May 28, 2014

  • WATUHUMIWA WALIOMFICHA MTOTO KWENYE BOKSI WAFIKISHWA MAHAKAMANI


    WATUHUMIWA WALIOMFICHA MTOTO KWENYE BOKSI WAFIKISHWA MAHAKAMANI
    Mtuhumiwa Mtonga Omari akitoka mahakamani huku 
    mikono ikiwa kichwani akijutia Unyama anayodaiwa  kumfanya mtoto huyo wa marehemu shemeji yake aliyefahamika kwa jina la Mwasiti Said.
    Watuhumiwa wa mtoto anayedaiwa kufichwa kwenye boksi, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi  mjini Morogoro, kujibu mashtaka ya kula njama na kufanya ukatili dhidi ya mtoto huyo.watuhumiwa hao waliofikisha mahakamani hapo chini ya Ulinzi mkali ni Rashid Mvungi (47), washtakiwa wengine katika kesi hiyo iliyovutia umati wa watu wa mji wa Morogoro ni mama mlezi wa Nasrah, Mariamu Said (38) na mume wake Mtonga Omar (30).


    Baba mzazi wa Nasra Bw Mvungi aliyevaa shati la karoakiingia kwenye mahabusu ya mahakama ya mkoa akisubiri kupelekwa gerezani baada ya kushinda kutimiza masharti ya dhamana,Wananchi waliokuwepo mahakamani hapo walifurahia watuhumiwa hao kupelekwa magereza baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
    Hatimaye wale 
    Washtakiwa hao walifikishwa katika mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mary Moyo, Jumatatu ya wiki hii  na kusomewa mashtaka hayo.
    Wakili wa Serikali, Sunday Hyera alidai kuwa washtakiwa  walitenda makosa hayo kati ya Desemba mwaka 2010 na Mei mwaka huu katika mtaa wa Azimio kata ya Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro.
     Wakili huyo alidai kuwa katika kipindi hicho, washtakiwa wakiwa walezi wa mtoto Nasrah, walimfanyia ukatili wa mtelekeza na kumpa malezi akiwa ndani ya boksi na hivyo kumsababishia magonjwa.

    Wakili huyo wa Serikali, aliyataja maradhi yaliyokumba mtoto huyo akiwa ndani ya boksi kuwa ni pamoja na utapiamlo, maumivu ya kifua na mvunjiko wa mifupa katika mwili wake.
    Hyera alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama kutaja tarehe ya kuisikiliza.

    Hata hivyo Wakili huyo aliiomba mahakama kuwa upande wa Jamhuri hauna kipingamizi kuhusu dhamana kwa washtakiwa.
    Mahakama chini ya hakimu wake Moyo, ilisema dhamana kwa washtakiwa iko wazi lakini kwa masharti ya kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh5 milioni kila mmoja.
    Alisema  sharti lingine ni wadhamini kuwa na barua kutoka kwa waajiri wa kuaminika au serikali za mitaa.

    Hata hivyo washtakiwa walishindwa kutimiza masharti hayo, hatua iliyowafanya warejeshwa gerezani
    Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 9 mwaka huu itakapotajwa tena..


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.