May 27, 2014

  • MHE.VICK KAMATA ALILIA NDOA YAKE, WABUNGE NAO WALILIA MICHANGO YAO

    Mheshimiwa Ummy Mwalimu alipopata nafasi ya kwenda kumtembelea hospitali shosti yake, Vicky Kamata.
    Na Mwandishi Wetu, Dar.
    Sakata la Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya UVCCM, Mkoa wa Geita Vicky Kamata sasa limeingia katika ukurasa mpya baada ya kuzinduka na kuanza kulilia ndoa yake huku nako wabunge mjini Dodoma wakililia michango yao.
    Kwa mujibu wa paparazi wetu aliyefika hospitali alipolazwa mbunge huyo ili aweze kujua hali inavyokwenda na wananchi wanazungumzia suala hilo, alidadavua kuwa kwa sasa Mbunge huyo amekuwa akililia ndoa yake.
    "Yani kila mmoja anaongea lake kuhusiana na sakata hili ila nimeweza kuongea na ndugu wa karibu anasema kwa sasa ndugu yao analilia ndoa yake japo sisi tumesema hatutaki hata kumuona tena huyo mwanaume anayeitwa Charles maana ndiye chanzo cha yote haya yaliyotokea," alisema ndugu wa karibu wa Mheshimiwa Vicky huku asitake kutajwa jina lake.

    Wananchi waliongeza kuwa hili lililomtokea mheshimiwa huyo ni dogo tu kufuatana na mambo ambayo amekuwa akiyafanya, "Sisi Wananchi tunaamini kila unalolifanya duniani malipo yake ni hapa hapa duniani hakuna haja ya kuficha ficha mambo... huyu mheshimiwa amezidi kubeba beba waume za watu na inafikia mpaka anavunja ndoa sasa hili lililomkuta ni fundisho kwake, ona sasa alivyoumbuka aibu hii ataipeleka wapi??? wananchi hao walihoji huku wakisema hilo ni fundisho kwa wote wenye tabia kama ya kwake.

    HUKO DODOMA:

    Pamoja na yote yaliyojitokeza, habari zinadai kwamba baadhi ya wabunge waliochanga pesa ili kufanikisha harusi hiyo tangu juzi wameanza kuulizia michango yao wataipataje kwa vile harusi basi tena!

    “Huku Dom (Dodoma) hakukaliki bwana. Baadhi ya wabunge wameanza kuulizia michango yao, wanasema kama harusi haipo basi na chao wakipate,” alisema mbunge mmoja akiomba kuhifadhiwa jina.

    Ndoa ya Mheshimwa Vicky Kamata na Charles ilikuwa ifungwe Mei 24, 2014 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza jijini Dar haikuweza kufungwa kutokana na kuwekewa pingamizi kuwa muoaji alikuwa ni Mume wa Mama Mwenye watoto 2.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.