Watoto waliozaliwa              wikendi iliopita nchini Uingereza wana hatari kubwa ya              kufariki ikilinganishwa na wale waliozaliwa siku za              juma,kulingana na watafiti.
          Utafiti uliofanyiwa              zaidi ya watoto milioni 1.3 waliozaliwa umebaini kwamba kuna              vifo 7.1 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa wikendi.
          Hii ni asilimia 7              zaidi ikilinganishwa na siku za juma.
          Taasisi ya Imperial              mjni London imesema kuwa iwapo siku zote zingekuwa na              viwango sawa vya vifo kama vile siku ya Jumanne,ambayo ina              viwango vya chini kungekuwa na vifo 770 vichache kwa mwaka.
          Watafiti hao wamesema              kuwa huku viwango vya vifo vikiwa chini,tofauti hiyo ni              muhimu na kuzua wasiwasi kuhusu viwango vya utunzaji              wikendi.
          Mnamo mwezi Septemba              ,utafiti tofauti ulibaini kwamba wagonjwa waliolazwa ili              kuhudumiwa wakati wa wikendi walikuwa na hatari zaidi ya              kufariki katika kipindi cha siku 30 ikilinganishwa na wale              waliolazwa katika siku za juma.
          Utafiti huo umetumiwa              na mawaziri katika harakati zao za kutaka kuongeza huduma              wakati wa wikendi,sera ambayo imezua mgogoro baina yao na              madaktari na kusababisha madaktari wapya kupiga kura              wakiunga mkono kufanya mgomo kuanzia juma lijalo.
          Utafiti huo              mpya,uliochapishwa na jarida la matibabu la Uingereza              uliangazia visa vya watoto wanaofariki wakiwa tumboni kati              ya kipindi cha siku saba wakiwa hospitalini kutoka mwaka              2010 hadi 2012.
        
0 comments:
Post a Comment