August 20, 2015

  • KIPINDUPINDU TISHIO DAR



    KIPINDUPINDU TISHIO DAR


    Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam


    HALI ya ugonjwa wa kipindupindu imeanza kuzua hofu Dar es Salaam, Tanzania na kusababisha kutolewa kwa amri ya kutouzwa chakula na matunda.

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick, leo ameawaambia waandishi wa habari kuwa ni marufuku uuzwaji wa vyakula, matunda na hata kuhudhuria katika misiba na matanga ya watu waliobainika kufa kwa ugonjwa wa kipindupindu.
    Kwa mujibu wa Sadick, hadi sasa ni watu 56 wamepatikana na ugonjwa huo baada ya kufanyiwa vipimo.
    Ameyataja maeneo ambayo wagonjwa hao wametoka kuwa ni Kjitonyama, Kimara, Makumbusho, Kigogo, Manzese, Tandale na Mwananyamala katika Manispaa ya Kinondoni.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.