Wataalamu wa jiolojia wameitwa kuchunguzwa ni jinsi            gani ardhi ilipasuka na kumeza magari 12 katika maegesho ya            magari jijini Mississippi.
        Shimo kubwa, la urefu wa futi 400 (120m) na upana wa            futi 35 (11m), lilitokea baadaye Jumamosi katika eneo la            Meridian, karibu na barabara kuu ya Alabama.
        Eneo hilo limekuwa likipokea mvua kubwa katika kipindi            cha wiki mbili zilizopita, kwa mujbiu wa gazeti la Meridian            Star.
        Hakuna aliyejeruhiwa katika kisa hicho, na wahandisi            wanatarajiwa kudadisi uthabiti wa ardhi eneo hilo leo.
        Bw Buck Roberts, tmkurugenzi wa usalama wa umma eneo            la Meridian, aliambia gazeti hilo kwamba hilo halionekani kuwa            shimo la kawaida ambalo hutokana na sehemu inayohifadhi maji            chini ya ardhi kukauka na ardhi kuporomoka.
        BBC.
        
0 comments:
Post a Comment