Mkurugenzi
wa Msama Promotins Alex Msama (kulia), akiwa na Mratibu wa Tamasha la
Pasaka John Melele, wakifurahia kusafiri na Jet 103 ndege ya ATCL hivi
karibuni.
SERIKALI
kupitia Wizara ya Uchukuzi inayoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe
inastahili, pongezi kwa kupiga hatua kubwa kujenga na kuimarisha sekta
ya usafirishaji wa anga nchini.
Mkurugenzi
wa Msama Promotins Alex Msama, ametoa pongezi hizo siku chache baada ya
Wizara hiyo kuendelea kuonesha mafanikio makubwa katika utoaji wa
huduma za anga nchini.
Msama
ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu amewahimiza Watanzania kujawa na
uzalendo na hivyo, kuliunga mkono Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa
kutumia huduma zake zilizoboreshwa ili liweze kupambana na changamoto
mbalimbali zilizopo katika sekta ya usafirishaji wa anga nchini.
Alisema
hatua ya Wizara ya Uchukuzi kuwekeza katika usafiri wa anga inapaswa
kuungwa mkono na kila Mtanzania kwa maslahi ya taifa.
“Huduma
zinazotolewa na ATCL sasa ni nzuri na zenye ubora unaolingana na
mazingira ya sasa, hivyo ni vema sisi Watanzania tujivunie; kila
Mtanzania anapaswa kujivunia na kutumia huduma za shirika hilo.”
Hata
hivyo, alitoa rai kwa makampuni, taasisi zote za serikali na mtu mmoja
mmoja kutumia ndege ya shirika hilo linalofanya safari zake katika mikoa
mbalimbali nchini. Kwamba hatua pekee ya kuongeza ufanisi wa ATCL ni
watu kutumia chao na kukilinda na kukituza.
Mpaka
sasa ATCL ina ndege mbili ikiwamo ya Jet 103, ambazo kwa muda mfupi,
zimeonesha ufanisi wa hali ya juu katika utoaji huduma wa safari za
anga.
Aliongeza
kuwa amefurahishwa na huduma ya Ndege ya ATCL itokayo Dar kwenda Mwanza
ambapo alisema kuwa ndege hiyo ni nzuri na pia huduma zake ni nzuri na
ikiwa angani inatulia mpaka unajisahau kama upo ndani ya ndege.
Aidha
alisema kuwa ni vyema kila mtanzania akatumia ndege hii kwani kwa ndege
zote alizopanda kwenda Mwanza hii ni ndege bora zaidi.
Pia
amewaasa Watanzania kuwa wazalendo kama wenzetu wakenya ambao wamekuwa
wazelendo kwa kutumia ndege zao kila wafanyapo safari, na hivyo ni vema
watanzania kutumia ndege za ATCL ili kusaidia shirika hilo kutoka ndege
mbili hadi kuongeza ndege zaidi.
0 comments:
Post a Comment