May 27, 2014

  • 20 WAFARIKI KATIKA AJALI YA TRENI INDIA

    Treni
    Maafisa wa huduma za treni nchini India wanasema kuwa takriban watu 20 wanahofiwa kufariki katika ajali ya gari moshi katika jimbo la Uttar Pradesh.
    Treni hiyo ya kubeba abiria iligongana na treni ya jizigo iliyokuwa imeemgeshwa katika kituo cha treni cha Chureb.
    Mabehewa sita ya treni hiyo ya Gorakhdham Express yaling'oka kutoka kwenye treni hiyo.
    Waokozi wanajaribu kuwaokoa abiria waliokuwa ndani ya treni hiyo na ambao bado wamekwama.
    Treni hiyo ilikuwa inasafiri kutoka mjini Gorakhpur hadi katika jimbo la Hisar Haryana.Chanzo BBC Swahili
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.