November 11, 2015

  • WANAOSUMBULIWA NA MARADHI YA FISTULA WATAKIWA KUJITOKEZA WATIBIWE BURE



    WANAOSUMBULIWA NA MARADHI YA FISTULA WATAKIWA KUJITOKEZA WATIBIWE BURE
    Kaimu Ofisa mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kulia)akiongea na baadhi ya wakina mama wanaotibiwa maradhi ya Fistula katika hospitali ya CCBRT wakati bodi ya Vodacom Foundation ilipowatembelea hospitalini hapo ili kujua maendeleo yao ya kiafya. Mfuko huo unawawezesha akina mama kusafirishwa kutoka mikoani kwa kutumiwa pesa za kuja kutibiwa hospitalini hapo kupitia huduma ya M-PESA.
    Bi.Muhoja Masano anayebatiwa matibabu ya maradhi ya Fistula katika hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam(kushoto)akimwelezea jambo Kaimu Ofisa mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kulia)wakati Bodi ya Vodacom Foundation ilipowatembelea akina mama wanaotibiwa maradhi hayo katika hospitali hiyo kutaka kujua maendeleo yao ya kiafya.Vodacom Foundation inawawezesha wakina mama kusafirishwa kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa kutumiwa pesa za kuja kutibiwa hospitalini hapo kupitia huduma ya M-PESA.
    Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Vodacom Foundation wakimsikiliza Ofisa mtendaji mkuu wa hospitali ya CCBRT ya jijini Dar es Salaam Erwin Telensman(wapili toka kulia) wakati Bodi ya Vodacom Foundation ilipowatembelea akina mama wanaotibiwa maradhi hayo katika hospitali hiyo kutaka kujua maendeleo yao ya kiafya.Vodacom Foundation inawawezesha wakina mama kusafirishwa kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa kutumiwa pesa za kuja kutibiwa hospitalini hapo kupitia huduma ya M-PESA.
    Mtoa huduma kwa wakina mama wanaosumbuliwa na maradhi ya Fistula katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salam,Theodara Millinga(kulia)akiwafafanulia jambo baadhi ya wajumbe wa bodi ya Vodacom Foundation waliotembelea hospitalini hapo kwa ajili ya kujua hali za kiafya kwa akina mama wanaotibiwa maradhi hayo katika hospitali hiyo. Vodacom Foundation inawawezesha wakina mama kusafirishwa kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa kutumiwa pesa za kuja kutibiwa hospitalini hapo kupitia huduma ya M-PESA.
    Akina mama wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Fistula wametakiwa kujitokeza ili waweze kusaidiwa kupata matibabu ya bure katika hospitali ya CCRBT iliyopo jijini Dar es Salaam na vituo ambavyo imefungua kwenye mikoa mbalimbali kwa kuwa ugonjwa huu unaotokana na matatizo ya uzazi unatibika.
    Wito huu umetolewa na Kaimu Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia wakati ujumbe wa bodi ya Vodacom Foundation ulipotembelea hospitalini ya CCRBT wakiwa kama wadau wanaoshirikiana na hospitali hiyo katika mapambano ya kutokomeza maradhi ya Fistula.
    Amesema Vodacom Foundation ambayo imekuwa mstari wa mbele kufadhili kugharamia akina mama wahanga wa Fistula kuwawezesha kusafiri kutoka kwenye makazi yao itaendelea kufanikisha matibabu ya akina mama hao hadi hapo ugonjwa huu utakapotokomezwa kabisa.
    "Vodacom kupitia huduma yetu ya M-Pesa tumekuwa tukiwawezesha akina mama kusafiri kutoka makwao hadi jijini Dar es Salaam baada ya kupata taarifa za maradhi ya fistula kupitia mabalozi wa Fistula waliopo mikoa mbalimbali na tumekuwa tukifadhili wahanga waliotibiwa na kupona kupatiwa ujuzi kupitia kituo cha Mabinti kabla ya kurejea makwao ili wafikapo huko waweze kujitegemea. Tunatoa wito kwa akina mama walioathirika kujitokeza kutibiwa kwa kuwa unatibika na natoa wito mtokapo hospitalini na kurejea kwetu muwe mabalozi wa kuhamasisha akina mama waathirika ambao hawajajitokeza kupata matibabu ".Alisema.
    Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa CCRBT,Erwin Telemans aliuelezea wajumbe hao wa bodi wa Vodacom Foundation kuwa hospitali hiyo ikiwa inaadhimisha miaka 20 tangu kuanzisha kwake hapa nchini inajivunia kujijengea heshima kubwa ya kutoa huduma bora za afya na kuweza kufanikisha matibabu kwa watanzania wengi.
    Telemans alisema mafanikio haya yasingepatikana bila kupata ushirikiano wa serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaoifadhili ikiwemo kampuni ya Vodafone na Vodacom Foundation ambazo ni moja ya wabia wake wakubwa katika kufanikisha matibabu kwa wagonjwa hususani yanayohusiana na uzazi wa akina mama.
    Alisema hivi sasa hospitali hiyo imejikita zaidi katika kutokomeza Fistula kwa kuboresha huduma za akina mama wajawazito ambapo kwa mwaka huu zaidi ya wanawake 100,000 wamepatiwa huduma za afya ya uzazi hospitalini hapo na ana imani matatizo yanayotokana na uzazi kwa akina mama nchini yatapungua baada ya kukamilika kwa ujenzi wa wodi ya akina mama hospitalini hapo ambayo inatarajiwa kutoa huduma bora kwa akina za uzazi na kupunguza matatizo ya uzazi na vifo vya akina mama na watoto wachanga.
    "Mbali na matatizo ya uzazi tumebobea katika huduma za magonjwa ya macho,upasuaji na matibabu ya ulemavu wa midomo,unyoshaji viungo vyenye ulemavu na kutoa viungo bandia kwa waathirika na huduma hizi zote tunazifanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na nachukua nafasi hii kuwashukuru na kuwaomba kuzidi kutuunga mkono ili tuendeleze jitohada za kutokomeza maradhi hususani kwa wananchi wenye vipato vya chini ambao iadi yao kubwa hawana wezo wa kumudu gharama za matibabu".Alisema.

    Naye mmoja wa wagonjwa anayetibiwa ugonjwa wa Fistula hospitalini hapo Leah Jonas ameishukuru hospitali hiyo kwa jinsi inavyowahudumia wahanga wa ugonjwa huo pia kwa niaba ya wenzake aliishukuru taasisi ya Vodacom Foundation kwa kufanikisha matibabu yao.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.