May 29, 2014

  • 26 wakamatwa kwa uvamizi wa mashamba



    26 wakamatwa kwa uvamizi wa mashamba
    Na John Gagarini, Kibaha

    JUMLA ya watu 26 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kuharibu mazao ndani ya shamba.

    Pia watu hao wanatuhumiwa kuvamia mashamba na kuingia kwa jinai kukutwa na bangi kete 38 na gramu 250 za bangi pamoja na pombe ya moshi lita 30.


    Akithibitisha kwa kutokea tukio hilo alisema kuwa uvamizi huo ulifanywa kwenye vitongoji vitatu tofauti vya Mkonga, Mkombozi na Tambani wilayani Mkuranga.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP)Ulrich Matei alisema kuwa walitishia kwa Silaha aina ya mapanga.

    Kamanda Matei aliwataja watu hao kuwa ni Ikwabe Paulo (36), Mwalami Bakari (38), Shamte Hamisi (35), Penina Peter (19), Grace Chacha (35), Latifa Salum (20), Said Issa (20), Said Hassan (18), Ramadhani Hassan (28), Kwarami Kingwandala (23), Omari Abdallah (20) Jafari Salum (45), Daniel Martin (18), Omari sufiani (32), Mussa John (30), Ally Abdallah (18), Augustino Tadei (28), Henry Lazaro (35), Bakari Lazaro (18), Issa John (21), Nemesi Venacy (35), Omari Mohammed (20), Stanley Mchuwa (28), Anthony Mchuwa (30).

    Aidha kamanda Matei aliongeza kuwa watu wengi waliokamatwa kwenye msako huo uliongozwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mkuranga Mrakibu (SP) Thobias Mapalala ni Grace Isafonce (18) na Helen Joseph (43) ambao walikamatwa wakiwa na Bangi Kete 38 na bangi nyingine ikiwa kwenye bakuli ya gram 250 huko eneo katika Kitongoji cha Mkombozi kata ya Tambani tarafa ya Mkuranga.

    "Watuhumiwa hao pia walikutwa wakiwa na Pombe ya Moshi (Gongo) lita 30 kwenye nyumba yao pamoja na muhuri ulioandikwa Mjumbe wa Shina namba 47 tawi la Shubani  Dar es Salaam ambao unasadikiwa ni wa kugushi wakiutumia kwa lengo la kutapeli mashamba," alisema kamanda Matei.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.