Serikali inatarajia kuweka katika mtaala wa elimu unaotumika sasa, somo la afya ya uzazi kwa vijana katika shule za msingi na sekondari nchini kupunguza mimba za utotoni na maambukizi ya Ukimwi.Hayo yalisemwa jana, Dar esSalaam na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Jenista Mhagama katika ufunguzi wa mkutano wa siku tatu kuhusu
serikali imeweka mikakati ya kuanzisha elimu hiyo ya afyaya uzazi na
jinsia kwa vijanakatika shule za msingi kutokana na ukubwa wa tatizo
la mimba za utotoni namaambukizi ya Ukimwi."Serikali inawahakikishia
wanasayansi kuwa elimu hiyo itawapa matokeo chanya kwamba hakutakuwa
na maambukizi wala mimba za utotoni kwa vijana hao,'' alisema Mhagama
katika hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi Msaidizi wa
masuala mtambuka katika wizara hiyo, Letisia Sayi.Mhagama alisema
elimu ya afya ya uzazi kwa vijana itasaidia kubadili tabia, kujikinga
kwa kutumia kondomu na wanaoishi na maambukizi kulinda afya zao.Naye,
Mtaalamu wa kitaifa wa masuala ya Ukimwi na elimu ya afya wa Shirika
la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Martin Herman alisema takwimu
za wizara hiyo zinaonesha wanafunzi 6000 kila mwaka wanaacha shule kwa
sababu ya mimba za utotoni.Herman alisema mpango huo wa kutoa elimu ya
afya utaanza Julai mwaka huu baada ya mapitio ya mtaala huo na
inatarajiwa ifikapo mwaka 2015 wanafunzi watajua afya ya uzazi na
kupata walimu waliobobea katika masomo hayo.Nchi zilizoshiriki mkutano
huo ni pamoja na Afrika Kusini, Kenya, Sweden, Uganda, Malawi,
Zimbabwe, Zambia, Burundi, Namibia, Rwanda, Botswana,
Lesotho,Swaziland, Angola, Ethiopia na wenyeji Tanzania
0 comments:
Post a Comment