Habari zilizosambaa mitandaoni kuhusiana na                mabunda ya noti za dola ya Kimarekani kuwa zimekutwa                nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa wa mtandao wa wizi                bandarini na TRA sio za kweli, Globu ya Jamii inaweza                kuthibitisha.
        Ukweli ni kwamba mabunda hayo ya noti yalikamatwa                huko jijini York, Portland, Marekani Mwezi Septemba mwaka                2010, na sio hapa Dar es salaam, Tanzania kama ambavyo                wadau wengi wa mitandao hasa ya Whatsapp na Instagram                wanavyovumisha.
        Tumelazimika kutoa habari hii ili kuokoa wadau                wetu wengi katika vuguvugu hili la uvumi wa mitandaoni                ambayo hupelekea kazi kuwa ngumu kwa wengi wetu                tunaotafuta na kutoa taarifa za uhakika na ukweli. Maana                samaki mmoja akioza wote huonekana wameoza.
        Vile vile hii ni kuwafumbua wale wote wanaohusika                kusimamia na kutekeleza sheria ya mitandao wawe macho na                kuanza kuchukua hatua madhubuti ili kupunguza kama si                kuondoa kabisa tabia hii mbaya ya kusema uwongo kila                kukicha.
        
0 comments:
Post a Comment