November 09, 2015

  • MWANAMUZIKI MKONGWE CAPT JOHN SIMON AFARIKI DUNIA



    MWANAMUZIKI MKONGWE CAPT JOHN SIMON AFARIKI DUNIA
    IMG_9699

    Capt John Simon

    MWANAMUZIKI mkongwe ambaye  kwa siku za karibuni alikuwa kwenye bendi ya Shikamoo Jazz, Capt John Simon, amefariki dunia leo katika hospitali ya Muhimbili. Mzee huyu alikuwa mmoja ya waanzilishi wa NUTA Jazz band, na baadae kadri ya maelezo yake mwenyewe, Mheshimiwa Rashid Kawawa, ndie alimtoa NUTA Jazz na wanamuziki wengine na kwenda kuanzisha JKT Jazz Band, iliyopata umaarufu kama Kimbunga Stereo.

    FIL6

    Waimbaji wa NUTA Jazz Band, toka kulia John Simon, Muhidin Gurumo, na kushoto Ally Akida

    Mzee John Simon pia alikuwa mwanzilishi wa Shikamoo Jazz Band, bendi ambayo ameitumikia mpaka siku zake za mwisho. Capt John Simon pia alikuwa makamu mwenyekiti wa CHAMUDATA mwishoni mwa miaka ya 90, akiwa makamu wa John Kitime, na hatimae kuwa mwenyekiti baada ya John kitime kujiuzuru nafasi yake. Taratibu za mazishi zitapatikana baada ya ndugu kukutana. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Tabata Kimanga.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.