Polisi katika nchi sita za Ulaya wamewakamata watu 17, kwa tuhuma za kupanga mashambulizi.
Watu hao wengi wao wakiwa Wakurd wa Iraq, wanachama wa kundi la Wapiganaji wa Kiislamu, wanadaiwa kwa kupanga mashambulizi nchini Norway na Mashariki ya Kati.
Katika kamata hiyo polisi walililenga kundi la Rawti Shax, ambalo wamesema ni kundi la waislamu wa dhehebu la sunni, ambalo limejikita kuiondoa serikali ya Iraq katika jimbo la Kurdistan, na kuweka utawala wa sharia.
Polisi wamesema kundi hilo lilikuwa likijiandaa kufanya mashambulizi ili kumuokoa kiongozi wake, Muhubiri mwenye msimamo mkali ,Mullah Krekar anayeshikiliwa nchini Norway.
0 comments:
Post a Comment