Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki akiungana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda walipoungana na
wananchi kufanya usafi katika mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam ili
kuepukana na ugonjwa uliozuka wa Dengue ambao umekuwa tishio wakati akizindua
zoezi la kufanya usafi jijini lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA
YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda pamoja na wananchi
walioungana nae, wakiangalia jinsi mto Mlalakuwa ulivyoharibiwa kutokana na mvua
zinazoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki (mbele) akiongozana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
kuvuka Mto Mlalakuwa kuongea na wananchi waliokuwa ng'ambo ya mto.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki akiwahimiza kuhama wananchi wanaoishi pembezoni wa Mto Mlalakuwa kutokana
na nyumba yao kubomoka na maji kama inavyoonekana.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda wakikagua mabanda ya mama
lishe yaliyopo pembezoni mwa mto Mlalakuwa ambayo kwa kiasi kikubwa yapo katika
hatarishi ya kuwapa wateja wao magonjwa yanayoambukiza.
Hapa wakijionea jinsi maji machafu
yanayotoka katika viwanda vilivyopo Mikocheni/Mwenge yakiingia katika Mto
Mlalakuwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki akiongea na mmoja ya viongozi wa Kampuni ya Coca Cola jinsi ya kuwasaidia
mama lishe wanaofanya biashara kuzunguka kiwanda hicho maana wapo katika
mazingira magumu yanayoweza kuchangia mlipuko wa magonjwa wakati wakizindua
zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’
lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki akitilia msisitizo suala la usafi kwa wakazi wa jiji ili kuepukana na
ugonjwa uliozuka wa Dengue ambao umekuwa tishio wakati akizindua zoezi la
kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’
lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakioungana
na viongozi wao kufanya usafi ili kuweka jiji salama.
Kila Mmoja akiwajibika.
Zoezi la usafi halikujali rangi wala
taifa...
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
akiongea na Mkurugenzi wa Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamiliton wakati akizindua
zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’
lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Mto Mlalakuwa ukiwa safi mara baada ya zoezi
kumalizika.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
(kushoto) wakizoa uchafu na viongozi wa manispaa ya Kinondoni akiwemo Mkurugenzi
wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Natty (kulia) wakati wa zoezi la kufanya usafi
lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni
mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa
Natty akiwa amebeba uchafu mara baada ya kumaliza kufanya usafi.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda
akiongea na Mkurugenzi wa Kampuni ya Nabaki Afrika, Hamiliton pamoja na wananchi
wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO
WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es
Salaam.
Umati wa Wananchi waliohudhuria katika
shughuli hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nabaki Afrika,
Hamiliton akitoa shukrani zake za pekee kwa wananchi waliofika kufanya usafi
pamoja.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Nipe Fagio, Said
Swale akiongea machache.
Mc Taji Liundi nae alipata nafasi ya kuongea
macache.
Viongozi wa makampuni mbali mbali
waliohudhuria wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la
‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’
0 comments:
Post a Comment