Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.            Jakaya Mrisho Kikwete ameamua na ameitangaza kesho, Alhamisi,            Novemba 5, mwaka huu, 2015, kuwa Sikukuu na siku ya mapumziko. 
                        Rais Kikwete amefanya uamuzi huo, ili kuwawezesha Watanzania            kushiriki katika sherehe za kuhitimisha Uongozi wa Serikali ya            Awamu ya Nne na kuingizwa madarakani Mheshimiwa Dkt. John            Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muung            ano wa Tanzania. 
                        Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo Jumatano,            Novemba 4, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi            Ombeni Yohana Sefue, Rais Kikwete ametoa uamuzi huo kwa mujibu            wa mamlaka aliyo nayo chini ya Kifungu cha 3 cha Sheria ya            Sikukuu za Kitaifa.
         Imetolewa na:
        Kurugenzi            ya Mawasiliano ya Rais,
        Ikulu,
        DAR                ES SALAAM.
        4            Novemba, 2015
        
0 comments:
Post a Comment