Rais wa              Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemuonya mwenzake wa Urusi              Vladimir Putin 'kutocheza na moto' kuhusu swala la taifa              lake kuidungua ndege ya kijeshi ya Urusi
        .Bwana Erdogan pia amesema kuwa              anataka kukutana na bwana Putin ana kwa ana katika              mazungumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa ili kusuluhisha              mzozo huo.
        Bwana Putin anataka kuombwa              msamaha na Uturuki kabla ya kuzungumza na Erdogan ,msaidizi              wa rais huyo amesema.
        Urusi imeamua kusitisha mpango wa              kusafiri bila viza miongoni mwa raia wa mataifa hayo mawili              kwa mujibu wa waziri wa maswala ya kigeni nchini humo.
        Uturuki inasema kuwa ndege hiyo              ilikuwa katika anga yake ilipolengwa,lakini Urusi inasema              kuwa ilikuwa katika anga ya Syria.
        ''Ningependa kukutana na bwana              Putin ana kwa ana mjini Paris'',alisema bwana Erdogan katika              hotuba yake katika runinga.
        ''Ningependa kusuluhisha tatizo              hili.Inaudhi kuona kwamba swala hili limeongezewa chumvi''.
        Lakini pia amesema kuwa Uturuki              haitaki kuharibu uhusiano wake na Urusi.
        Waziri wa maswala ya kigeni nchini              Urusi Sergei Lavrov ameonya kuwa kisa hicho kinaweza              kuathiri maslahi ya Uturuki.
        
0 comments:
Post a Comment