Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

Showing posts with label Majanga. Show all posts
Showing posts with label Majanga. Show all posts

July 16, 2014

  • MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MOMBA.


    MTU MMOJA AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MOMBA.
    MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BAKARI DAMSON(27) MKAZI WA MAJENGO AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI ADC 3671 AINA YA TOYOTA LAND CRUISER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA FRANK MATHEW SIKONGA (29) MKAZI WA CHIPAKA.

    TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15.07.2014MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO KATIKA MTAA WA MWAKA, KATA NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA AMEKAMATWA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

    KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKIANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

    Imetolewa na:
    [BARAKAEL N. MASAKI – ACP]

    KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


  • July 15, 2014

  • AJALI YA PIKIPIKI NA MAGARI YAUA WATU WATATU


    AJALI YA PIKIPIKI NA MAGARI YAUA WATU WATATU


    Gari aina ya Range Rover lenye likiwa limeharibika vibaya baada a kugongana uso kwa uso na gari dogo

    Gari dogo aina ya Toyota Corolla lilikiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na Range Rover katika makutano ya barabara ya Arusha/Moshi jirani kabisa na kipita shoto(Keep left) cha Arusha
    Mifuko maalumu ya kuzuia abiria asiumie wakati wa ajali ikiwa imefumuka baada ya ajali .

    Pikipiki ikiwa chini ya gari aina ya Range Rover baada ya kugongwa.
    Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakitizama pikipiki iliyokuwa chini ya gari hiyo
    Hivi ndivyo pikipiki inavyoonekana ikiwa chini gari.
    Askari polisi wa kikosi cha usalama barabarani wakichukua vipimo mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo ambayo watu wawili wanadaiwa kufariki dunia papo hapo huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya akiwemo dereva bodaboda aliyevunjika miguu.


    Baadhi ya wanannchi wakitizama ajali iliyotokea katika makutano ya barabara kuu ya Moshi/Arusha na ile ya kuelekea ofisi za mkuuu wa wilaya ya Moshi


  • July 12, 2014

  • ZANZIBAR UCHOCHORO MPYA WA MADAWA YA KULEVYA



    ZANZIBAR UCHOCHORO MPYA WA MADAWA YA KULEVYA
    Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata Ali Suleiman Rashid (34) akiwa na mikoba 14 ya wanawake aliyohifadhia dawa za kulevya zenye uzito wa kilo tano akitokea Oman katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume visiwani humo.
    Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Mkuu ya Polisi Ziwani mjini Zanzibar, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI ), Yussuf Ilembo alisema kuwa mtuhumiwa huyo raia wa Tanzania  amekamatwa muda mfupi baada ya kushuka kutoka Ndege ya Oman yenye namba za usajili .WY.717 iliyokuwa ikitokea Muscat. alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Julai 9,  saa 8 mchana akiwa amehifadhi mikoba hiyo katika sanduku kubwa lenye rangi nyeusi na maofisa wa upelelezi waligundua ndani yake kuwemo mikoba 14 iliyokuwa na dawa hizo ikiwa imeshonewa kwa vitu maalumu.
     Dawa hizo  za kulevya zina uzito wa kilo 5.605, zilihifadhiwa
    kwenye mikoba 14 inayotumiwa na wanawake. Upelelezi kukamilika, atafikishwa mahakamani mara moja.
    alisema DCI Ilembo.
    Alisema polisi inaendelea na uchunguzi wake ili kusaka mtandao wa watu wanaojishughulisha na vitendo hivyo kwa kuchunguza njia mbalimbali za mawasiliano za mtuhumiwa huyo aliyekamatwa.
    Kwa mujibu wa polisi,  mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia hati ya kusafiria namba AB 363906 iliotolewa Desemba 29 mwaka 2009 Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Dar es Salaam na tayari  ameshasafiri katika nchi za Brazil, China, Japan, Hong Kong, Afrika Kusini na Falme za Kiarabu.
    Ilembo aliwataka wananchi kuchukua hatua kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuwafichua kwa siri, wanaoingiza dawa za kulevya na wauzaji ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
     Wakati wa kulindana, kuleana na kuoneana aibu umekwisha, kila mmoja ajione ana wajibu wa kulilinda taifa kwa maisha yake na vizazi vijavyo.
    alisema DCI Ilembo.
    Mapema mwaka huu polisi walikamata mabegi mawili yakiwa na dawa za kuelvya katika chumba cha kuondokea abiria, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.


  • July 11, 2014

  • DAKTARI MWINGINE FEKI ANASWA HOSPITALI YA RUFAA MORO


    DAKTARI MWINGINE FEKI ANASWA HOSPITALI YA RUFAA MORO
    Daktari feki akielekea kwenye gari.
    Askari Polisi wakimtoa nje daktari feki, Karume Habibu (22) kutoka kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako alihojiwa kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano zaidi.
    Daktari feki, Karume Habibu akiingizwa kwenye gari.
    ...Akificha uso kukwepa kamera za GPL.
    Baadhi ya wafanyakazi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro wakishuhudia tukio hilo.
    WIMBI la madaktari feki kuingia katika hospitali wakijifanya madaktari na kutoa huduma mbalimbali limeendelea ambapo leo amenaswa mwingine mkoani Morogoro.
    Daktari huyo feki aitwaye Karume Habibu (22)amenaswa katika Hospitiil ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa mahojiano zaidi.
    GP


  • SEKESEKE ZITO DEREVA NA TRAFIKI....!SHUHUDIA MWENYEWE



    SEKESEKE ZITO DEREVA NA TRAFIKI....!SHUHUDIA MWENYEWE
    Trafiki akimdhibiti dereva wa gari dogo aina ya Toyota Pick up.
    SEKESEKE la aina yake kati ya dereva wa gari dogo aina ya Toyota Pick up na trafiki ambao majina yao hayakujulikana mara moja liliibuka na kuzua maswali mengi kwa mashuhuda huku mambo ya rushwa yakitajwatajwa.  Tukio hilo lilizozua maswali mengi liliibuka juzi Jumatano, Bamaga, Mwenge jijini Dar jirani na kituo cha mafuta cha Bamaga.
    Katika tukio hilo, dereva huyo na trafiki walikuwa wakikunjana, ambapo dereva alikuwa akilalamika kuonewa (Haikujulikana kivipi) wakati askari huyo wa usalama barabarani akisisitiza kuwa jamaa huyo alivunja sheria.
     
    Gari aina ya 'Land Rover' (break down) lililotumika kuvuta gari la aina ya Toyota Pick up la dereva huyo. 
     ILIKUWAJE?
    Kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu 'OFM' cha Global Publishers, kikiwa katika pitapita zake za kusaka matukio na kuhakikisha maadili hayavunjwi ndipo kilipokutana na kisanga hicho cha kushangaza.

    Trafiki alisikika akimwambia dereva kuwa amevunja sheria za barabarani huku gari lake likiwa bovu hivyo aliamuru gari hilo kuvutwa hadi kituoni kwa ajili ya ukaguzi lakini dereva huyo alikataa.
     
    ...ilikuwa ni vigumu sana kwa dereva huyo kukubali gari lake kukamatwa.
     DEREVA
    Pamoja na kuelezwa kuwa gari lake lilikuwa na matatizo na mahali alipoegesha hapakuwa sahihi, dereva huyo alipayuka: "Nawajua nyie trafiki, kazi yenu ni kuonea watu sasa mimi sitoi kitu hapa, labda mniue."Siendi popote, mkiondoa gari nalala mbele yake ili mnigonge nife, mimi nimesema silitoi."
     
    ...dereva akizidi kubisha kwa uamuzi uliochukuliwa na afisa usalama wa barabarani 'trafiki' .
     TRAFIKI
    Trafiki huyo aliyeonekana kuwa makini na kazi yake, hakuwa na makuu, zaidi alitaka gari livutwe hadi kituoni huko sheria ingefuata mkondo wake baada ya ukaguzi.
     Mashuhuda wa tukio hilo, waliliambia Ijumaa kuwa, kilichohitajika ilikuwa ni busara ya masikilizano kuliko kuvutana kwa maneno na afisa wa polisi.
     
    Afisa usalama wa barabarani akisisitiza kulichukua gari la dereva huyo kwa ukaguzi zaidi.
     "Sasa kama gari lake anajua ni zima, anabishana nini na polisi? Ikiwa anajiamini kuwa aliegesha sehemu sahihi, hofu yake ni nini? Kama kweli anajua yupo sawa, anatakiwa kukubali kwenda polisi, gari likakaguliwe. 

    "Wakati mwingine unaweza kuwalaumu tu askari, kumbe ni tabia ya watu kukataa kutii sheria bila shuruti. Sasa anafikiri kwa maneno makali anayotoa kwa huyo askari atamwachia?
     
    Raia wakishuhudia mkasa huo uliotokea katika kituo cha mabasi yaendayo Mwenge cha Bamaga.
     "Anasema eti hatoi kitu, kwani kaombwa rushwa pale au anadhani kila trafiki anayemkamata dereva aliyevunja sheria anataka rushwa?" alisikika shuhuda mmoja akihoji kwa jazba.
    Hata hivyo, pamoja na mkwara wa jamaa huyo, gari lake lilifanikiwa kuvutwa kuelekea polisi ambapo jamaa huyo alipanda gari lingine kulifuata.


  • LAANA : SHOGA AEJIFUNGUA MTOTO WA KIUME



    LAANA : SHOGA AEJIFUNGUA MTOTO WA KIUME

    Hii imeripotiwa kutoka katika mtandao mmoja huko Nigeria Kuwa Mwanaume huyu Shoga amejipatia Mtoto wa kiume  akiwa amezalishwa na mwanume mwenzakesoma maelezo hapa 
    This is the emotional moment as gayy dads gives birth and met their son for the first time..The couple's emotional moment was captured by photographer Lindsay Foster who wrote
    "I had the opportunity to photograph this amazing birth on June 27 for a surrogate and two expecting and anxious daddies. Hours were spent with them in the hospital room while the surrogate mom was laboring and I got to know them quite well.They are two compassionate people who felt all the emotions that every new parent feels. They asked all appropriate questions of the birthing mom and the midwife and educated themselves as best as they could for their son's arrival. I am so proud of these two dads."


  • MOTO MKUBWA WATEKETEZA VIBANDA VILIVYOPO NYUMA YA STENDI YA DALA DALA MKOANI DODOMA NA KUSABABISHA HASARA




    MOTO MKUBWA WATEKETEZA VIBANDA VILIVYOPO NYUMA YA STENDI YA DALA DALA MKOANI DODOMA NA KUSABABISHA HASARA

     Moto huo mkubwa uliteketeza mali nyingi sana za dhamani wafanya biashara wa maeneo hayo ulidumu takribani masaa 3 ambapo jeshi la zimamoto pamoja na wananchi walifanya jitahada za kuudhibiti moto huo ili usiweze kuendele, huku jeshi la polisi likiimarisha ulinzi wa kutosha kutokana na vibaka kuvamia eneo hilo.


    Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo eneo hilo walidai chanzo cha moto huo kilionekana kutokea kwenye nguzo ya umeme iliyokuwa maeneo hayo ambapo inasemekana ndio sababu kubwa ya moto huo.
     












    CDT:BOSS NGASA TZ


  • July 08, 2014

  • Mama aua watoto wake watatu waliokuwa na ulemavu.


    Mama aua watoto wake watatu waliokuwa na ulemavu.
    totoo1
    Mama mmoja nchini Uingereza amekiri kuwauwa watoto wake watatu waliokuwa na ulemavu.Mama huyo Tania Clarence, mwenye miaka 42, amekiri kuwa na hatia kwa kosa la kuwauwa watoto wake ambao ni mapacha wa kiume wenye umri wa miaka mitatu na wa kike aliyekuwa na umri wa miaka minne kwa misingi ya kukwepa majukumu.

    Watoto hao walikutwa ndani ya nyumba yao.
    Clarence amekuwa akitibiwa ugonjwa wa akili Kusini mwa London ambapo alishtakiwa April 24 mwaka huu


  • July 05, 2014

  • HILI NDIYO DARAJA HATARI MJINI SHINYANGA,UKIPITA HAPO JIANDAE KUCHARANGWA MAPANGA


    HILI NDIYO DARAJA HATARI MJINI SHINYANGA,UKIPITA HAPO JIANDAE KUCHARANGWA MAPANGA
    DARAJA HILI LIPO MAENEO YA MAGEREZA SHINYANGA MJINI SHINYANGA BARABARA YA SHINYANGA MWANZA NI MAARUFU KAMA DARAJA LA MHUMBU.
    PAMOJA NA DARAJA HILI KUWEPO KARIBU NA MAGEREZA LAKINI SASA LIMEGEUKA DARAJA LA KUMWAGA DAMU, KWANI IMEPITA ZAIDI YA MWAKA SASA WAKABAJI NA VIBAKA WAMEKUWA KAMA UWANJA WAO KWA KUCHARANGA WATU MAPANGA ,KILA KUKICHA WATU WANAOPITA ENEO HILO. 

    NA SASA HIVI WATU WANAOTUMIA DARAJA HILI IKIFIKA SAA 1 JIONI TU HUWEZI KUPITA BILA KUPIGWA PANGA.
    VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA SHIKAMONI!!


  • July 04, 2014

  • MAJAMBAZI WATATU WAUWAWA JIJINI ARUSHA



    MAJAMBAZI WATATU WAUWAWA JIJINI ARUSHA
    WATU watatu wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi wameuwawa jijini Arusha walipokuwa katika harakati ya kwenda kupora mamilioni ya fedha zilizokuwa zinapelekwa benki na kampuni ya Arusha Islamic Centre inayohusika na utengenezaji na uuzaji wa vigae iliyopo eneo la Esso  mjini hapa.



    Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Arusha leo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas amesema kuwa,majambazi hao watatu  waliuawa jana tarehe 3 eneo la TBL -Njiro  wakiwa kwenye harakati za kwenda kupora fedha hizo.

    Alisema kuwa, majambazi hao walikuwa mahali wanapanga njama majira ya saa 4;20 asubuhi wakisubiria kuteka gari lililokuwa limebeba  fedha zilizokuwa zinapelekwa benki zaidi ya milioni 100  huku wakiwa na gari aina ya Toyota Corola yenye namba za usajili T 762 CWE.

    Alisema kuwa, raia wema walitoa taarifa kuhusiana na tukio hilo ndipo  polisi walifika eneo ambalo majambazi hao walikuwa wamejificha katika  eneo la unga ltd relini ambapo majambazi hao walishtuka na kuanza kuirishia gari hiyo ya polisi risasi.




    Kamanda Sabas alisema kuwa,Askari wake walioona Majambazi hao wanawamiminia risasi kama mvua,ndipo na wao walipojibu mashambulizi na na kufanikiwa kuwawa kwa majambazi hao watatu na kufanikiwa kuchukua silaha yao aina ya shortgun yenye namba A 947514 M aina ya  Pumpaction ikiwa na risasi 3 .



    Kamanda alisema kuwa, bado majina ya majambazi hayo hayajafahamika ambapo wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount Meru.


    Aidha Kamanda aliwashukuru wananchi kwa juhudi kubwa sana walizoonyesha na ushirikiano hadi kukamatwa kwa majambazi hayo na kuwataka kuendelea kuongeza juhudi hizo zaidi.


  • HATARI: Angalia hisia za Mashoga 2 huko Canada waliopata mtoto wao wa kwanza



    ngalia hisia za Mashoga 2 huko Canada waliopata mtoto wao wa kwanza



    This is the emotional moment two dads met their son for the first time. The couple's emotional moment was captured by photographer Lindsay Foster who wrote
    "I had the opportunity to photograph this amazing birth on June 27 for a surrogate and two expecting and anxious daddies. Hours were spent with them in the hospital room while the surrogate mom was laboring and I got to know them quite well. They are two compassionate people who felt all the emotions that every new parent feels. They asked all appropriate questions of the birthing mom and the midwife and educated themselves as best as they could for their son's arrival. I am so proud of these two dads."
    The pictures liked over 6,000 times also attracted negative comments and the couple, Mr. Barone and Mr. Nelson said.

    "Thank you to everyone out there who has taken the time to like, comment and share our picture! This was truly an incredible moment in our lives that will be captured forever by the lovely Lindsay Foster Photography. We are so lucky that we have a beautiful, healthy baby boy! All comments posted are respected, although we may not agree with the negative ones, the positive ones far outweigh the negative. Everyone is entitled to their own opinion. This is a moment of pure love and acceptance. Milo is surrounded by unconditional love and he will grow up knowing many different types of families and accept everyone, (intolerant people included). Milo was born during World Pride. This picture represents everything Pride is about. Love has no colour nor gender nor sexual preference. Love is unconditional. Thank you again from the bottom of our hearts! xxoo"


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.