Katibu Mkuu Kiongozi              Balozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na              uchapishaji wa kadi za Christmas na Mwaka Mpya kwa gharama              za serikali/umma, kwa mwaka huu.
        Balozi Sefue,              ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha              kadi hizo, afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe.
          
        Badala yake Balozi              Sefue ameagiza fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na              uchapishaji wa kadi, zitumike kupunguza madeni ambayo              Wizara, Idara na Taasisi za umma zinadaiwa na              wananch/wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe              katika matumizi mengine ya kipaumbele.
        Gerson Msigwa
        Kaimu Mkurugenzi wa              Mawasiliano, IKULU
        26 Novemba, 2015
        
0 comments:
Post a Comment