Ndege moja iliyokuwa              imewabeba wahamiaji 500 raia wa Nigeria imetua mjini Lagos              kutoka Uingereza.
          Wahamiaji hao 500              wametimuliwa na maafisa wa Uingereza baada ya kupatikana              wakiishi nchini humo kinyume cha
           sheria.Wengi wao wameelezea              kutoridhishwa kwao na hatua ya kurejeshwa nchini Nigeria kwa              nguvu.
          Mmoja wao amemueleza              mwandishi wa habari wa BBC aliyeko Lagos kuwa polisi nchini              Uingereza walimkamata na kumfurusha mara moja pasi na kuma              ruhusa ya kutwaa vitu vyake.
          Wachache kati yao              ambao wamesema hawana jamaa mjini Lagos wamesalia katika              uwanja wa ndege wasijue pa kwenda.
          Hivi majuzi serikali              ya Nigeria ilielezea kutoridhishwa kwake na mpango ya              utawala wa Uingereza ya kuwafurusha wahamiaji elfu              thelathini 30,000 kutoka Uingereza.
          Nigeria inasisitiza              inataka sheria zifwatwe kikamilifu kabla ya kutimuliwa kwa              raia wake 29,000 kutoka Uingereza.
          Aidha Nigeria inataka              Uingereza ihakikishe kuwa wale wanaorejeshwa ni wenye siha              nzuri na wale wanaoweza kusafiri kwa ndege.
          Vilevile Nigeria              inataka Uingereza ihakikishe kuwa wale wanaopelekwa Nigeria              wanaasili na vyeti halali vya Nigeria na kuwa wanaweza              kujishughulisha kimaisha kabla ya kuwarejesha Nigeria na              kuwabwaga huko.
        
0 comments:
Post a Comment