Katibu
Mkuu wa ICAO Bw. Raymond Benjamin akipata maelezo mafupi kutoka kwa
Kaimu Meneja Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga Bw. John Mayunga
alipotembelea Kituo cha Hali ya Hewa kilichopo katika uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Katika ziara hiyo Bw Raymond
alipendezewa na jinsi Mamlaka ilivyoboresha huduma kwa kutumia
teknolojia ambapo wateja wanapata ‘flight Folders’ za taarifa za hali ya
hewa kwa njia ya kielekronikali (Aviation Information System (AIS).
Huduma hii ni moja ya maboresho yaliyofanywa na TMA katika kukidhi
matakwa ya wateja wa usafiri wa anga kwa kuzingatia sera ya ubora (QMS)
ya Mamlaka yenye kusisitiza uboreshaji wa huduma kulingana na mahitaji
ya wakati husika. TMA ni moja ya taasisi za hali ya hewa chache na za
awali kutunikiwa cheti cha ubora wa Kimataifa (ISO:9001:2008) katika
ukanda wa nchi za Afrika na kuendelea kukidhi matakwa ya kukimiliki
cheti hicho mpaka sasa.
0 comments:
Post a Comment