November 04, 2015

  • Breaking News: Karim Benzema akamatwa na hii ndio kesi inayomkabili


    Breaking News: Karim Benzema akamatwa na hii ndio kesi inayomkabili

    Mshambuliaji wa Real Madrid na Ufaransa Karim Benzema amekamatwa na polisi leo hii huko nchini Hispania – shirika la habari la AFP linaripoti.

      AFP wanaripoti kwamba mshambuliaji huyo amekatwa na polisi kwa kuhusishwa na kesi ya kutaka kupata kipato isivyo halali ili kuficha siri ya mkanda wa ngono wa Mathieu Valbuena.
     Mchezaji wa zamani wa Ufaransa na Liverpool Djibril Cisse hivi karibuni alikamatwa na polisi nchini Ufaransa kwa makosa hayo hayo yanayofanana na Benzema.

    Cisse aliachiwa na polisi tarehe 13 kufuatiwa kukamatwa nyumbani kwake saa 12 asubuhi jijini Paris.

    Leo hii sasa shirika la habari la Ufaransa AFP wameripoti Benzema amekamatwa na polisi kwa kesi hiyo hiyo ya Blackmail.

    AFP wameripoti kwamba Benzema alienda polisi leo asubuhi saa 3, kabla ya kuwekwa kizuizini.
    Endapo atakutwa na hatia basi mchezaji huyo atafunguliwa kesi inayoweza kumuweka ndani kwa miaka 5



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.