November 11, 2015

  • TRA YAJIVUNIA KASI KATIKA UKUSANYAJI KODI.



    TRA YAJIVUNIA KASI KATIKA UKUSANYAJI KODI.
    index
     
    ISO
    9001:2008 CERTIFIED
    TAARIFA YA MAKUSANYO YA KODI
    Mamlaka
    ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya shilingi  trililion 3.77kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba 2015 ambayo ni sawa na
    asilimia  97.6. ya lengo la makusanyo ya sh trilioni 3.87 ikiwa ni jitihada za TRA kutekeleza mkakati wa serikali ambao
    unaitaka kukusanya Ths . Trililioni 12.3
    kwa mwaka wa fedha 2015/2016. 
    Kwa
    mujibu wa Kamishna  Mkuu wa TRA Rished
    Bade, mwezi Julai TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 849,582.9ambacho ni asilimia 99.4 ya lengo la kukusanya shilingi
    bilioni 854,922.9.
    Mwezi
    Agosti TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 890,536.7 ambacho ni asilimia 101.5 ya lengo la kukusanya shilingi
    biilioni 876,974.2 .ambapo mwezi Septemba jumla ya shilingi trilioni1,067,888.3 zilikusanywa ikiwa ni
    asilima 91.7 ya lengo trilioni 1,163,999.4
    kwa mwezi mwezi Oktoba TRA  iilkusanya
    shilingi bilioni 970,089.6 ikiwa ni
    asilima 99.3 ya lengo la kukusanya shilingi
    bilioni 976,441.5.
    Taarifa
    ya mwenendo wa makusanyo ilipitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TRA katika kikao
    cha bodi kilichofanyika jana tarehe 10 Novemba 2015 katika ofisi za makao makuu
    ya TRA" amesema Bw. Bade.
    Mafanikio
    katika makusanyo haya yametokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na mamlaka
    baada ya kusaini mkataba na Waziri wa Fedha ambapo Kamishna Mkuu alisaini
    mkataba na kila Mkuu wa Idara na wakuu wa Idara kusaini mikataba na wafanyakazi
    walioko chini yao ili kila mfanyakazi kuwajibika ipasavyo.
    Wito
    wa TRA ni kwa mfanyabiashara na wadau wote wa kodi kutimiza wajibu wao wa
    kulipa kodi kwa hiari ili kuchangia pato la taifa.
    Sambamba
    na hilo TRA imepokea kwa furaha sana wito wa Mheshimiwa Rais John Pombe
    Magufuli wa kuhimiza ukusanyaji wa mapato bila woga na bila kumwonea mtu.
    "Pamoja
    Tunajenga Taifa Letu"
    Rished Bade
    KAMISHNA MKUU


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.