Tunakujali, Tunakuthamini na Pia Tunakupenda!

November 29, 2015

  • NEWS ALERT: TAARIFA SAHIHI YA MABUNDA YA NOTI KWENYE NDOO INAYOZAGAA MITANDANO HII HAPA....


    NEWS ALERT: TAARIFA SAHIHI YA MABUNDA YA NOTI KWENYE NDOO INAYOZAGAA MITANDANO HII HAPA....
    Habari zilizosambaa mitandaoni kuhusiana na mabunda ya noti za dola ya Kimarekani kuwa zimekutwa nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa wa mtandao wa wizi bandarini na TRA sio za kweli, Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha.
    Ukweli ni kwamba mabunda hayo ya noti yalikamatwa huko jijini York, Portland, Marekani Mwezi Septemba mwaka 2010, na sio hapa Dar es salaam, Tanzania kama ambavyo wadau wengi wa mitandao hasa ya Whatsapp na Instagram wanavyovumisha.
    Tumelazimika kutoa habari hii ili kuokoa wadau wetu wengi katika vuguvugu hili la uvumi wa mitandaoni ambayo hupelekea kazi kuwa ngumu kwa wengi wetu tunaotafuta na kutoa taarifa za uhakika na ukweli. Maana samaki mmoja akioza wote huonekana wameoza.
    Vile vile hii ni kuwafumbua wale wote wanaohusika kusimamia na kutekeleza sheria ya mitandao wawe macho na kuanza kuchukua hatua madhubuti ili kupunguza kama si kuondoa kabisa tabia hii mbaya ya kusema uwongo kila kukicha.





  • SAKATA LA MAKOTENA KUPOTEA BANDARINI HII HAPA BARUA KUTOKA TRA KWENDA BAKHRESA


    SAKATA LA MAKOTENA KUPOTEA BANDARINI HII HAPA BARUA KUTOKA TRA KWENDA BAKHRESA


  • MBARONI KWA KUUA WATU WATATU WA FAMILIA MOJA



    MBARONI KWA KUUA WATU WATATU WA FAMILIA MOJA
    Polisi mkoani Ruvuma inamshikilia Amani Hyera (42), mkazi wa kijiji cha Kikunja wilayani Songea kwa tuhuma za kuwaua watu watatu.



    Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela, alisema tukio hilo limetokea juzi.

    Alisema siku ya tukio Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Songea akiwa ofisini kwake, alipokea taarifa ya mauaji ya watu watatu.

    Alisema anayedaiwa kufanya mauaji hayo ni Hyera, mkazi wa kijiji cha Kikunja.

    Alisema mtu huyo anadaiwa kuwaua watoto wawili na mama yao kwa kuwakatakata mapanga kwa kile kilichosadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

    Alisema baada ya kufanya mauaji hayo,  alijaribu kujiua kwa kujikata na panga shingoni, lakini hakufanikiwa kutokana na wananchi kufika kwenye eneo hilo la tukio na kumdhibiti.

    Kamanda Msikhela alisema mtuhumiwa  anaendelea kupata matibabu na taratibu za kisheria zinafuata mara tu baada ya afya yake kuimarika.

    Aliwataja waliouawa katika tukio hilo kuwa ni Ester Kadege (48), ambaye ni mama mzazi wa watoto waliouawa, Edson Msuha (6) na Kazed Kadege (13).

    Alisema marehemu Ester alikuwa na watoto wawili ambao walizaliwa kwa baba tofauti ambapo uchunguzi wa awali wa polisi umebaini kuwa mtuhumiwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ester na baadaye waliachana kufuatia Ester kudai kuwa ameokoka na kwamba hataki tena masuala ya kimapenzi.



  • MAGUFULI AWAWEKA ROHO JUU VIGOGO WA MASHIRIKA YA UMMA




    MAGUFULI AWAWEKA ROHO JUU VIGOGO WA MASHIRIKA YA UMMA  Rais John Magufuli akisalimiana          na Waziri

    Siku moja baada ya Rais John Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa kuwasimamisha watendaji wa Bandari na TRA, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amemtaka kila mtendaji mkuu au ofisa masuhuli wa Serikali kujiuliza ni kwa kiasi gani anatekeleza kwa vitendo dhamira ya Rais ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.



    Alitoa kauli hiyo jana katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, ikifafanua maagizo ya Rais kuhusu kupunguza matumizi yasiyo ya lazima katika wizara, idara na taasisi za Serikali.
    Juzi, Majaliwa alifanya ziara ya ghafla katika ofisi za Bandari na kuwasimamisha watumishi hao akiwamo Kamishna wa Kodi na Forodha wa TRA, Tiagi Masamaki na Habibu Mponezya wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja ambao wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha uliotokana na upotevu wa makontena zaidi ya 349.
    Baadaye, Rais Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade baada ya kubaini 'madudu' katika ofisi za mamlaka hiyo ikiwa ni mwendelezo wa kasi aliyoanza nayo katika ukaguzi na udhibiti wa matumizi ya fedha za umma.
    "Rais ameonyesha njia, sasa kwa wakati huu ni vyema kila mtendaji mkuu wa Serikali, ajiulize endapo Rais Magufuli atafika katika eneo langu la kazi, ni kwa kiasi gani atakuta nimetekeleza maagizo yake?" alisema Balozi Sefue.
    Balozi Sefue pia alizungumzia uchapishaji wa kalenda na vitabu vya kumbukumbu huku akihoji umuhimu wa wake.
    "Kila mtendaji mkuu wa Serikali au afisa masuhuli apime mwenyewe kama ni lazima kutengeneza na kuchapisha kalenga na diary na kama ni lazima achapishe kwa kiasi gani?
    "Ni matumizi mabaya ya fedha za umma kwa kila wizara, idara na taasisi za Serikali kuchapisha idadi kubwa ya kalenda na diaries ambazo wakati mwingine hata hazitumiki mpaka mwaka unakwisha," aliongeza Balozi Sefue.
    Kwa hatua zinazochukuliwa ni dhahiri watendaji wakuu wa mashirika, taasisi za umma na wizara mbalimbali watakuwa matumbo joto kwa kuwa hawajui ni lini viongozi hao watatua kwao.
    Hayo yanatokea wakati ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyotolewa mapema mwaka huu inaonyesha ukaguzi uliofanywa katika taasisi 176 za Serikali Kuu, halmashauri 163 na mashirika ya umma 109 ulibaini ufisadi katika mishahara hewa na katika miradi ya maendeleo.
    Mashirika ya umma yanayotazamwa ni Shirika la Nyumba (NHC), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Shirika la Maendeleo ya Mafuta (TPDC), Kampuni la Reli Tanzania (TRL), Shirika la Reli Tanzania na Zambia (Tazara), Tanesco, mifuko ya hifadhi ya jamii; NSSF, PPF, LAPF, PSPF, GEPF, NHIF na mashirika ya hifadhi za taifa kama Tanapa na Ngorongoro pamoja na mamlaka za udhibiti kama Ewura, Sumatra, TCRA, TCAA na SSRA.
    Kutokana na hatua hizo za Rais Magufuli na Majaliwa, Waziri Mkuu wa zamani, Dk Salim Ahmed Salim alisema kasi hiyo inawathibitishia Watanzania kuwa alichokuwa akikisema Dk Magufuli na kukiahidi kipindi cha kampeni ni cha kweli.
    Alisema hayo wakati akizungumza na mwandishi wetu baada ya kufungua mahafali ya 13 ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), yaliyofanyika, Dar es Salaam jana.
    "Watumishi wa Serikali hivi sasa wajizatiti kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ili waendane na kasi hii ya Dk Magufuli.
    "Nina imani hata hawa wauguzi na madaktari waliohitimu leo (jana), ambao wamepikwa na kuiva, wataweza kuendana na kasi hii," alisema Dk Salim ambaye pia ni mkuu wa chuo hicho.

    Watendaji wazungumza
    Baadhi ya watendaji wa mashirika ya umma waliozungumza jana kwa nyakati tofauti walisema wako tayari kwenda sambamba na kasi ya Rais Magufuli huku wengine wakiahidi kuzungumzia hilo siku tano zijazo.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema Tanesco imejiandaa kufanya kazi na Magufuli kwa kasi aliyoanza nayo.
    Alipoulizwa atawezaje kwenda sambamba na kasi ya Rais Magufuli katikati ya shirika linalokabiliwa na changamoto nyingi, Mramba alisita kutoa ufafanuzi wa swali hilo kuahidi kulitolea majibu hivi karibuni.
    Shirika hilo la umeme limekuwa likikabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya usambazaji wa umeme, mikataba mibovu kwa kampuni zinazouza umeme, kushindwa kukusanya fedha za mauzo ya umeme na uhujumu na mitandao ya wizi wa umeme.
    Alipoulizwa, Msemaji wa Tazara, Conrad Simuchile alitaka atumiwe maswali kwa mtandao ili aweze kujibu kesho kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji, Ronald Phiri.
    Januari mwaka huu, Phiri aliliambia gazeti hili kuwa mamlaka hiyo inaweza kufa endapo nchi washirika hazitawekeza mtaji mkubwa ili kuongeza uzalishaji.Tazara imekuwa na migogoro ya muda mrefu na wafanyakazi wake katika malipo ya mishahara lakini uongozi wake unadai hali hiyo inachagizwa na kushuka kwa uzalishaji. Kuhusu mpango wa kwenda na kasi ya Rais Magufuli ndani ya TRL, Mkuu wa Masoko, Charles Ndenge alisema atatoa ufafanuzi kesho ofisini kwake.
    Mei mwaka huu, aliyekuwa Waziri wa uchukuzi, Samuel Sitta aliwasimamisha kazi vigogo watano akiwamo Mkurugenzi Mtendaji TRL, Kipallo Kisamfu na watumishi wengine wanne baada ya kupitia uchunguzi wa tuhuma zilizowakabili.
    Watendaji hao walisimamishwa kazi kutokana na tuhuma za kuhujumu mamlaka hiyo kupitia ununuzi wa mabehewa mabovu 274 ya mizigo, uliofanyika chini ya mkataba kati ya TRL na Kampuni ya M/S Hindusthan, hatua iliyosababisha hasara ya Sh230 bilioni.
    MWANANCHI.


  • MKOA WA DODOMA UMEANZA KUTEKELEZA AGIZO LA MHE. RAIS MAGUFULI LA KUFANYA USAFI SIKU YA UHURU 9 DISEMBA, 2015



    MKOA WA DODOMA UMEANZA KUTEKELEZA AGIZO LA MHE. RAIS MAGUFULI LA KUFANYA USAFI SIKU YA UHURU 9 DISEMBA, 2015
    Mkoa wa Dodoma umeanza rasmi kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli lililotaka kufanyika kwa usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya nchi siku ya tarehe 9 Disemba, 2015 kama mojawapo ya maadhimisho ya siku ya uhuru na kuwataka viongozi na wataalamu kusimamia utekelezaji wa agizo hilo. 
     Uongozi wa Mkoa umeamua kuanza mapema zoezi la ufanyaji usafi pasipo kusubiri tarehe 9 Disemba na umepanga kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu likihusisha usafi wa kila siku na usafi wa siku zote za Jumamosi kuanzia saa 1:00 hadi saa 3:00 asubuhi. 
    Taasisi mbalimbali zilizopo Mkoani Dodoma zimetumia Jumamosi ya jana Novemba 28, 2015 kushirikiana na wananchi kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma ambapo Viongozi na Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Ofisi ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wamefanya usafi eneo la Bahi Road kuelekea Nkuhungu kwa kuondoa taka na michanga kwenye mitaro ya maji ya mvua, kufyeka na kuchoma taka eneo la makaburi ya Kizota. 
     Kwa mujibu wa Ratiba ya usafi iliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira mjini Dodoma-DUWASA ilifanya usafi eneo la kuanzia ofisi za waziri mkuu (Mtaa wa Mahakamani) hadi ofisi za hazina ndogo. 
    TANESCO Mkoa wa Dodoma walisafisha eneo la kituo cha kuuzia mafuta cha BP Capital hadi soko la Sabasaba. Taasisi nyingine ni pamoja na jeshi la Magereza ambapo lilifanya usafi kuanzia mzunguko wa barabara ya kuelekea Bahi hadi maeneo ya magorofa mengi wakati mabenki yalisafisha mitaa na barabara zinazopita mbele ya majengo yao ya benki na Wakala wa Barabara TANROADS wao walisafisha kuanzia kituo cha mabasi ya mikoani hadi soko la Sarafina. 
    Kwa upande wa wananchi walioshiriki zoezi hilo la kufanya usafi, wamepongeza utaratibu na kusema utasaidia kuweka mji katika mazingira safi. 
    Akiwawakilisha wananchi walioshiriki zoezi hilo, Mkazi wa Dodoma Onesmo Stephano alielezea kuwa utaratibu huo wa viongozi wa Mkoa na watumishi wa serikali kushiriki kufanya usafi unawatia hamasa kubwa wananchi nao kushiriki pale wanapoona viongozi wao wanashiriki kufanya nao usafi. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa alibainisha kuwa siku ya tarehe 9 Disemba itakuwa siku ya kutathimini kazi ya usafi inayoendelea kufanyika ndani ya Mkoa, pia utafanyika usafi kwenye maeneo ya huduma za jamii kama masoko na Hospitalini. 
     Maagizo yaliyotolewa wakati wa kupanga mikakati ya utekelezaji wa agizo la kufanya usafi kwenye Mkoa wa Dodoma ni pamoja na mamlaka za serikali za mitaa katika ukaguzi na usimamizi wa zoezi la usafi kwenye maeneo ya makazi na shughuli mbalimbali wafanye ukaguzi wa vyoo. Vilevile ukaguzi kwa kazi iliyofanyika ya usafi wa mazingira ya makazi, maeneo ya huduma za jamii, maeneo ya utupaji taka. 
    Maelekezo mengine ni pamoja na matumizi ya sheria ndogo kama kutoa ILANI, Makatazo na adhabu za Faini kwa makosa ya uchafuzi wa mazingira. Uongozi wa Mkoa wa Dodoma umeelezea kuwa zoezi hili la kufanya usafi wa mazingira kila siku na usafi wa pamoja wa kila siku za jumamosi utasaidia kupunguza magonjwa mengi yatokanayo na uchafu wa mazingira kama vile kipindupindu, kuhara na magonjwa mengine ya milipuko na kwa sasa wanasubiri Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kutoa ratiba ya zoezi la usafi la Jumamosi 
     Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge (kulia walioingia mtaroni) na watumishi wengine wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Roadmapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
     Wafanyakazi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
     Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakijiorodhesha baada ya kumaliza zoezi la usafi wa mazingira mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira, orodha hiyo itatumika kuwabaini watumishi ambao hawajashiriki zoezi la usafi.

     Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Dodoma Bazil Mwiserya akishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.

    Watumishi wa Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kufanya usafi kwa kufyeka magugu eneo la makaburi ya Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.
     Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge akiongoza  kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road 
    Wafanyakazi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Manispaa ya Dodoma wakishiriki zoezi la kusafisha mitaro ya maji ya mvua eneo la Bahi Road mapema leo ikiwa ni mwanzo wa utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kutumia siku ya uhuru 9 Disemba kufanya usafi wa mazingira.


  • Putin orders several sanctions against Turkey



    Putin orders several sanctions against Turkey
    Russian President Vladimir Putin issued a decree for sanctions against Turkey on Saturday, days after a Russian warplane was shot down in Turkey. Turkish Presdient Tayyip Erdogan expressed regret over the warplane incident earlier on Saturday, saying:
    "We are truly saddened by this incident," Erdogan said. "We wish it hadn't happened as such, but unfortunately such a thing has happened. I hope that something like this doesn't occur again."
    However, Putin wasn't moved by Erdogan's regret, instead he put an end to chartered flights from Russia to Turkey, a ban on some goods and bars extensions of labor contracts for Turks working in Russia,he didn't specify what goods are to be banned or give other details and a ban on Russian tourist companies' vacation packages that include a stay in Turkey.
     
    Putin's decree also calls for ending visa-free travel between Russia and Turkey and orders the tightening of control over Turkish air carriers in Russia "for security reasons." The decree was issued "to protect Russian citizens from crimes," a Kremlin statement said.
     
    Putin calls what Turkey did as a stab in the back.

    Meanwhile, addressing supporters in the western city of Balikesir, Erdogan said neither country should allow the incident to escalate and take a destructive form that would lead to "saddening consequences."
    He renewed a call for a meeting with Putin on the sidelines of a climate conference in Paris next week, saying it would be an opportunity to overcome tensions.
    Erdogan's friendly overture however, came after he again vigorously defended Turkey's action and criticized Russia for its operations in Syria.
    "If we allow our sovereign rights to be violated ... then the territory would no longer be our territory," Erdogan said.
    On Saturday Turkey issued a travel warning urging its nationals to delay non-urgent and unnecessary travel to Russia, saying Turkish travelers were facing "problems" in the country. It said Turks should delay travel plans until "the situation becomes clear."

  • November 28, 2015

  • BALOZI ZATAKIWA KUJIPANGA KUIWAKILISHA TANZANIA



    BALOZI ZATAKIWA KUJIPANGA KUIWAKILISHA TANZANIA

    Kufuatia agizo la Rais John Magufuli alilotoa hivi karibuni la kusitisha safari za nje kwa wizara, idara na taasisi za serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imeanza kutekeleza kwa kutoa maelekezo kwa Balozi zake za nje.



     
    Wizara hiyo imezielekeza Balozi zote zilizopo maeneo mbalimbali duniani kujipanga ili kushiriki kikamilifu katika kuiwakilisha serikali kwenye mikutano yote ya kimataifa na kikanda inayofanyika katika maeneo yao ya uwakilishi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam na wizara hiyo, imeeleza
    Tanzania ina Balozi 35 zikiwamo bazozi ndogo tatu, vituo viwili vya biashara na konseli za heshima 17 katika nchi mbalimbali.
     
    "Hizi zote zitahusika katika kuendeleza utekelezaji wa diplomasia yetu ya uchumi na uwakilishi wa maslahi ya nchi yetu," ilieleza taarifa hiyo.
    Hadi sasa mikutano ambayo tayari imefanyika na Balozi zetu kuwakilisha ni pamoja na Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) unaoendelea nchini Malta na Mkutano wa Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Habari wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika nchini Lesotho.
     
    Aidha, imetoa wito kwa wizara, idara na taasisi za serikali kuwasilisha mapema taarifa za mikutano inayohusu sekta zao ili kutoa fursa ya kuzianyia kazi kwa wakati na kuhakikisha ushiriki wa Tanzania unakuwa wenye tija kwa taifa.
     
     Ilieleza kuwa wizara inaungana na wadau wengine kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua anazozichukua za kuleta ufanisi mkubwa wakazi na kubana matumizi ili kuiwezesha serikali kuwahudumia wananchi.
    CHANZO: NIPASHE


  • UTURUKI YAMUONYA PUTIN KUTO CHEZA NA MOTO




    Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemuonya mwenzake wa Urusi Vladimir Putin 'kutocheza na moto' kuhusu swala la taifa lake kuidungua ndege ya kijeshi ya Urusi
    .
    Bwana Erdogan pia amesema kuwa anataka kukutana na bwana Putin ana kwa ana katika mazungumzo ya mabadiliko ya hali ya hewa ili kusuluhisha mzozo huo.
    Bwana Putin anataka kuombwa msamaha na Uturuki kabla ya kuzungumza na Erdogan ,msaidizi wa rais huyo amesema.


    Urusi imeamua kusitisha mpango wa kusafiri bila viza miongoni mwa raia wa mataifa hayo mawili kwa mujibu wa waziri wa maswala ya kigeni nchini humo.
    Uturuki inasema kuwa ndege hiyo ilikuwa katika anga yake ilipolengwa,lakini Urusi inasema kuwa ilikuwa katika anga ya Syria.
    ''Ningependa kukutana na bwana Putin ana kwa ana mjini Paris'',alisema bwana Erdogan katika hotuba yake katika runinga.
    ''Ningependa kusuluhisha tatizo hili.Inaudhi kuona kwamba swala hili limeongezewa chumvi''.


    Lakini pia amesema kuwa Uturuki haitaki kuharibu uhusiano wake na Urusi.
    Waziri wa maswala ya kigeni nchini Urusi Sergei Lavrov ameonya kuwa kisa hicho kinaweza kuathiri maslahi ya Uturuki.



  • RAIS DK.SHEIN ATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI MAHONDA LEO



    RAIS DK.SHEIN ATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI MAHONDA LEO
     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda  kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India
     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akionesha kitu wakati alipotembelea kiwanda cha Sukari cha Mahonda Wilaya ya Kaskazini B. Unguja leo ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,akiwa katika ziara aliyofuatana na Viongozi mbali mbali wa Serikali
     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo wakati alipofuatana Meneja wa  Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda Bw.Rajesh Kumar (wa pili kulia) kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati naKampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,(kulia ni ) Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiangalia hatua ya ujenzi na kupata maelezo katika  Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda  kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo wakati alipofuatana Meneja wa  Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda Bw.Rajesh Kumar (katikati) alipotembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja,(kulia) Meneja mradi Tushar Mehta.
    Picha na IKULU, Zanzibar


  • KOMBE AMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KWA KUWAPATIA JAMBO LEO FAGIO ZA USAFI SIKUKUU YA UHURU



    KOMBE AMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KWA KUWAPATIA JAMBO LEO FAGIO ZA USAFI SIKUKUU YA UHURU
     Waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo, wakifurahia kupata fagio walizokabidhiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Zahanati ya Mji Mwema Kigamboni, Dar es Salaam, Omary Kombe (kulia), katika hafla iliyofanyika katika chumba cha habari cha gazeti hilo, Dar es Salaam. 
    Kombe ametoa msaada huo kuunga mkono maelekezo ya Rais Dk. John Magufuli ya kufuta sherehe za Sikukuu ya Uhuru ili wananchi washiriki siku hiyo kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu nchini. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)



  • BREAKING NEWS : Kigogo CCM kortini kwa kulawiti wanawe ... Mmoja ana mwaka mmoja, mwingine miaka mitano.



    BREAKING NEWS : Kigogo CCM kortini kwa kulawiti wanawe ... Mmoja ana mwaka mmoja, mwingine miaka mitano.
     Katibu Msaidizi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Rogers Msangi (44), amepandishwa kizimbani mjini Moshi akituhumiwa kuwalawiti watoto wake wawili.

    Msangi, ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Mwanga, alipandishwa kizimbani jana mbele ya Hakimu Mkazi, Anthony Ngowi. Msangi alikanusha tuhuma dhidi yake na alipelekwa rumande katika Gereza Kuu la Karanga, Moshi baada ya wadhamini wake wawili kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

    Makosa anayodaiwa kutenda kigogo huyo yanaangukia katika shtaka la kumwingilia binadamu kinyume cha maumbile kinyume cha kifungu 154 cha Kanuni ya Adhabu. Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Novemba 16 mwaka huu, katika eneo la Mwangodi wilayani Mwanga, mshtakiwa alimlawiti mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi mitatu.

    Katika shtaka la pili, Wakili wa Serikali, Ignas Mwinuka alidai kati ya Oktoba na Novemba mwaka huu katika eneo hilo, mshtakiwa alimlawiti mtoto wake mwingine mwenye umri wa miaka mitano.

    Mshtakiwa huyo anayetetewa na Wakili Ralph Njau alikanusha mashtaka hayo. Hakimu Ngowi alimweleza mshtakiwa kuwa dhamana yake iko wazi kwa masharti kwamba asaini hati ya dhamana ya Sh6 milioni na awe na wadhamini wawili wa kuaminika ambao ni watumishi wa umma na wenye vitambulisho halali.

    Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na hivyo alipelekwa rumande hadi Desemba 7 kesi hiyo itakapotajwa.


  • BREKING NEWS: KASHFA YA BANDARI WATUMISHI WENGINE WASIMAMISHWA KAZI LEO







  • November 27, 2015

  • SERA YA ELIMU BURE INAKARIBIA KUKAMILIKA KUANZA KUTUMIKA JANUARI MWAKANI



    SERA YA ELIMU BURE INAKARIBIA KUKAMILIKA KUANZA KUTUMIKA JANUARI MWAKANI

    Serikali imesema siku za karibuni watatoa muongozo utakaoonyesha jinsi sera mpya ya elimu bure itakavyotekelezwa kuanzia mwezi Januari.




    Hii imejulikana baada ya mkutano kati ya Kati Mku wa Wizara ya Elimu, Profesa Sifumi Mchome na wakurugenzi wa Idara tofauti zilizo chini ya wizara hiyo, walijadili kwa kina utekelezaji wa sera kutokana na mikakati iliyowekwa na Serikali ya awamu ya tano.



    Katibu wa Wizara ya elimu amesema kuwa mfumo huu mpya utawaletea ahueni wazazi nchi nzima, amesema pia wanategemea kuongeza idadi ya watoto wanaojiunga na elimu ya msingi kutoka asilimia 45 mpaka asilimia 100 itakapofika mwaka 2020.

    Elimu bure mpaka kidato cha nne ni ahadi iliyotolewa na Rais Magufuli wakati wa Kampeni.

    Akiongelea vyuo vya Ufundi, amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuingia kwenye uchumi wa viwanda, kwa hiyo elimu ya ufundi lazima ijielekeze huko.


  • BREAKING NEWSS::RAIA YEYOTE ATAKAYETOA TAARIFA ZA UHAKIKA NA KUFICHUA WATU WANAOKWEPA KURIPA KODI KUJINYAKULIA ZAWADI



    BREAKING NEWSS::RAIA YEYOTE ATAKAYETOA TAARIFA ZA UHAKIKA NA KUFICHUA WATU WANAOKWEPA KURIPA KODI KUJINYAKULIA ZAWADI

  • SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU HAZINA KUACHWA TUPU



    SERIKALI YAKANUSHA KUHUSU HAZINA KUACHWA TUPU
    Na Jovina Bujulu-Maelezo

    Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.

    Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.

    "Hazina inazo pesa za kutosha  na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu,  kununua mashine za BVR  kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi  na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu" alisema Bwa. Cheyo.

    Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.

    Aliendelea kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.

    Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi Trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.

    Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa.


  • BREAKING NEWS : RAIS MAGUFULI AMSIMAISHA KAZI KAMISHA MKUU WA TRA





    Aliyekuwa Kamishna wa TRA Rished Bade
    Rais John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi kamishna wa mamlaka ya mapato TRA Bw.Rished Bade na kumteua Bw.Philiph Mpango kukaimu nafasi hiyo.
    Taarifa kutoka ikulu zimesema kuwa uamuzi huo wa rais Magufuli umefuatia ziara ya waziri mkuu bandarini uliobaini upotevu wa makontena 349.
    Aidha rais Magufuli amemtaka Rished Bade kutoa ushirikiano kwa Philiph Mpango wakati uchunguzi ukiendelea.


  • BREAKING NEWS : WAZIRI MKUU AIBUA MADUDU YA UPOTEVU WA MAKOTENA 346 YENYE DHAMANI YA BILIONI 80


    BREAKING NEWS : WAZIRI MKUU AIBUA MADUDU YA UPOTEVU WA MAKOTENA 346 YENYE DHAMANI YA BILIONI 80
    Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
    Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo hakuyafurahia. 


  • Marekani Yaipa Kibano Tanzania .....Yaitaka Serikali itoe Maelezo Uchaguzi Zanzibar na Sheria ya Mtandao , Yatishia kusitisha Msaada wa Trilioni



    Marekani Yaipa Kibano Tanzania .....Yaitaka Serikali itoe Maelezo Uchaguzi Zanzibar na Sheria ya Mtandao , Yatishia kusitisha Msaada wa Trilioni

    Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) wa Marekani umeonya kuwa hali ya kisiasa Zanzibar na tukio la hivi karibuni la watu kukamatwa chini ya sheria mpya ya uhalifu mtandaoni yanaweza kuathiri vigezo vya kuiwezesha Tanzania kupata msaada.

    Katika barua ya MCC ya Novemba 19, ambayo imesainiwa na Naibu Makamu wa Rais wa Idara ya Operesheni ya Miradi kwa Afrika, Jonathan O. Bloom kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile, mfuko huo umetaka maelezo kuhusu utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar pamoja na ufafanuzi wa sheria ya uhalifu wa mtandaoni.

    "MCC inashukuru kwa uongozi na dhamira yako wakati wa mchakato mzima wa maendeleo ya mradi huu. Msaada wa dola milioni 472 (ambazo ni zaidi ya Sh trilioni moja), una nafasi kubwa ya kusaidia kuleta mageuzi katika sekta ya nishati na kuwaunganisha maelfu ya watu katika gridi.

    "Lakini mgogoro wa Zanzibar na ukamataji watu wa hivi karibuni kupitia sheria mpya ya uhalifu mtandaoni umetutia wasiwasi.

    "Kama ujuavyo, mataifa washirika wa MCC wanapaswa kuendeleza na kuonyesha dhamira ya utawala bora, ambayo ni pamoja na kufuata misingi ya demokrasia na kulinda uhuru wa kutoa mawazo. 
     
    "Hata hivyo, matukio ya karibuni yanaifanya MCC na wadau wetu kujawa na maswali kuhusu dhamira hiyo," inasomeka barua hiyo ya MCC iliyosainiwa na Bloom.

    Kwa mujibu wa barua hiyo, MCC inafuatilia kwa karibu nyendo za Serikali katika ushughulikiaji wa masuala hayo ya utawala bora, hasa kipindi hiki kuelekea mkutano wa mwezi ujao wa bodi ya mfuko huo.

    "Utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar kwa namna ya kuridhisha pande zote husika na haja ya kuiona Serikali ikifafanua hadharani nia yake na sheria ya uhalifu wa mtandaoni, kama vile kuchapisha utekelezaji wa kanuni zinazoakisi mchango wa mdau na kuonyesha dhamira ya kuendelea kulinda uhuru wa kutoa maoni, kutaisaidia MCC kuitathimini Tanzania kwa namna chanya juu ya kuendelea kwa dhamira yake ya kutimiza sharti la kufuzu kupata misaada," ilisema barua hiyo.

    Barua hiyo ilimalizia kwa kusema: "Wasiwasi huu ni kikwazo cha mipango yetu ya ushirika. Tunaamini utashughulikia wasiwasi huu ipasavyo na tunatarajia kupata jibu kutoka kwako."

    Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dk. Likwelile, hakupatikana na hata alipotafutwa kwa njia ya simu hakupokea.

    Pamoja na juhudi hizo, pia alipotumiwa ujumbe mfupi wa simu hakujibu, ambapo alipotafutwa Msemaji wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, kuhusu barua hiyo ya MCC, alisema hana taarifa na hajaiona.

    "Sina taarifa na wala sijaiona barua hiyo, hivyo siwezi kusema chochote labda mpaka nitakapoongea na bosi aniambie kama amepokea barua hiyo," alisema Mduma.

    Mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu, Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiwa nchini Marekani kuhudhuria shughuli za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN), alikutana na Mtendaji Mkuu wa MCC, Dana J. Hyde na watumishi waandamizi, akiwamo Makamu wa Rais wa Operesheni za mfuko huo, Kamran Khan.

    Katika mkutano huo, MCC ilitangaza kuwa Tanzania imetimiza masharti yote ya kupatiwa awamu ya pili ya fedha za maendeleo kutoka katika mfuko huo, kuanzia mwakani, zaidi ya dola za Marekani milioni 472.8, sawa na zaidi ya Sh trilioni moja za Tanzania.

    Katika mkutano huo, Rais mstaafu Kikwete, aliambatana na ujumbe wa maofisa kadhaa akiwamo Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Yusuf Omar Mzee.

    Katika awamu ya kwanza ya fedha za MCC, Tanzania ilipata dola za Marekani milioni 698 (sawa na Sh trilioni 1.46).

    Kama MCC wataridhika na maelezo ya Serikali kupitia Wizara ya Fedha, Tanzania itakuwa imepata jumla ya Sh trilioni 2.45 kwa awamu zote mbili kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka 10.

    Awamu ya kwanza ya fedha hizo zilitumika kujenga Barabara za Tunduma- Sumbawanga, Tanga-Horohoro na Namtumbo- Songea- Mbinga.

    Desemba 10, mwaka jana, Marekani pia ilibainisha hatua ya uamuzi wa utolewaji wa fedha za awamu ya pili za MCC utategemea hatua zitakazochukuliwa na Serikali kuhusu sakata la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 200 katika akaunti ya Tegeta Escrow.

    Uamuzi huo wa Marekani ambayo inafadhili miradi mingi ya mabilioni ya fedha nchini, ulionekana kama mtihani  wa pili kwa Rais mstaafu Kikwete, baada ya ule wa maazimio ya Bunge yaliyotaka viongozi wakiwamo mawaziri waliotajwa katika kashfa hiyo kuwajibishwa.

    Waliowajibishwa na Rais Kikwete ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa, Sospeter Muhongo na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

    Wengine ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.

    Chanzo: Mtanzania


  • Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.