May 27, 2014

  • Ujumbe wa watu watano kutoka Makumbushoya Utamaduni, Malindi Kenya watembelea Sauti za Busara




    Ujumbe wa watu watano kutoka Makumbushoya Utamaduni, Malindi Kenya watembelea Sauti za Busara
    Ujumbe wa watu watano kutoka Makumbusho ya Utamaduni, Malindi Kenya ukiongozwa na kiongozi wao, Ghazzal Swaleh, jana walitembelea Ofisi ya Sauti za Busara, mjini Zanzibar, kujifunza mbinu za kuinua vipaji vya wasanii wa utamaduni wa kiafrika baina ya Zanzibar na Kenya, kuona mafanikio ya Tamasha la Utamaduni la Sauti za Busara Zanzibar na kudumisha mahusiano mema baina ya Zanzibar na Kenya. Ujumbe huo ulifanya mazungumzo kwa kubadilishana mawazo na Viongozi wa Sauti za Busara.
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Machano Othman Said (kushoto) ambaye alitoa mwaliko kwa wageni hao (kulia) kutembelea Zanzibar, akitoa utambulisho baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Sauti za Busara, Maisara mjini Zanzibar jana.
    Uongozi wa Saui za Busara Zanzibar ukiongozwa na Dj.Yussuf (wa pili kulia) ukielezea mafanikio ya Saui za Busara kwenye mkutano huo na ujumbe kutoka Kenya jana.
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Machano Othman Said (wa tatu kushoto) akikabidhi machapisho ya Mpango Mkakati wa miaka mitano ya Sauti za Busara kwa kiongozi a ujumbe huo kutoka Malind Kena, Ghazzal Swaleh. Kushoto ni Mwenyekiti wa Sauti za Busara, Simai Mohamed Said na Dj.Yussuf.
    Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar, Simai Mohamed Said (kulia) akizungumza kwenye kikao na ujumbe kutoka Makumbusho ya Utamaduni, Malindi nchini Kenya alioembelea Ofisi hizo, Maisara mjini Zanzibar jana. Picha na Martin Kabemba


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.