November 28, 2015

  • BREAKING NEWS : Kigogo CCM kortini kwa kulawiti wanawe ... Mmoja ana mwaka mmoja, mwingine miaka mitano.



    BREAKING NEWS : Kigogo CCM kortini kwa kulawiti wanawe ... Mmoja ana mwaka mmoja, mwingine miaka mitano.
     Katibu Msaidizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Rogers Msangi (44), amepandishwa kizimbani mjini Moshi akituhumiwa kuwalawiti watoto wake wawili.

    Msangi, ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Mwanga, alipandishwa kizimbani jana mbele ya Hakimu Mkazi, Anthony Ngowi. Msangi alikanusha tuhuma dhidi yake na alipelekwa rumande katika Gereza Kuu la Karanga, Moshi baada ya wadhamini wake wawili kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

    Makosa anayodaiwa kutenda kigogo huyo yanaangukia katika shtaka la kumwingilia binadamu kinyume cha maumbile kinyume cha kifungu 154 cha Kanuni ya Adhabu. Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Novemba 16 mwaka huu, katika eneo la Mwangodi wilayani Mwanga, mshtakiwa alimlawiti mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu.

    Katika shtaka la pili, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alidai kati ya Oktoba na Novemba mwaka huu katika eneo hilo, mshtakiwa alimlawiti mtoto wake mwingine mwenye umri wa miaka mitano.

    Mshtakiwa huyo anayetetewa na Wakili Ralph Njau alikanusha mashtaka hayo. Hakimu Ngowi alimweleza mshtakiwa kuwa dhamana yake iko wazi kwa masharti kwamba asaini hati ya dhamana ya Sh6 milioni na awe na wadhamini wawili wa kuaminika ambao ni watumishi wa umma na wenye vitambulisho halali.

    Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na hivyo alipelekwa rumande hadi Desemba 7 kesi hiyo itakapotajwa.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.