May 28, 2014

  • Taarifa mpya ya yule mwanamke anayesubiri kunyongwa Sudan, ajifungua mtoto akiwa gerezani.


    Taarifa mpya ya yule mwanamke anayesubiri kunyongwa Sudan, ajifungua mtoto akiwa gerezani. sudanYule mwanamke wa Sudan ambaye anasubiri kutumikia adhabu ya kifo baada ya kuisaliti dini yake, amejifungua mtoto akiwa gerezani karibu na mji wa Khartoum kwa mujibu wa mwanasheria wake.
    Mwanamke huyo Meriam Yehya Ibrahim Ishag, aliolewa na mwanaume wa kikristu na amehukumiwa kunyongwa mapema mwezi huu baada ya kukataa kuuacha ukristu.
    Mwanamke huyo ameruhusiwa kumhudumia mtoto wake huyo wa kike kwa miaka miwili kabla ya kutumikia adhabu hiyo.
    Meriam alizaliwa na baba wa kiislamu ambapo ameshtakiwa kwa sheria za kiislamu sharia. Sudan ina idadi kubwa ya watu wa jamii ya kiislamu inayoongozwa na sheria za kiislamu


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.