November 14, 2015

  • WATANZANIA WENGI HAWAWEKI AKIBA - SABASABA MOSHINGI



    WATANZANIA WENGI HAWAWEKI AKIBA - SABASABA MOSHINGI
     Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba, Kenya, Bi.Anne Karanja, (Katikati), na Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Posta Uganda, Bw. Stephene Mukweli, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa mkutano wan ne wa Bodi ya Wadhamini, ya Umoja wa Mabenki ya Afrika Mashariki, ASBEA, uliomalizika Novemba 13, 2015 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 
    (Habari picha na K-Vis Media/Khalfan Said)
    AFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Bw. Sabasaba Moshingi, amewahimiza wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kwenye akaunti zao.
    Bw. Moshingi aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kutano wanne wa bodi ya wadhamini ya Umoja wa Mabenki ya Akiba wa Nchi za Afrika Mashariki, (ASBEA), uliomalizika Novemba 13, 2015 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
    "Lengo la Umoja huu ni kuhamasishawananchi wan chi wanachama wa ASBEA, kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba kama njia ya msingi ya kutokomeza umasikini, kimarisha uchumi na kujenga uwekezaji wenye faida katika uchumi wa mataifa yetu." Alisema.
    Afisa Mtendaji huyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano huo uliohudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba ya Kenya, (KPOSB), Anne Karanja, na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta nchini Uganda, Stephene Mukweli, pamoja na wajumbe wengine, alisema Nchi za Afrika Mashariki bado zipo nyuma kwenye suala zima la uwekaji akiba na kutolea mfano Tanzania, ambapo alibainisha.

    "Takriban asilimia 14 tu ya wananchi wa Tanzania ndiowanaojiwekea akiba kwenye akaunti zao, kiasi hiki ni kidogo sana ukilinganisha na asilimia 23 ambayo ndio wastani wan chi zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara." Alisema Bw. Moshingi.
    Umoja huo wa ASBEA ulioanzanishwa mnamo mwaka 2001, unakusudia kupanua wigo wa wanachama wake ambapo uko kwenye majadiliano ili kuzishawishi nchi za Rwanda, Burundi na Sudani Kusini kujiunga na umoja huo.
    Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta ya Akiba ya Kenya,Anne Karanja alisemaukuaji wa teknolojia umeleta changamoto kubwa katika sekta ya kibenki barani Afrika na hivyo ni wajibu wa wa ASBEA kuangalia namna bora ya kuitumia teknolojia hiyo katika kuzipeleka huduma za kibenki karibu zaidi na wananchi ili kukuza uchumi wao na nchi wanachama kwa ujumla.
    Jumuiyaya ASBEA ina jumla ya wateja milioni 3, wanaoweka takriban akiba ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 314 katika amana, wakijivunia utoaji huduma kupitia mawakala, magari ya kutolea huduma, matawi ya Benki na ATMs.
     Wajumbe wakimsikiliza mtoa mada, Mkurugeni Mtendaji wa Benki ya Posta Kenya, Bi.Anne Karanja
     Bi. Anne Karanja
     Bw. Stephene Mukweli
     Bw. Sabasaba Moshingi
     Mjumbe akizungumza
     Wajumbe wakisikiliza kwa makini
     Mjumbe kutoka Tanzania kifuatilia kwa umakini mkutano huo
     Afisa wa Benki ya Posta Tanzania, akifuatilia mad zilizokuwa zikitolewa




     Wajumbe wa bodi ya ASBEA, wakiongozwa na Bw. Moshingi, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya mwenendo wa mkutano wao na malengo yake





  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.