Kampuni
ya Google inaanza kutengeneza magari yanayojiendesha yenyewe badala ya
kuboresha vyombo vya moto vilivyotengezwa na makampuni mengine.
Magari hayo yatakuwa na vitufe vya kusimama na kujiendesha bila kuendeshwa na mtu,wala kuwa na usukani.
Picha
za gari hilo zinaonyesha kuwa gari hilo ni kama mfano wa magarimengine
ya mjini yenye muonekano mzuri, yaliyobuniwa kuyafanya yasitishe na
kufanya watu wayakubali na kukubali teknolojia hiyo mpya.
Mgunduzi msaidizi wa magari hayo, Sergey Brin amebainisha mipango hiyo jijini California.
Lakini pamoja na hatua hiyo, watafiti wanachunguza juu ya uwezekano wa kutumika kwa teknolojia hiyo mpya.
0 comments:
Post a Comment