Baadhi ya wanakijiji na Wanausalama wakifuatilia kwa Makini Kikao hicho.
*******
UONGOZI wa Kijiji
cha Ikhoho Kata ya Maendeleo Wilaya ya Mbeya unatuhumiwa kufuja fedha
za michango ya maendeleo zaidi ya shilingi milioni tatu zilizochangwa na
wananchi pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.
Tuhuma
hizo zilitolewa jana mbele ya mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini
hapo ambao ulihudhuriwa na Polisi Tarafa,Mkaguzi wa Polisi Galusi
Ligula, pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji aliyeondolewa madarakani, January Mwambole na Mtendaji wa Kijiji, Wakaa Nkembo.
Wakizungumza
kwenye mkutano huo wananchi wamedai kuwa kwa kutumia madaraka yao
viongozi hao waliwatoza wanafunzi 45 wa shule ya msingi ya kijiji hicho
shilingi 525,000/- wanafunzi wakidaiwa kuvunja choo cha shule.
Walisema
Wanafunzi 40 walitozwa shilingi elfu tano kila mmoja katika ofisi ya
kijiji na wanafunzi watano wakilipa shilingi elfu sitini na tano katika
Kituo cha Polisi cha Inyala ambapo waliwekwa mahabusu kabla ya wazazi
wao kulipa pesa hizo.
Waliongeza
kuwa kwa kutumia madaraka yao viongozi hao walianza kuwaandama wananchi
waliokuwa wakihoji uhalali wa tozo hilo ambapo kijana mmoja
aliyefahamika kwa jina la Bahati Kitundu alifunguliwa jalada la kutishia
kufanya fujo kijijini kutokana na kuandika barua ya malalamiko kwa Mkuu
wa Wilaya ya Mbeya juu ya kero za michango mbalimbali Kijijini hapo.
Wananchi
hao walisema mbali ya pesa za choo cha shule ya Msingi viongozi hao
wanatuhumiwa kutafuna michango ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Ikhoho
ambazo walikusanya kutoka kwa wananchi na kutoziwasilisha sehemu husika
kwa muda mrefu na baadhi ya wananchi walikamatwa kwa kushindwa kutoa
pesa hizo kwa wakati.
Aidha
katika mkutano huo Jeshi la Polisi lilitumia fursa ya kutoa elimu kwa
wananchi kutotumia mabavu katika shughuli za maendeleo na viongozi
watimize majukumu yao.
Baada
ya kumalizika kwa mkutano huo wananchi hao waliazimia kuunda tume ya
watu watano kwa ajili ya kujiridhisha na tuhuma hizo kabla ya
kuwasimamisha kazi viongozi wa Kijiji
Na Mbeya Yetu
0 comments:
Post a Comment