ALIYEKUWA mbunge wa Igunga, Rostam Aziz, (CCM), amefiwa na baba yake Aziz Abdulrasool (73) jijini Dar es Salaam jana asubuhi.
Akizungumza
nyumbani kwa marehemu Oysterbay jana, mtoto wa pili wa marehemu, Akram
Aziz, alisema baba yake alifariki saa 12 asubuhi ikiwa ni saa mbili tu
baada ya kurudishwa nchini kutoka Ufaransa alikuwa anatibiwa.
“Baba
amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa
saratani,tumemrudisha nchini jana saa 10 alfajiri kutoka Ufaransa,
lakini ilipofika saa 12:30 alifariki dunia.
“Baada
ya kugundulika kuwa na saratani, alianza matibabu Nchini Ufaransa na
Kurudi hapa Nyumbani…Mara ya mwisho baba alipelekwa nje miezi miwili
iliyopita, lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya akaomba tumrudishe
nyumbani ili awe karibu na ndugu na mafariki zake,”alisema Akram.
Marehemu
alizikwa jana katika makaburi ya Kisutu, saa 10 jioni jijini Dar es
Salaam na amewacha wajane watatu,watoto 17 na wajukuu nane.
0 comments:
Post a Comment