Katibu                Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dkt.                Yamungu Kayandabila akizungumza na wadau wa Mawasiliano,                Sayansi na Teknolojia katika mkutano maalum wa siku ya                Sayansi Duniani. Kushoto kwake ni Afisa utawala na fedha                wa UNESCO, Spencer Bokosha ambaye alimwakilisha Mkurugenzi                Mkazi wa UNESCO- Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues. Mkutano                huo ulifanyika katika ukumbi wa wizara hiyo jijini Dar es                Salaam Novemba 10. 2015. (Picha zote na Andrew Chale,                Modewjiblog).
        Na                Andrew Chale, Modewjiblog
        [DAR                ES SALAAM-TANZANIA] Tanzania kupitia wadau wa Sayansi                nchini imedhamilia kupiga hatua zaidi katika kufikia                malengo ya Agenda 2030 kwa kuchangamkia fursa za maendeleo                katika Sayansi.
        Hayo                yameelezwa jijini hapa wakati wa wadau wa Mawasiliano,                Sayansi na Teknolojia, walipokutana katika majadala wa                Siku ya Sayansi Duniani kwa ajili ya Amani na Maendeleo                (World Science Day for Peace and Development).
        Akisoma                neno, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na                Teknolojia, Dkt. Yamungu Kayandabila amelipongeza Shirika                la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),                katika kukuza Sayansi nchini.
        Dkt.                Yamungu ameelezea kuwa, nchi yoyote ile ilikuendelea,                inategemea Sayansi hivyo kwa Tanzania ni wakati wa                kuchangamkia fursa ili kufikia malengo na Agenda 2030.
        "Tanzania                tuna fursa nyingi na za kutosha. Tuna Nyuklia na hii ni                uchumi tosha tutakapofanyia kazi kwa malengo tutafika                mbali kwani inahitaji Sayansi ya kina.
        Navipongeza                vyuo mbalimbali vilivyopo nchini ikiwemo DIT, Nelson                Mandela cha Arusha, Chuo cha Sayansi Mbeya na vingine                vingi" ameeleza Dk. Yamungu.
        Aidha,                Dkt. Yamungu ametaka Sayansi kuendana na suala la ulinzi                wa chakula na miundombinu mingine ikiwemo suala la maji                huku akihimiza wanafunzi kuyapenda na kuyasoma masomo ya                Sayansi na suala la umuhimu wa Sayansi na namna inavyoweza                kuathiri maisha ya watu kila siku.
                Afisa                Utawala na Fedha wa UNESCO, Spencer Bokosha ambaye                alimwakilisha Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa UNESCO-                Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues akisoma ujumbe maalum wa                siku ya Sayansi Duniani wakati wa mkutano huo wa wadau wa                Sayansi.
        Kwa                upande wake Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia Prof.                Evelyn Mbede amepongeza wadau wa Sayansi na Teknolojia kwa                kujimuika katika maadhimisho ya siku hiyo ya Sayansi                Duniani ambapo ameelezea kuwa Wizara yake milango ipo wazi                kwa wadau wote katika kuhakikisha wanapiga hatua katika                kukuza na kuendeleza Sayansi hapa nchini.
        Kwa                upande wake, Afisa Utawala na Fedha wa UNESCO, Spencer                Bokosha ambaye alimwakilisha Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi                wa UNESCO- Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues alipongeza                juhudi za Serikali ya Tanzania katika kutilia mkazo suala                la Sayansi na Teknolojia na kufanya suala hilo kuwa                mtambuka kwa maendeleo ya vizazi vya sasa na baadae.
        Akisoma                ujumbe maalum kutoka UNESCO, Bw. Bokosha alieleza kuwa                kupitia Sayansi na Teknolojia na ubunifu, maendeleo ya                Taifa endelevu, uimarishaji wa mazingira ikiwa ni pamoja                na kuongezeka kwa maandalizi kwa ajili ya kukabiliana na                Mabadiliko ya Tabianchi na madhara yake hivyo Sayansi                inahitajika kwa kiwango kikubwa juu ya hilo.
        Aidha,                ameeleza kuwa, UNESCO imekuwa mstari wa mbele katika                kuanzishwa kwa moduli za elimu ya Mazingira katika shule                za Sekondari.
                Profesa                John Kondoro Mkuu wa Chuo cha Teknolojia cha jijini Dar es                Salaam – (DIT) akitoa mada katika mkutano huo wa wadau wa                Sayansi wakati wa maadhimisho ya siku ya Sayansi.
        Akinukuu                ujumbe maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi                Irina Bokova katika ujumbe alieleza:
        "Hii                ni siku ya Sayansi Duniani kwa amani na Maendeleo na                imekuja miezi miwili baada ya makubaliano ya Agenda 2030                ya maendeleo endelevu.
        Hivyo                Serikali zote zitambue nguvu ya Sayansi ya kutoa majibu                muhimu kwa usimamizi mzuri wa maji kwa ajili ya hifadhi na                matumizi endelevu ya bahari, ulinzi wa mazingira na viumbe                hai, ilikukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na majanga                na kuendeleza uvumbuzi na kuondokana na umasikini na                kupunguza tofauti" alieleza katika nukuu hiyo.
                Afisa                kutoka UNESCO NAT.COM, Bw. Joel Samuel akitoa mada katika                mkutano huo wa wadau siku ya Sayansi Duniani.
                Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF,                        Godfrey Simbeye, akifafanua jambo wakati wa                        mjadala huo juu ya maendeleo ya Sayansi na                        Teknolojia nchini katika mkutano uliowakutanisha                        wadau wa Sayansi katika maadhimisho ya Siku ya                        Sayansi Duniani.
            Wadau                wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakiwa katika picha                ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa siku                ya Sayansi Duniani.
        
0 comments:
Post a Comment