Bomoabomoa ya nyumba na makazi zilizojengwa kinyume cha sheria iliendelea jana katika Wilaya ya Kinondoni, ambapo Kanisa la Anglikana pamoja na Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Mivumoni zimekumbwa na bomoabomoa hiyo.
Shughuli                hiyo ya ubomoaji ilianza jana saa 12 asubuhi katika eneo                la Mbezi Jogoo, ambapo nyumba 25, makanisa mawili, fremu                mbili za biashara na sehemu ya kuoshea magari                zilibomolewa.
                Mbali                na kanisa la Aglikana,  kanisa jingine ni la Tanzania                Assemblies of God (TAG) lililopo Bunju B, nyumba ya                mwanajeshi ambaye amerejea kutoka  kulinda amani Darfur                Sudan nayo imebomolewa na kusababisha mke wa mwanajeshi                huyo kuzirai.
                Mbezi                  Jogoo
                Bomoabomoa                ilifanyika karibu na kiwanda cha Interchick ambapo nyumba                moja na eneo la kuoshea magari vilibomolewa.
                
                Aidha                bomoabomoa iliendelea eneo la Basihaya Bunju ambapo                 nyumba 19 zilibomolewa pamoja na fremu mbili za biashara                ya mbao inayomilikiwa na Ally Khamis.
                
                Mwenyekiti                wa Mtaa wa Basihaya, Kata ya Bunju, Malinus Ndule alisema                nyumba hizo tayari wananchi wake walilipwa fidia ikiwemo                viwanja katika eneo la Mabwepande.
                Waumini                  waangua vilio
                Waumini                wa Kanisa la Tanzania Assemmbles of God (TAG) walifika                eneo la tukio wakiwa na Biblia wakiomba na kuangua kilio                huku wakisema Mungu ana mpango nao.
                Akizungumzia                tathimini ya ubomoaji huo, Mhandisi wa Manispaa ya                Kinondoni, Baraka Mkuya alisema shughuli hiyo inaendelea                vyema na ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa                kuwafichua vigogo waliojenga kinyume na sheria.
         
0 comments:
Post a Comment