November 04, 2015

  • Chumba cha maiti Dodoma chazua balaa


    Chumba cha maiti Dodoma chazua balaa
    Jengo la Hospitali ya Rufaa ya                mkoa wa Dodoma
    Jengo la Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma
     
     
    MAJOKOFU ya chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma hayafanyi kazi kwa muda wa siku nne sasa hali ambayo imesababisha usumbufu mkubwa kwa wafiwa wanaopeleka maiti zao katika hospitali hiyo
    Mmoja wa wafia aliyejitambulisha kwa jina moja la Winfrida kutoka Maili mbili amesema wameshindwa kuhifadhi mwili wa marehemu ambaye ni wifi yake na kulazimika kuzika bila watoto wake waliopo nje ya nchi kufika kushuhudia mama yao anavyozikwa.
    Hali hiyo imethibitishwa na mmoja kati ya wahudumu wa kitengo cha kuhifadhia maiti katika hospitalini hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja na Joseph amesema majokofu yote ya chumba hicho muhimu hayafanyi kazi.
    "Hali ni mbaya kwa kweli kwa sababu kwa sasa tunalazimika kutumia dawa ili kuzuia maiti zisioze .
    "Lakini pamoja na hayo tunalazimika kuwashauri wafiwa kuchukua maiti zao mapema kwani dawa hazina uwezo wakuhifadhi maiti kwa muda mrefu," alieleza.
    Aidha, Joseph aliongeza kuwa uongozi wa hospitali una taarifa juu ya kuharibika kwa majokofu hayo, na kuongeza kuwa: "Sifahamu hatua ambazo uongozi umechukua mpaka sasa kuyarekebisha majokufu, ila hali ni mbaya na inahitaji ukarabati wa haraka sana."
    Juhudi za kuongea na Mganga Mkuu wa Mkoa juu ya swala hili ziligonga mwamba baada ya kuambiwa kwamba yupo likizo wakati wasaidizi wake wote wakidaiwa kuwa katika vikao.
    Juhudi zaidi za kutaka kuonana na wasaidizi hao au kuzungumza nao kwa simu ziligonga mwamba.
    Msaidizi wa ofisi ya mganga mkuu ambaye akutaja jina lake alikuwa kizingiti kwa kukataa katakata kutoa namba ya mganga mkuu au msaidizi kwa madai kuwa wameisha katazwa kutoa namba za simu za wakuu hao kwa wateja.
    "Sasa hapa hakuna hata daktari yeyote wakuongelea jambo hili, wote hawapo na kiukweli, kutokana na kanuni za kazi za hapa, haturuhusiwi kutoa namba ya simu ya mganga yeyote yule. Labda ujaribu kurudi baadaye," amesema mmoja wa wasaidizi wa ofisi ya mganga mkuu.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.