Mwanamke mmoja ambaye              babu yake alichukua ukanda wa video wa mauaji ya rais John F              Kennedy kama filamu ya nyumbani ameishtaki serikali ya              Marekani kwa mapato yake.
          Gayle Nix Jackson pia              anataka kulipwa fidia ya dola milioni 10 za filamu hiyo              iliochukuliwa na Orville Nix mnamo mwezi Novemba mwaka 1963.
          Aliiuza filamu hiyo              kwa shirika moja la habari mwaka huo lakini baadaye ilipewa              serikali ili uchunguzi ufanywe.
          Bi Nix Jackson              anasema kuwa aliambiwa mwaka huu kwamba shirika hilo la              habari la serikali linalodaiwa kumiliki kanda hiyo halina.
          Kanda hiyo              ilichukuliwa na filamu ya Nix mkabala na upande ambapo gari              la rais aina ya Limousine lilikuwa, kutoka mahala ambapo              filamu maarufu ya Zapruder ilichukuliwa tarehe 22 mwezi              Novemba 1963.
          Filamu hiyo ya Nix              inaonyesha risasi ikimpiga rais,mkewe rais Jackie Kennedy              akipanda juu ya gari hilo na jasusi Clint Hill akiruka na              kuingia ndani ya gari hilo.
          Orville Nix aliiuza              filamu yake kwa UPI kwa dola 5,000 kukiwa na makubaliano ya              malipo mengine baada ya miaka 25.
          Lakini baadaye              ilipewa serikali ili uchunguzi ufanywe.
          Ilionekana mara ya              mwisho na kamati ya bunge iliokuwa ikichunguza mauaji hayo              mwaka 1978.
        
0 comments:
Post a Comment