Marekani imeiondoa Burundi kutoka kwenye mikataba yake            ya kibiashara AGOA iliyowezesha mataifa ya Afrika kuingiza            bidhaa zao katika soko la Marekani bila kulipa kodi.
        Katika barua aliyoiandikia bunge la Congress , rais            Barrack Obama ameelezea kuwa amechukua hatua hiyo baada ya            kushuhudia kushuka kwa viwango vya demokrasia katika taifa            hilo la Afrika ya Kati.
        ''Burundi haijafanya jitihada zozote za kurejesha            amani na utangamano'' Obama.
        Obama alisema kuwa badala ya kuimarika kidemokrasia,            Burundi inaendelea kushuhudia wapiganiaji wa haki za            kidemokrasia wakikamatwa na kufungwa jela huku wengine wengi            wakiuawa kwa kudai haki zao za kikatiba zifwatwe.
        Aidha Obama ameelezea kuwa hatua ya serikali ya rais            Nkurunziza ya kuwanyamazisha makundi ya wapinzani kwa            kuwashika kuwaua na hata kuwatesa ni kinyume na maadili ya            taifa linalodai kuzingatia demokrasia.
        Marufuku hiyo ya Burundi inaanza kutekelezwa mwezi            januari mwakani.
        Burundi ilitumbukia katika mzozo wa kisiasa na            kukumbwa na machafuko punde baada ya rais Pierre Nkurunziza            kutangaza nia ya kuwania muhula wa tatu kinyume na katiba ya            taifa.
        Aidha kulitokea jaribio la mapinduzi lakini likazimwa.
        Nkurunziza alishiriki uchaguzi huo na akashinda, hata            hivyo kumeendelea kuwa na visa vya maandamano,mauaji na            kutoweka kwa wapinzani wake.
        Takriban watu 200 wameuaawa tangu machafuko yaanze            mwezi Aprili
        Inakisiwa kuwa watu 200,000 wametoroka makwao na sasa            wanaishi kwenye kambi za wakimbizi katika mataifa jirani.
        Mpango wa AGOA (African Growth and Opportunity Act)            ulianzishwa yapata muongo mmoja uliopita ilikuzisaidia mataifa            maskini ya Afrika kuuza bidhaa zao katika soko la Marekani.
        
0 comments:
Post a Comment