Mgonjwa aliyeahidiwa matibabu na Rais John Magufuli, Chacha Makenge amefanyiwa uchunguzi na majibu ya kipimo cha MRI na sasa anasubiri upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Chacha aliyekuwa amekwama                      kupatiwa matibabu kwa kukosekana vipimo vya CT Scan                      na MRI, amepatiwa matibabu hayo kwenye hospitali                      hiyo ya rufani chini ya uangalizi wa madaktari                      bingwa.
              Akizungumza na gazeti                      hili jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Taasisi ya                      Mifupa Muhimbili (Moi), Almas Jumaa alisema, Chacha                      alikuwa mgonjwa wa kwanza kufanyiwa kipimo cha MRI                      baada ya kutengamaa Novemba 11, amegundulika kuwa na                      tatizo kwenye uti wa mgongo.
              Alisema, awali mgonjwa                      huyo alifanyiwa kipimo cha CT Scan nje ya hospitali                      hiyo na kugundulika ana matatizo kadhaa, lakini MNH                      ilihitaji kujiridhisha na ndipo walipogundua                      mvunjiko katika pingili zake za uti wa mgongo.
              " Kwa sasa, anaendelea                      vizuri na baada ya vipimo madaktari wamegundua                      katika uti wake wa mgongo kuna mahali kulikuwa na                      mvunjiko na inavyoonyesha aliupata muda mrefu,                      alikuwa akiishi na tatizo hilo, madaktari wameshauri                      wiki ijayo afanyiwe upasuaji ili kurekebisha tatizo                      hilo," alisema Almas.
              Alipotembelewa katika                      wodi ya Sewahaji, Chacha aliyelazwa hospitalini hapo                      Septemba 8, alisema tangu Rais Magufuli afanye ziara                      yake, wamekuwa wakitibiwa kwa wakati kutokana na                      mashine hiyo kurekebishwa.
              "Nimpe pole na pongezi                      rais kwa kazi ngumu aliyoifanya, ameunganisha daraja                      baina ya MNH na Moi, awali ilikuwa ngumu, lakini                      sasa kuna urahisi wa huduma, matengenezo ya vipimo                      yameokoa wagonjwa wengi.
              "Awali, kupata vipimo nje                      ilichukua muda ili kukamilika," alisema Chacha,                      aliyedai alisubiri vipimo vya MRI na CT Scan kwa                      miezi miwili.
              Alipoulizwa hali halisi                      ya kipimo cha CT Scan, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa                      Muhimbili, Aminiel Aligaesha alisema bado mafundi                      kutoka Kampuni ya Phillips ya Uholanzi wanaendelea                      na matengenezo ya mashine hiyo.
              "Kipimo cha CT Scan bado                      kipo kwenye matengenezo na pindi kitakapotengamaa                      tutaufahamisha umma na kwa kuwa wanaotengeneza                      wanatokea Kampuni ya Muccos, itakapokuwa imeleta                      shida watakuja mafundi kutoka Uholanzi," alisema                      Aligaesha.
              Novemba 9, Rais Magufuli                      alifanya ziara ya kushtukiza MNH na kukutana na                      kasoro lukuki, zikiwamo za wagonjwa kulala sakafuni,                      mashine za vipimo na uchunguzi wa magonjwa kutofaya                      kazi kwa zaidi ya miezi miwili.
            
0 comments:
Post a Comment