Wananchi wakifuatilia kikao cha baraza la madiwani Wilaya ya Mbarali.
Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Modest Kilufi akichangia jambo kwenye mkutano wa Baraza.
Baraza la Madiwani la Wilaya ya Mbarali likiendelea na kikao.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Kenneth Ndingo akiongoza kikao cha baraza la madiwani.
**************************
HATIMAYE
Baraza la Madiwani Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya limefuta ushuru wa
mazao wa shilingi elfu mbili kwa gunia uliokuwa ukitozwa kwa wakulima
Wilayani humo ili kuepusha mgogoro ulokuwepo.
Kufutwa
kwa ushuru huo kumekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro
kupokea malalamiko kutoka kwa Wakulima wa Wilaya ya Mbarali ambao
walidai kutozwa ushurukwenye mpunga ambao umevunwa kwa ajili ya chakula
na siyo biashara.
Mkuu
wa Mkoa aliagiza kuitishwa kwa Baraza la dharula ili kujadili
mustakabali wa suala hilo, ambapo Baraza lilitii agizo na kufanya kikao
Mei 27,mwaka huu katika ukumbi wa Maji Mbarali na kuamua kutengua
ushuru huo uliokuwa umepitishwa na Madiwani hao.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Keneth Ndingo, katika hotuba yake
alisema Halmashauri inatakiwa kufikiria vyanzo vingine ili kuziba pengo
hilo ambalo ni hasara ya zaidi ya shilingi milioni 640.
Alisema
Baraza limeridhia kupunguza mawakala wa kukusanya ushuru kutoka kumi
wa awali na kubakia wanne ili kuleta ufanisi wa mapato na kurahisisha
udhibiti wa mapato ili kuondokana na hati chafu ya ukaguzi.
Alisema
katika mpango mpya kutakuwa na kanda mbili za makusanyo ambazo ni
kutoka Tarafa ya Rujewa na Tarafa ya Ilongo na kila Tarafa kutoa
mawakala wawili watakaokusanya ushuru kwa ufanisi na kuboresha mapato ya
Halmashauri.
Mmoja
wa wakulima Christopher Uhagile aliyehudhuria kikao hicho maalumu
alimpongeza mkuu wa Mkoa Abbas Kandoro kwa kuchukua hatua za haraka
kuitisha Baraza hilo kwani amani ilitoweka kutokana na mkanganyiko
uliojitokeza baada ya kuanza utekelezwaji wa sheria ya ukusanywaji wa
ushuru kwa mkulima.
Baadhi
ya Madiwani walimlalamikia Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Modestus Kilufi,
kuwa kitendo cha kuhoji ushuru uliopitishwa na baraza ni usaliti.
Walisema
mkulima kutozwa ushuru wakati yeye ni mjumbe wa Baraza na alikuwa
miongoni mwa wajumbe waliopitisha mkulima kutozwa ushuru wa mazao hivyo
hakupaswa kuhoji chochote kwani kauli hiyo ni ya kuwachonganisha
wakulima.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Gullam Hussein Kiffu aliwataka
watendaji wote wa Halmashauri na Madiwani kushirikiana ili kukusanya
mapato yatakayowezesha Halmashauri kujiendesha na kuleta maendeleo kwa
wananchi.
NA MBEYA YETU
0 comments:
Post a Comment