July 09, 2014

  • DKT.MAGUFULI AZOA WANACHAMA WAPYA 350 HUKO MARA, AFUNGUA KOMBE LA LUGOLA



    DKT.MAGUFULI AZOA WANACHAMA WAPYA 350 HUKO MARA, AFUNGUA KOMBE LA LUGOLA
    Katika ziara yake Mkoani Mara Dkt.Magufuli alifanya ziara Kijiji cha Mwibara (M/Kiti - TLP), Kata ya Mwibara (Diwani-TLP) Jimbo la Mwibara (Mbunge - CCM). 
    Akiwa katika kijiji cha Mwibara alifungua kombe la Kangi Lugola kisha kuhutubia wananchi. Kwa upendo M/Kiti na Diwani wa kata ya Mwibara wote kutoka TLP- walimzawadia Mbuzi wawili. Aidha, Magufuli aliweza kuzoa wanachama wapya zaidi ya 200 kata ya Mwibara na akafanya mkutano kata jirani ya Iramba na kuzoa wanachama wengine zaidi ya 150. 
     Dkt.Magufuli aliweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja kwenye mfuko wa maendeleo wa jimbo hilo. Jimboni kwa Nimrodi Mkono alizindua kivuko kipya cha MV Mara kitakachofanya safari zake kati ya Jimbo la Mwibara (Iramba) kwenda Jimbo la Musoma Vijijini (Majita). 
    Kivuko hiki kimeigharimu serikali shilingi milioni 545.2. Awali wananchi walisafiri kilomita 240 lakini kwa kutumia kivuko hiki watatumia dakiki 30 tu, zaidi ya hapo nauli walikuwa wakilipa shilingi 2000/- kwa mtu mmoja lakini kwa kivuko hiki kipya nauli ni shilingi 500/- na wanafunzi bureee! 
     Dkt.Magufuli pia aliweza kukagua ujenzi wa barabar ya Bunda - Kisorya sehemu ya Kisorya - Bulamba inayojengwa kwa shilingi bilioni 51.1/-. 
     Waliohudhulia: Kangi Lugola (MB), Nimrodi Mkono(MB),Mhandisi Iyombe (Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi), Mhandisi Evarist Ndikilo (RC-Mwanza & Ag.Mara), Ester Bulaya (MB-Viti Maalum), Wenyeviti wote wa Bodi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Kamati ya Ulinzi ya Mkoa n.k
     Dkt.Magufuli akifungua michuano ya  kombe la Lugola kwa kupiga penati golikipa akiwa Kangi Lugola, wanaoshuhudia ni Mhandisi Iyombe (Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi),Mhandisi Evarist Ndikilo (RC-Mwanza & Ag.Mara). Matoke, Magufuli alifunga goli.
    Golikipa Kangi Lugola baada ya kupangua penati ya Magufuli...Hadi refa alishangilia!
    Dkt.Magufuli akizawadiwa Mbuzi wawili 
    Wananchi wakinyoosha mikono kuapa kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mwibara 
    Dkt.Magufuli, Mhe Kangi Lugola na Mhe Nimrodi Mkono wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa MV.Mara


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.