Jaji Kiongozi, Shaban Lila                      alisema jana kuwa tayari wadau mbalimbali wa haki                      jinai wameanza kukutana kuangalia namna ya kuanzisha                      mahakama hiyo kama sehemu ya utekejezaji wa ahadi ya                      Rais.
              Akizungumza katika hafla                      ya kuhitimisha mafunzo ya kushughulikia mashauri                      nyeti ya jinai kwa majaji 12 wa Mahakama Kuu ya                      Tanzania, alisema juzi walikuwa na mazungumzo na                      Wizara ya Katiba na Sheria kuangalia mfumo wa                      uendeshaji wa mahakama hiyo.
              "Tunaangalia tuianzishe                      kama mahakama huru au ifanywe ndani ya muundo wetu                      wa mahakama kwa kuipa kipaumbele maalumu. Lakini                      tunafikiria zaidi kama ingekuwa ni kitengo maalumu                      ndani ya Mahakama Kuu kitakachokuwa kikishughulikia                      mafisadi," alisema Jaji Lila.
              Hata hivyo, Jaji Lila                      hakutaja muda maalumu utakaotumika kumaliza mchakato                      wa kuanzisha mahakama hiyo, huku akisema unahusisha                      wadau wengi na unyeti wake unahitaji maandalizi                      makubwa.
              Jaji huyo bila kutaja                      takwimu, alieleza kuwa kesi za makosa makubwa ya                      jinai zinaongezeka nchini ukilinganisha na miaka ya                      nyuma hasa zile zinazohusu utakatishaji fedha,                      ugaidi, usafirishaji wa dawa za kulevya,                      usafirishaji wa nyara za Serikali hasa wanyama hai                      na mazao yake na ufisadi.
              Balozi wa Uingereza                      nchini, Dianna Melrose alimpongeza Rais Magufuli kwa                      kuonyesha msimamo wa kupambana na makosa ya jinai                      yakiwamo ya dawa ya kulevya, usafirishaji wa nyara                      za Serikali na utakatishaji fedha.
              "Nilikuwa nimeketi bungeni                      namsikiliza Rais siku alipokuwa akilihutubia Bunge,                      japo hotuba yake ilikuwa kwa Kiswahili lakini                      nilipata faraja kubwa nilipomuona akiwa mkali katika                      masuala hayo," alisema Balozi Melrose.     
            
0 comments:
Post a Comment