyingine, akiwa mkoani Dodoma juzi, Rais Kikwete aliwataka Watanzania kuendelea kulinda na kupigania amani iliyopo kwa ustawi na usalama wa nchi .
     
    Rais Kikwete alisema hayo juzi kwenye uzinduzi wa tamasha la uzalendo lililoasisiwa na wasanii wa muziki na filamu nchini ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa video ya wimbo maalumu wa Muungano wa Tanzania na Zanzibar.
     
    Alisema uzalendo kwa Watanzania ndiyo njia pekee ya kufanya taifa liendelee kutunukiwa hadhi ya kisiwa cha amani duniani.
     
    Katika tamasha hilo lililofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Rais Kikwete alisema ili kuwaenzi waasisi wa taifa, ni lazima kudumisha misingi ya amani na kujitolea kizalendo kulilinda na kulitetea taifa kama walivyofanya waasisi Mwalimu Julius Nyerere na Shehe Abeid Amani Karume.
     
    Pia aliwataka wasanii kutumia vizuri talanta walizojaliwa kufikisha ujumbe wenye uzalendo kwa Tanzania.

    Credit: Habari Leo



  • Jackline Wolper: Msaka Pesa toka Machame aliyeishia kwa Matapeli wa Mapenzi jijini Dar



    Jackline Wolper: Msaka Pesa toka Machame aliyeishia kwa Matapeli wa Mapenzi jijini Dar

    Jackline  Wolper  ni  mmoja  kati  ya  warembo  wenye  umaarufu  mkubwa  nchini  na  katika   soko  la  Filamu  za  Tanzania.

    Anamvuto  unaokubalika  na  wengi  na  ameweza  kujipatia  umaarufu  mkubwa  sana  kupitia  filamu  alizoshirikishwa  na  alizozifanya  chini  ya  kampuni  yake  mwenyewe. Pia  ni  mwandishi  mzuri  wa  Script  na  muongozaji  mzuri  wa  filamu....

    Alizaliwa  Moshi  mkoani  Kilimanjaro  na  kupata  elimu  yake  ya  msingi  katika  shule  ya  msingi  Mawenzi  huko huko  Moshi.Baadae  alipata  elimu  ya  sekondari  katika  shule  ya  sekondari  Magreth  Ekenywa  iliyopo  jijini  Arusha  na  inasemekana  aliendelea  na  masomo  nchini  Kenya.....

    Rekodi  zinaonyesha  kuwa  alitua  jijini  Dar  kati  ya  mwaka  2005  na  2007  akiwa  na  jukumu  moja  tu  la  kusaka  pesa.Kama  ilivyo  ada  kwa  jamii  ya  watu  wa  kabila  lake  baada  ya  kufika  jijini  Dar  hakulaza  damu, fasta  alicheki  michongo  ilipo  na  kuanza  kuifanyia  kazi..

    Kujulikana  kwake  kulianzia  pale  alipoanza  kupita  mitaani  akitembeza  bidhaa  za  mikononi  na  kuziuza  kwa  bei  ya  promosheni. Hakuna  aliyejua  machina  Wolper  angekuja  kuwa  bonge  la  staa  nchini  Tanzania...

    Ni  kipindi  hiki  ambacho  wanaume  walimchukulia  poa  na  kumpita  bila  hata  salamu kama  vile  wafanyavyo  kwa  kina  dada  wanaotembeza  bidhaa  za  mikononi.Ni  wanaume  wachache  sana  ndo  waliweza  kugundua  uzuri  wa  Wolper  na  kumtupia  maneno  mawili  matatu  yenye  ushawishi  wa  ngono....

    Baadae  aliingia  kwenye  biashara  za  Saluni  maeneo  ya  Tandale  jijini  Dar  kabla  ya  kujiingiza  kwenye  sanaa  ya  uigizaji....

    Kipindi  flani  Wolper  akiishi  maeneo  ya  Mwenge  alikutana  na  mtu  mmoja  wa  kabila  lake  aliyefahamika  kwa  jina  la  Injia  Macha  ambapo  jamaa  huyo  alianzisha  utani  wa  kumuita  mjomba  lakini  baadaye  ujomba  ukapitiliza  na  akaanza  kuomba  kulila  tunda....

    Inasemekana  kwamba  jamaa  alifanikiwa  kulila  tunda  kwa  kipindi  kirefu  na  aliponogewa  alimuhamisha  Wolper  toka  Mwenge  alikokuwa  akiishi  na  dada  yake  na  kumpangishia  chumba  cha  kwanza  maeneo  ya  Sinza  Mori....

    Injinia  huyo  alimpatia  Wolper  gari  chakavu  aina  ya  Toyota  Celica  ambapo  baada  ya  siku  kadhaa  Wolper  aliipiga  bei  gari  hiyo.....

    Akiwa  mitaa  ya  Sinza ndipo  akakutana  na  mwanadada  Lucy  Komba  ambaye  ni  msanii  wa  filamu  aliyemshawishi  kujiingiza  katika  tasnia  hiyo....Kipindi  hicho  ilikuwa  ni  mwaka  2009.

    Baada  ya  kupata  mtonyo  wa  Movie, Wolper  aliuchangamkia  na  kwa mara  ya  kwanza  akaonekana  katika  filamu  ya  'Ama  Zangu  Ama  Zao'  iliyofanywa  na  mwanadada  Lucy  Komba...

    Baada  ya  hapo  alianza  kupata  mialiko  toka  kwa  watu  mbalimbali  ili  aweze  kuigiza  kwenye  filamu  zao.Alifanikiwa  kukutana  na  Director  mkongwe,William  Mtitu  na  marehemu  Steven  Kanumba  na  kufanya  filamu  mbalimbali  zilizomjengea  jina  katika  tasnia  hiyo....

    Baada  ya  kuanza  kupata  mafanikio, Wolper  alizinguana  na  Injia  Macha  ambaye  alikuwa  amempatia  gari  nyingine  aina  ya  Toyota  GX  100....

    Mgogoro  mkubwa  uliibuka  kiasi  cha  Injia  Macha  kuwatumia  polisi  kumnyanga'anya  gari  hilo  Wolper.Polisi  walimkuta  akiwa  na  gari  hilo  maeneo  ya  Ilala  ambapo  alielezwa  kuwa  gari  hilo  linatafutwa  na  mwenyewe  na  lina  kesi  katika  kituo  cha  polisi  Oysterbay.

    Wolper  akiwa  hajui  kama  mchongo  huo  ume injiniwa  na  Injia  Macha  alitaka  kuwavimbishia  kifua  maafande  akidai  kuwa  gari  hilo  alinunuliwa  na  mjomba  wake na  kadi  anazo.Lakini  alijikuta  akigonga  mwamba  kuondoka  na  gari  hilo  pale  polisi  walipomtaka  waende  kituoni  kulihifadhi  gari  hilo  kisha  akamlete  huyo  mjomba  wake  pamoja  na  kadi  za  manunuzi  ya  gari  hilo...

    Wapekenyuzi  wanaeleza  kuwa  kipindi  hicho  tayari  Wolper  alikuwa  na  bwana  mwingine  na  Injia  Macha  alishaushtukia  mchongo  na  ndio  sababu  alimfanyia  umafia  bila  Wolper  kujua....

    Wolper  akaingia  mkenge, akamshtua  bwana'ke  mpya  kuhusu  polisi  wanachotaka  kukifanya.Bwana'ke  akamwambia  asijali, wakutane  Oysterbay  Polisi  ili  akalichukue  hilo  gari  mbele  ya  maafande....

    Kilichotokea  ni  kwamba  baada  ya  Wolper  kufikia  kituo  cha  Polisi  alivutwa  sikio  na  afande  mmoja  kwamba  Injinia  Macha  yupo  kituoni  hapo  na  anawasubiri  kwa  hamu  yeye  na  bwanake  waje  na  documents  za  umiliki  wa  gari  hilo  hali  iliyomfanya  Wolper  aingie  mtini....

    Inasemekana  kuwa  kama  bwana  mpya  wa  Wolper  angetokea  kituoni  hapo  angetiwa  ndani  yeye  na  Wolper  kwa  kesi  ya  wizi  wa  gari  lakini  machale  yakawacheza  wakalala mbele.....

    Baadaye  Wolper  alisikika  kupitia  Radio  Clouds  FM akitangaza  kuwa  amedhulumiwa  gari  na  mjomba  wake  ambaye  alimuongezea  pesa  kidogo  katika  manunuzi  ya  gari  hilo  lakini  baadaye  akawa  anamtaka  kimapenzi  na  kumzushia  kwamba  amemuibia  gari. Huu  ndo  ukawa  mwisho  wa  Wolper  na  Injia  Macha.

    Baada  ya  kutemana  na  Injia  Macha, Wolper  alipitia  kwenye  mikono  mingi  ya  kimahusiano  lakini  uhusiano  mwingine  uliompandisha  chati  ni  ule  wa  Abdallah  Mtoro  almaarufu   Dallas....

    Dallas  akiwa  hana  jina  la  kutosha  ndani  ya  jiji  la  Dar  es Slaam, ghafla  alikuwa  maarufu  baada  ya  kutangaza  ndoa  na  Wolper  na  hasa  pale  alipompatia  kiasi  cha  Dolla  elfu  10 ( Tsh 16 Milioni)  akampatie  marehemu  Sajuki  kwa  ajili  ya  matibabu. Kitendo  hicho  kilimfanya  Wolper  awafunike  mastaa  wote  wa  kike  akiwemo  Wema  Sepetu......
    Hata  hivyo  mahusiano  ya  Dallas  kwa  Wolper  yalijaa  utapeli  mwingi  kwani  wakiwa  bado  hawajafahamiana  na  Dallas  ambaye  inasemekana  ni  mfanyabiashara  wa  'Sembe'  alimuingia  kimafia  Wolper  na  kufanikiwa  kumteka  kimapenzi  hadi  akafunga  naye  ndoa.....

    Umafia  alioufanya  Dallas  ni  pamoja  na  kumpenyezea  vitu  vya  thamani  kama  vile  magari  ya  kifahari  na  pesa  za  matumizi.

    Kwa  kuwa  Wolper  tangu  anatoka  Machame  alijua  anakuja  mjini  kutafuta  pesa, hakupoteza  muda  kutaka  kujua  mambo  mengi  kuhusu  Dallas. Alichoaangalia  ni  Dallas  amekuja  na mkono  gani?  Mkono  mtupu, mkono  wa  birika  au  mkono  wa  madini?

     Alipogundua  kwamba  jamaa  alikuwa  na  madini  ya  kutosha  akajitoa  mzima  mzima  na  kumkabidhi  Dallas  moyo  wake  wote , mwisho  wa  siku  akajikuta  akiumbuka  na  kuambulia  maumivu  baada  ya  kumtambua  Dalls  ni  mtu  wa  namna  gani.


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.