Na              Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
        WANANCHI wa Kata ya                Saranga Manispaa ya Kinondoni wametakiwa kujitokeza kupiga                kura ya Diwani Novemba 15 mwaka huu.
        Akizungumza na                waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Manispaa ya                Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty amesema kuwa kufanya                uchaguzi huo kunatokana na kuharibika kwa uchaguzi wa                Oktoba 25 ulisababishwa na vurugu.
        Amesema wananchi                wanaotakiwa kupiga kura kwa kata hiyo ni wale                waliojiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura.
        Natty amesema                waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura  ni 58,611                ambao ndio wataoruhusiwa kutimiza haki yao ya kikatiba ya                kupiga kura kwa diwani wanayemtaka kuongoza kata hiyo.
        Amesema vituo vya                kupiga vitafunguliwa majira ya saa moja asubuhi na                kufungwa saa 10 jioni na baada ya hapo zoezi likiwa                limekamilika la uhesabiaji kura atatangazwa mshindi katika                uchaguzi huo.
        Uchaguzi wa diwani                katika kata hiyo ilitokana na vurugu kubwa ambazo zilianza                majira ya 11:000 asubuhi ilifanywa na baadhi ya wasimamizi                wa vituo na watu wasiojulikana katika cha kugawa vifaa                eneo TANROAD Temboni.
        
0 comments:
Post a Comment