November 08, 2015

  • WAWEKEZAJI KUTOKA HONGKONG WAWASILI



    WAWEKEZAJI KUTOKA HONGKONG WAWASILI

    KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Kitengo cha viwanda vya nguo katika Wizara ya Viwanda na Biashara, juzi kimepokea timu ya wawekezaji ya VF Corporation kutoka Hong Kong.


    Taarifa iliyotolewa na TIC jana, ilisema kituo hicho kimewataka wawekezaji hao kuiangalia Tanzania kama eneo muhimu kwao kufanya uwekezaji katika bara la Afrika kutokana na kuwa na mazingira na sera rafiki ya kufanyia biashara.
    TIC imebainisha kuwa Tanzania ina wananchi wapatao milioni 48, hivyo kuwa na soko zuri kwa bidhaa zao na pia upatikanaji wa malighafi ni rahisi, kuna nguvu kazi ya kutosha na jambo kubwa ni amani na utulivu wa nchi.
    VF Corporation iliyoanzishwa mwaka 1899, inaingiza kipato cha dola bilioni 12.3 na inajulikana kimataifa katika kutengeneza viatu na vifaa vyake akiwa na bidhaa zaidi 30, washiriki wa biashara 60,000.
    Baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa ni mavazi ya jeans, michezo, viatu vya michezo.
    Kwa sasa VF Corporation inaagiza bidhaa katika kiwanda kimoja hapa nchini na inaangalia uwezekano wa kupanua wigo wa manunuzi katika viwanda vingine nchini.
    Katika ziara yao, wawekezaji hao wamepitia upya mazingira ya uwekezaji nchini kwa lengo la kuangalia uwezekano wa kuhamasisha viwanda vyao vingine kuangalia Tanzania kama asili ya viwanda vya nguo.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.