Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.
Mchawi huyo alimhadaa mama                  huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya                  pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18. 
            
Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa kifungo cha                  miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya                  uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka. 
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, Chipeta                  alihukumiwa pamoja na mwenzake bwana Peter Christopher                  aliyepatikana na hirizi zinazotumika kufanyia uchawi.
Bwana Chipeta alimlaghai Bi Catherine Njeri hela                  zake tarehe tofauti tofauti kati ya mwezi wa Agosti na                  Decemba 2012 baada ya mwanamke huyo kuwaendea na                  kumwomba wazifanye pesa hizo ziwe maradufu
Walijitetea kwa kusema kuwa mwanamke huyo                  aliwaendea ili wampe nguvu za kichawi aweze kuwashinda                  wapinzani wake wa kisiasa
Maafisa wa polisi walipata hirizi hizo na vifaa                  walivyotumia kwa uchawi mwezi Februari 1, 2014 katika                  nyumba ya kukodisha iliyo kando ya barabara ya Juja                  viungani mwa mji mkuu Nairobi.
Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa                  wanaume hao waliona mwanamke huyo kuwa mjinga na basi                  kumnafiki kwa urahisi na kuwa hawana majuto au toba
chanzo:bbc
chanzo:bbc

0 comments:
Post a Comment